Jinsi China na India zinavyoisaidia Urusi kukwepa vikwazo kwa kununua mafuta kwa bei nafuu

Chanzo cha picha, Getty Images
Urusi imepata wateja wapya wa sekta yake kubwa ya mafuta na gesi ambao wanaisaidia kukabiliana na vikwazo vikali vya kiuchumi iliyowekewa na nchi za magharibi.
Baada ya kuvamia Ukraine, Urusi ilibadilisha Saudi Arabia kama muuzaji mkuu wa mafuta kwa China.
Kremlin inasemekana ilitoa punguzo la bei kwa Beijing kwa bei yake ya mafuta na gesi, na kuiruhusu kupata soko la bidhaa ambayo haikuweza kuuza kutokana na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa dhini ya Moscow.
Pia iligeukia India: kabla ya uvamizi,1% ya mauzo ya nje ya mafuta ya Urusi yaliuzwa kwa nchi hiyo ua Asia, kufikia mwezi Mei, mauzo iliongezeka hadi 18%.

Chanzo cha picha, Reuters
Hii ina maana kwamba, licha ya kwamba Urusi imeshuhudia kupungua kwa mapato yake kutokana na mauzo ya mafuta na gesi, mapato kutoka kwa sekta ya nishati bado yanatosha kufadhili, pamoja na mambo mengine, juhudi za kijeshi ambazo uvamizi wa Ukraine unawakilisha.
Mafuta yaliyopunguzwa
Kulingana na data kutoka kwa Mamalaka ya Forodha ya China, uagizaji wa bidhaa ghafi ya Urusi - ikiwa ni pamoja na bidha inayokuja kupitia bomba la Bahari ya Siberia na Pasifiki - ilifikia tani milioni 8.42 mwezi uliopita.
Hii iliwakilisha ongezeko la 55% ikilinganishwa na mwaka jana, na kufikia viwango vya juu zaidi katika mwezi wa Mei.
Kampuni zinazomilikiwa na serikali ya China kama vile Sinopec na Zhenhua Oil zimeongeza ununuzi wao wa mali ghafi katika miezi ya hivi karibuni.

Chanzo cha picha, Reuters
Kampuni hizo zilipokea punguzo kubwa kutoka kwa Urusi, kwasababu wanunuzi wa Ulaya na Marekani walianza kususia mafuta na gesi ya Urusi kufuatia uvamizi huo.
Hii iliiacha Saudi Arabia katika nafasi ya pili kati ya nchi zinazosambaza mafuta kwa China, ikiwa na tani milioni 7.82.
Lakini Urusi sio nchi pekee iliyo na vikwazo ambavyo China inanunua mafuta: kulingana na data iliyochapishwa Jumatatu, Beijing ilinunua tani 260,000 za mafuta ghafi kutoka Iran mwezi uliopita, ununuzi wa tatu kama huo tangu Desemba.
Mianya ya kisheria
Kulingana na ripoti iliyochapishwa wiki iliyopita na Kituo cha Utafiti kuhusu Kawi na Hewa Safi (CREA), Urusi imeshuhudia kupungua kwa mauzo ya hidrokaboni tangu mwanzo wa kuwekewa kwa vikwazo.
Hata hivyo ripoti hiyo inaonya kwamba Moscow imepata mianya wa kisheria kuendelea kuuzanje.
Mojawapo itakuwa kusafirisha mafuta kwa nchi zinazokuwa, kama vile India, ili kuyasafisha, na kisha kuweza kutuma bidhaa hiyo iliyosafishwa kwa nchi za Ulaya.

Chanzo cha picha, Reuters
"Ripoti hiyo inasema mafuta zaidi ya Urusi inasafirishwa India kusafishwa na sehemu kubwa ya mafuta hayo yanapenyezwa katika masoko ya Ulaya," anasema mwandishi wa biashara wa BBC Theo Legget.
"Na huku Moscow ikitafuta masoko mapya na mafuta ya Urusi yakihamishwa kutoka kwenye mabomba hadi kwenye meli, ambazo nyingi wazo zinamilikiwa na makampuni ya Ulaya."
"Ili Urusi vikwazo dhidi ya Urusi viweze kufikia malengo yake, masuala kama haya lazima yashughulikiwe."
Kizungumkuti cha Ulaya
Muungano wa Ulaya (EU) unasalia kuwa mteja mkuu wa mafuta na gesi ya Urusi.
Inakadiriwa kuwa dola bilioni 59 kati ya dola bilioni 97 zilizopokewa na Urusi katika mauzo ya nje ya nishati katika siku 100 za kwanza za vita vya Ukraine zilitoka kwa EU.
Lakini haijafanikiwa kufikia makubaliano ya kupiga kabisa marufuku ununuzi wa hidrokaboni kutoka Urusi.
EU inapanga kuweka marufuku ya uagizaji wa mafuta ya Kirusi kuwasili kwa bahari kabla ya mwisho wa mwaka, kupunguza uagizaji kwa zaidi ya 60%.
Aidha, mwezi Machi, Jumuiya ya Ulaya ilichukua hatua ya kupunguza uagizaji wa gesi ya Urusi kwa angalau theluthi mbili katika kipindi cha mwaka mmoja.
Kwa upande wake, Marekani ilipiga marufuku kabisa ununuzi wa mafuta, gesi na makaa ya mawe kutoka Urusi, na Uingereza inatarajiwa kufanya vivyo hivyo kabla ya mwisho wa 2022.
Nini kinaweza kutokea?
"Pamoja na kupanda kwa bei ya mafuta," mwandishi wa BBC Business Global Dharshini David, anasema "sio madereva pekee wanaopanga foleni wanapoona punguzo."
David anaeleza kuwa India na Uchina zimeweza kuchukua fursa ya hali ya sasa nchini Urusi, lakini anaonya kwamba, kutokana na kuanza kutumika kwa vikwazo vya Ulaya na mpito kwa wasambazaji wengine, wakati mzuri wa usafirishaji wa Urusi utadumu kwa muda tu.
"Mapato ya mafuta ya Urusi tayari yameanza kushuka, na hii itaongezeka huku mataifa mengine yakitafuta vyanzo mbadala vya nishati."
















