Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je Iran itajiunga na Hezbollah katika vita na Israel?
Tunaanza ziara yetu ya kusoma magazeti na gazeti la Israel "Yedioth Ahronoth" na makala ya maoni iliyoandikwa na Nadav Eyal, yenye kichwa "Je Iran itajiunga na Hezbollah katika vita dhidi ya Israel?" Ambayo anaanza kwa kurejelea hofu ya kuanzisha shambulio la Iran kwa kuunga mkono Hezbollah ikizingatia uwezekano wa kufanya operesheni dhidi ya Jeshi la Israel kaskazini.
Mwandishi huyo anasema jambo baya zaidi kuhusu hilo ni kwamba “Israel na Marekani hazina mpango madhubuti endapo makubaliano hayataafikiwa kuhusu kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas.
Wakati ambapo Ikulu ya White House inataka vita kukoma, kila kitu kingine kimekuwa cha pili katika mpangilio.
Hii sio maono ya nguvu kubwa ya maendeleo.
Mwandishi huyo anaongeza kuwa, baada ya Washington kuiunga mkono Israel kwa takriban miezi saba, ikiwa ni kipindi kirefu kuliko vita vingine vya Israel huko nyuma, Rais wa Marekani, Joe Biden, ana mawazo yake ya kisiasa, na tatizo kubwa zaidi limekuwa ni kwamba Marekani, bila kujali uchaguzi, haina mkakati wa muda mrefu wa kukabiliana na Iran na washirika wake wa kikanda.
Mwandishi anaibua maswali ambayo anayataja kuwa ya dharura zaidi: Ikiwa Hezbollah itaendelea kufyatua risasi kaskazini na Israel ikaingia kwenye vita vikubwa zaidi huko, vipi vita vikali vitaweza kuendelea upande wa kusini, kwa kutilia maanani nguvu kazi ya jeshi la Israel na hifadhi ndogo?
Iwapo jeshi la Israel litaanzisha uvamizi wa ardhini ndani ya Lebanon na Hezbollah kushambuliwa, je Nasrallah atakata fundo linalounganisha Gaza na Lebanon?
Mwandishi anasema kwamba uwanja wa vita kwa Israeli unahama kutoka kusini kwenda kaskazini, akibainisha kuwa jeshi na Waziri wa Ulinzi, Yoav Galant, wameazimia kujaribu kurudisha makumi ya maelfu ya wakaazi wa Israeli kaskazini .
Mwandishi anaamini kuwa kuna uwezekano mara tatu, wa kwanza ni usitishaji vita na utulivu, ambao ni uwezekano ambao jeshi la Israeli linaona kuwa hauvutii, ikimaanisha kuwa vita vinasimama kusini.
Uwezekano wa pili uliopendekezwa na mwandishi unahusu kufikia makubaliano kusini, ikiwa ni pamoja na kurudishwa kwa mateka, na kutumia dirisha hili kuanzisha operesheni ya kijeshi nchini Lebanoni.
Jeshi la Israeli linapendelea chaguo hili kwa sababu makubaliano yatakomboa vikosi kutoka kusini, lakini uwezekano wa kisiasa wa hii kutokea ni mdogo, kwani wale wanaosimamisha vita Kusini kwa kawaida hawangefanya hivyo kuanzisha vita ngumu zaidi Kaskazini.
Mwandishi huyo anasema katika operesheni hiyo, Hezbollah inatarajiwa kurusha maelfu ya makombora mazito na sahihi kiasi katika maeneo ya kaskazini, Haifa na kwingineko, na hata pale pande zote mbili, Israel na Nasrallah, zitakapoamua lengo lao, Israel inatarajiwa kushuhudia viwango vya juu zaidi vya uharibifu, na mashirika ya kijasusi ya Magharibi yanakadiria kuwa Iran huenda ikaungana na kuishambulia Israel katika vita kamili na Hezbollah.
Mwandishi anaangazia kauli iliyotolewa na chanzo chenye hadhi ya juu cha Israel, ambacho ni, “Ikiwa ilidhaniwa hadi sasa kwamba Hezbollah ingejiunga ikiwa tutaishambulia Iran, basi kuna hitimisho kwamba Iran itajiunga ikiwa tutaishambulia Hezbollah kwa kina. ”
Mwandishi anaongeza kuwa kuna changamoto nyingine ambazo lazima zizingatiwe. Kwa kuzingatia ripoti kwamba Marekani inaendelea kuchelewesha kuwasili kwa silaha kwa Israeli, hata sasa, silaha hizi ni muhimu kwa vita vya Lebanon.
Mwandishi huyo anasema dhana iliyomo ndani ya taasisi ya usalama ya Israel ni kwamba kuna mafanikio makubwa ya kimbinu, ambayo yanaweza kuongezwa iwapo kutahitajika kuanzishwa kampeni mpya ya kijeshi katika eneo la kaskazini, na kuashiria hali ya wasiwasi ndani ya jeshi la Israel, kuanzishwa kwa vitisho vipya na miuungano ya pande za mbali, hasa Iran.
Mwandishi anazungumzia hofu kubwa kwamba Gaza itageuka kuwa shimo jeusi, na kuvutia madola muhimu zaidi kwa Israeli, wakati vitisho vikali vinaendelea mashariki na kaskazini, na hii itaendelea kusababisha uharibifu mkubwa wa kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na mvutano katika mahusiano na Umoja wa Mataifa.
Nadav Eyal anahitimisha makala yake kwa kubainisha kwamba Waisraeli kwa mara nyingine tena wameingia katika mtego wa kuahirisha mambo, jambo ambalo linamtofautisha Waziri Mkuu wa sasa wa Israel, kwa sababu hafanyi hivyo.
Mchezo wa Kujadiliana na Moto"
Tunaligeukia gazeti la Saudia "Asharq Al-Awsat", na bado tuko kwenye makabiliano kati ya Israel na Hizbullah, msimamo wa Iran, na makala iliyoandikwa na Iyad Abu Chakra yenye kichwa "Kuhusu hali ya Lebanon ... Mwandishi anabainisha kuwa Israel haijatimiza sehemu kubwa zaidi ya mpango wake wa kuharibu makazi katika Ukanda wa Gaza, na mwelekeo wake wa kutibua hali katika nchi za Magharibi.
Benki, vipengele vya mamlaka ya vita vya Israel vinazidisha vitisho vyao kwa Lebanon.
Mwandishi huyo anasema kwamba, kwa upande mwingine, uongozi wa Iran unajibu kwa njia yake na namna ya kawaida kuimarika kwa Israel, “ukitiwa nguvu na ufahamu wake thabiti kwamba Marekani, mamlaka ya kimataifa inayoikumbatia na kuiendesha Israel, haizingatii kuwa katika hali ya vita nayo.
Badala yake, kama tunavyoona, inawaachia wafanya mazungumzo na majenerali kudhibiti hali hiyo.
Mwandishi anaongeza kuwa wakati huo huo, Walebanon hawaonekani kuwa wamejifunza chochote kutoka kwa matukio ya zamani.
Wao “bado ni mateka wa fikira zao za kikabila na matakwa yao ya kidhahania ambayo yamethibitishwa mara kadhaa kuwa si sahihi,” hasa kwa vile siku zote wameshindwa kuelewa kipengele cha sababu katika siasa, siku zote wakichanganya kati ya sababu na matokeo.
Mwandishi anaamini kwamba "viongozi wa Israeli, ambao wanajua hasa wanachofanya kwa kupitisha 'sera ya uhamishaji wa ardhi i' kusini mwa Lebanoni, hawako mbali hata kidogo na kufikiria kusababisha ugomvi wa kimadhehebu na kuchora ramani mpya."
Anaongeza kuwa, kwa upande mwingine, mradi wa Iran umethibitisha, kwa upande wake, kwamba ni "suala ambalo uwezo wake wa kuandaa na kutekeleza mipango ya uhamishaji na makazi haupaswi kupuuzwa.
.”
'Uingereza haina usawa'
Tunahitimisha ziara yetu na gazeti la Uingereza la "The Guardian" na makala iliyoandikwa na mwandishi wa masuala ya sheria Haroun Siddiq yenye kichwa "Uingereza haina usawa wa kimaadili katika kutuma silaha kwa Israeli na misaada kwa Gaza." Mwandishi anaanza makala yake kwa taarifa iliyotolewa na shirika la Uingereza la Oxfam kuelezea ugavi wa Uingereza wa silaha kwa Israeli wakati wa kutoa misaada ya kibinadamu kwa Gaza.
Mwandishi huyo anasema kuwa Uingereza ilikataa wito wa kusitisha uuzaji wa silaha kwa Israel, jambo ambalo lilileta changamoto ya kisheria, kwani Oxfam siku ya Alhamisi ilipewa kibali rasmi cha kuingilia kati. Kwa Israeli na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, msimamo wa Uingereza "hauna mantiki."
Mwandishi anaongeza, akimnukuu afisa huyo katika mahojiano maalum na gazeti la The Guardian, kwamba iwe inasemekana ni vifaa au silaha kamili zinazouzwa, ni jambo la msingi, kwa sababu vifaa peke yake vinaunda vifaa hivi vinavyoua watu wengi wasio na hatia, na Uingereza lazima iache kuuza silaha hizi. Serikali haiwezi kutoa misaada ya kibinadamu na kuzungumza juu ya matarajio yake ya amani katika eneo hilo kwa wakati mmoja, na kisha pia kusafirisha mabomu. Hii ni ukosefu wa usawa wa kiakili na kimaadili.
Mwandishi anabainisha kuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher alisimamisha mauzo ya silaha kwa Israeli wakati wa Vita vya Lebanon, na Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan alisimamisha usafirishaji wa mabomu Julai 1982, na pia aliripotiwa kushtushwa na picha za watoto wa Kipalestina waliouawa wakati wa shambulio la bomu. Mnamo Agosti 12, ilifikia hatua kwamba alionya Israeli wakati huo kwamba uhusiano wote wa baadaye wa Marekani na Israeli ungekuwa hatarini ikiwa hali hii itaendelea.
Mwandishi anahitimisha makala yake kwa kubainisha kwamba takwimu za serikali zilizochapishwa wiki iliyopita zilionyesha kuwa Uingereza ilitoa leseni 108 kwa Israel kati ya mashambulizi ya Oktoba 7 na Mei 31, na hakuna ombi la leseni ya kuuza silaha lilikataliwa au kufutwa katika kipindi hiki cha muda. Serikali ya Uingereza ilikataa kutoa maoni yake kuhusu maelezo yaliyomo katika maandishi ya makala hiyo.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla