Haidrojeni itapunguza utegemezi wa Ujerumani wa gesi ya Urusi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Vita nchini Ukraine vimepunguza sera ya nishati ya Ujerumani.
Tangu kuanza kwa vita Ujerumani imepunguza utegemezi wake kwa mafuta ya Urusi kutoka 35% hadi 12% na kwa gesi ya Urusi kutoka 55% hadi 35%.
Walakini, biashara ya nishati ni chanzo kikubwa cha mapato kwa Moscow. Katika kipindi cha miezi miwili ya kwanza ya vita, Ujerumani ililipa karibu €9bn (£7.7bn; $9.6bn) kwa uagizaji wa mafuta na gesi kutoka Urusi kwa mujibu wa Shirika la CREA la Finland.
Veronika Grimm ni profesa wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Erlangen-Nuremberg, na kwa sasa ni mmoja wa washauri watatu maalum wa Ujerumani kwa serikali ya shirikisho wa masuala ua uchumi.
"Tunahitaji kubadilisha na kuondoa vyanzo vyetu vya nishati haraka kuliko ilivyopangwa hapo awali," anasema. Ili kusaidia kufikia lengo hilo, Bi Grimm anataka taifa "kuboresha" matumizi yake ya 'haidrojeni.
Haidrojeni inaweza kuhifadhi kiasi kikubwa cha nishati, kuchukua nafasi ya gesi asilia katika michakato ya viwandani, na chembechembe za nishati za mafuta katika lori, treni, meli au ndege ambazo hazitoi chochote ila mvuke wa maji ya kunywa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Shauku ya Bi Grimm inazidi kupata nguvu. Kwa mujibu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati (IEA), kikundi cha utafiti wa nishati, nchi kadhaa zimechapisha mikakati ya kitaifa ya haidrojeni, au zinakaribia kufanya hivyo.
Licha ya hatua hizi za kuvutia, bado haijabainika kuwa matumizi makubwa ya haidrojeni yanaweza kufanywa kuwa ya manufaa.
Wakosoaji wanaonya kuwa wawakilishi wa sekta hiyo, ambao hutawala mabaraza mengi ya haidrojeni duniani kote, mara nyingi huegemea upande wa haidrojeni kwani huahidi ruzuku na kudumisha mahitaji ya vifaa kama vile mabomba, meli za mafuta na vingine.
Haidrojeni ya kijani huzalishwa kwa kutumia umeme kutoka kwa nishati mbadala ili kugawanya maji katika molekuli za haidrojeni na oksijeni kwa kutumia 'electrolyser'. Lakini hizo mashine na umeme wa kuziendesha zinabaki kuwa gharama.
Gharama hizi zina maana kwamba, kwa sasa, haidrojeni isiyo na uchafuzi kama hiyo huchangia asilimia 0.03% tu ya uzalishaji wa haidrojeni duniani, kulingana na IEA.

Chanzo cha picha, Getty Images
Haidrojeni ya gharama nafuu zaidi ya mara tano ya bei ni hsidrojeni ya kijivu, hii inatokana na gesi asilia, au katika baadhi ya matukio kutoka kwa mafuta au makaa ya mawe.

Marekani, Canada, Uingereza, Uholanzi na Norway zinaongoza kwa kusukuma matumizi ya haidrojeni ya bluu, kwa michakato ya maeneo ya mafuta na gesi kwa hifadhi ya muda mrefu, au kwa kile kinachoitwa urejeshaji wa mafuta ulioimarishwa ambao huongeza uchimbaji.
Lakini nchini Ujerumani, hata hivyo, picha ni iko tofauti.
Volker Quaschning, profesa wa mifumo ya nishati mbadala katika Chuo Kikuu cha Berlin cha Sayansi anakosoa mkakati wa haidrojeni wa Ujerumani: "Serikali ya Merkel iliitumia kama sill nyekundu kuficha kushindwa kwake katika masuala ya mpito wa nishati."

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo Januari, Waziri wa Uchumi wa Ujwerumani, Robert Habeck alitangaza mpango kabambe wa kutengeneza na kuongeza maradufu lengo la miaka miwili la uzalishaji wa ndani wa haidrojeni ya kijani kupanda kutoka MW 70 hadi 10 GW ifikapo 2030.
Lengo hilo linawakilisha robo ya lengo zima la Umoja wa Ulaya, EU la 40GW, na ni kubwa kuliko lengo la Ufaransa la 6.5 GW.
Kwa hivyo wakati uzalishaji huu wa ndani unaongezeka, Ujerumani inatazamia pia kupata haidrojeni kutoka nje ya nchi.
Andreas Kuhlmann, mkuu wa Wakala wa Nishati wa Ujerumani, (kampuni inayomilikiwa na serikali inayowezesha mpito wa nishati inayoratibu Baraza la Haidrojeni), anasema Ujerumani imeharakisha kwa kiasi kikubwa mazungumzo ya kimataifa ya kununua hidrojeni.
Hiyo inaweza kujumuisha kutengeneza mabomba ya haidrojeni ili kuunganishwa na kusini mwa Ulaya, ambapo hali nzuri ya nishati ya jua na upepo huruhusu uzalishaji wa bei nafuu wa haidrojeni.
Bw Habeck anatembelea wauzaji nishati nje ya nchi. Ndani ya wiki moja mwezi wa Machi, alisafiri hadi Norway ili kukubaliana juu ya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa bomba la haidrojeni.
Alitembelea Umoja wa Falme za Kiarabu kutia saini mikataba mitano ya ushirikiano. Nchi nyingine anazozitupia jicho bwana Habeck ni Ireland, Saudi Arabia, Oman, Chile, Namibia na Australia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ingawa anakubali hitaji la kuagiza haidrojeni kutoka nje, Bw Quaschning anakosoa baadhi ya matumaini ya Bw Habeck. "Kuagiza haidrojeni kutoka kwa mimea ya jangwa itakuwa ya dhaifu, isiyofaa na ya gharama kubwa," anaelezea.
Kila hatua katika msururu wa ugavi hutumia baadhi ya nishati asilia: kuondoa chumvi katika maji ya bahari ili kupata maji safi kama malighafi, uchanganuzi wa umeme, upitishaji maji kwa usafirishaji, usafiri kupitia meli ya mafuta, usafiri wa ndani kupitia bomba nchini Ujerumani na ubadilishaji upya wa haidrojeni kuwa umeme.
"Kwa pamoja, hatua hizi zingekutumia angalau 70% ya umeme uliozalishwa hapo awali jangwani," Bw Quaschning anasema.
Shinikizo liko kwa Ujerumani kuacha kutumia pesa nyingi kwa nishati ya Urusi, lakini itakuwa mchakato mgumu.
Wengi watakuwa na matumaini kwamba haidrojeni hurahisisha mpito huo kwa kutimiza ahadi yake wakati huu.













