Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanaume ambao hawataki kupigania Ukraine
Ukraine haikidhi mahitaji yake ya wanajeshi.
Watu wa kujitolea hawatoshi. Nchi kila mara inahitaji kuziba nafasi ya makumi ya maelfu ambao wameuawa au kujeruhiwa. Wengine zaidi wamechoka, kufuatia mapigano ya miezi 18 baada ya uvamizi wa Urusi.
Lakini baadhi ya wanaume hawataki kupigana. Maelfu wameondoka nchini, wakati mwingine baada ya kuwahonga maafisa, na wengine kutafuta njia za kuwakwepa maafisa wa kuajiri, ambao nao wameshutumiwa kwa mbinu zisizofaa.
"Mfumo umepitwa na wakati," anasema Yehor. Alimwona baba yake akikabiliana na matatizo ya afya ya akili baada ya kupigana na Jeshi la Soviet huko Afghanistan.
Ndio maana hataki kupigana. Ameomba tusitumie jina lake halisi ili kulinda utambulisho wake.
Kwa kawaida, kabla ya uvamizi wa Urusi, wanaume ambao hawakutaka kufanya utumishi wa kijeshi wangepewa njia mbadala - kama vile kufanya kazi katika sekta ya kilimo au huduma za kijamii.
Chaguo hilo liliondolewa baada ya sheria ya kijeshi kuanza kutumika mwaka jana, lakini Yehor anadhani bado inapaswa kuzingatiwa.
"Kila hali ni ya mtu binafsi," abisha Yehor. "Ijapokuwa imeandikwa katika katiba kwamba raia wote wanaume wanapaswa kupigana, kwa maoni yangu, haiendani na maadili ya leo."
Hivi majuzi alitumwa kwenye kituo cha kuratibu askari baada ya kuzuiwa na polisi huko Kyiv, kwa tuhuma za kukwepa rasimu. Hatimaye aliruhusiwa kwenda nyumbani, baada ya thibitisha kwamba alikuwa na matatizo ya mgongo, lakini anahofia siku zijazo hataponea.
Kuna msamaha unaotolewa huduma, ikiwa ni pamoja na kuwa na afya mbaya, kuwa mzazi asiye na mwenzi, na kutunza mtu aliye katika hatari. Lakini wale wanaopatikana na hatia ya kukwepa rasimu wanakabiliwa na faini ikiwa watapatikana na hatia, au hata kifungo cha miaka mitatu jela.
"Kila mtu anapaswa kuruhusiwa kuchangia vita hivi hali yake ikimruhusu," anasema Yehor. "Ninawahurumia watu ambao wako vita, lakini sina jinsi ya kupigania kwa amani."
Njia inayotumiwa na Kyiv kuwaandikisha wanaume jishini imeshutumiwa kuwa ya kifisadi.
Rais Volodymyr Zelensky amemfuta kazi kila mkuu wa kanda ya kuajiri nchini Ukraine baada ya madai mengi kuibuka dhidi ya maafisa katika mfumo huo, ikiwa ni pamoja na kupokea rushwa na vitisho.
Mkuu mmoja wa jeshi huko Odesa alishutumiwa hivi majuzi kwa kununua magari na mali katika pwani ya kusini mwa Uhispania iliyogharimu mamilioni ya dola. Afisa huyo anaripotiwa kuwa na ufahamu wowote kuhusiana na wa hili.
Maafisa wa ulinzi wameiambia BBC kwamba makosa yanayodaiwa ni "ya aibu na hayakubaliki".
Uhamasishaji ndio sababu inayofawanya wanaume wengi walio chini ya miaka 60 kutoweza kuondoka Ukraine. Maelfu mara nyingi hujaribu kutoroka nje ya nchi, haswa kupitia milima ya Carpathia hadi Romania.
Kwa wale wanaoamua kusalia nchini, gumzo la mitandaoni huwasaidia kuepuka kuandikwa. Machapisho ya telegramu hutoa vidokezo kuhusu mahali walipo maafisa wa kuandaa rasimu na wapi wanashika doria. Kuna makundi ya mtandaoni katika mikoa na miji tofauti kote nchini, wakati mwingine makundi hayo huwa na zaidi ya wanachama 100,000 kila moja.
Maafisa katika vikundi hivi wanajulikana kama Zaituni, kwa sababu ya rangi ya sare zao. Watu wanaokutana nao kwa kawaida hukabidhiwa notisi zinazowaamuru wajiandikishe katika kituo cha urasimu, lakini kuna ripoti za wengine kuchukuliwa mahali hapo, bila kupewa nafasi ya kurudi nyumbani.
Wizara ya Ulinzi ya Ukraine inawahimiza watu kuweka maelezo yao kwenye hifadhidata ya kitaifa, na inasema kwamba ikiwa wataitwa watatumwa kwenye mpango ujao.
Lakini kuna madai ya maafisa kutumia mbinu kali au za kutisha. Pia kuna ripoti za wanajeshi kujikuta wako mstari wa mbele kwa mwezi mmoja tu wa mafunzo.
Mamlaka zinaonekana kutaka kurejesha imani ya umma.
"Ni sawa kuogopa," ni kauli mbiu ya kampeni yao ya hivi punde ya habari. Ni jaribio la kuchora ulinganifu kati ya hofu za utotoni na wasiwasi wa leo.
Katika kambi ya majira ya joto iliyoachwa huko Kyiv, raia wanafunzwa kuwakabili askari Urusi, hali ikiwalazimu. Wanashika doria kwenye njia kabla ya mkufunzi kupiga kelele, "Kikundi cha pili! Grenade!" Wanaume na wanawake walijitupa chini haraka.
Bunduki zao si za kweli, lakini kuna matumaini kwamba baadhi ya washiriki watajiandikisha kwa ajili ya jambo halisi. Anton, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 22, tayari ameamua.
"Vita vilipoanza, sikuwa tayari kuandikishwa," ananiambia wakati wa mapumziko ya kubingiria kwenye nyasi.
"Sasa lazima nijitayarishe kwenda vitani siku zijazo."
Anton anasema sio vyema watu waepuke rasimu, lakini anaelewa kwa nini mtu asingependa kupigana.
BBC ilimuuliza kama anahofia uwezekano.
"Bila shaka," anajibu, karibu anikate kauli. "Kila mtu anaogopa. Lakini ikiwa hali itazidi kuwa mbaya zaidi, sioni nikiendelea kukaa hapa Kyiv."
Ukraine imekaidi matarajio yote katika utetezi wake dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Mtazamo wa Moscow umelazimika kubadilika kutoka kuchukua nchi nzima hadi kujaribu kushikilia sehemu kidogo.
Lakini Ukraine inaendelea kuimarisha mipango yake.
Sio tu kwa mbinu yake ya kivita, ambao unaleta matokea chanya kuliko wengi walivyotarajia, lakini pia kwa jinsi inavyowahamasisha raia wake kupigana.
Bila shaka kuna hitaji lisilopingika, lakini pia ukweli usio na karaha kwamba, uwanja wa vita sio wa kila mtu.