Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, wanawake wanapokua anga za mbali wanakabilianaje na hedhi?
Hedhi ni changamoto kwa kila mwanamke. Lakini je nini hufanyika ikiwa wanawake watapata hedhi katika anga za mbali? Je, wanakabiliana vipi na suala hili? Nini kingetokea iwapo mwanaanaga mwanamke Sunita Williams, angelazimika kukaa angani kwa muda mrefu kwa ghafla na kuwa katika kipindi cha hedhi?
Kwa kawaida, wanawake wanaposafiri, huwa wafikiri kuhusu ya lini watapata hedhi na ikiwa ni lazima kusafiri wakati huo.
Sunita Williams pia aliingia angani kwa ajili ya safari ya anga za mbali ya ya siku nane lakini alilazimika kukaa huko kwa zaidi ya miezi 9. Wakati huo huo, Sunita Williams huenda alifikiria hilo au hakufikiria hili , kulingana na umri wake.
Lakini je, inakuwaje wakati mwanamke anapolazimika kuwa katia anga za mbali kwa miezi mingi angani kama yeye wakati wa siku za hedhi yake? Swali linatokea jinsi watakavyoshughulikia vipindi katika anga za mbali.
Kupata majibu sahihi kuhusu maswali haya, BBC imezungumza kwa mara ya kwanza na Dkt. Varsha Jain, 'daktari wa magonjwa ya wanawake wa anga za juu na ambaye amefanya kazi na NASA katika utafiti kuhusu afya ya wanawake angani.
Mnamo 2019, Dkt. Varsha Jain alizungumza na mwandishi wa BBC Emma Barnett kuhusu masuala haya.
Majibu ya Varsha Jain yamewasilishwa katika ripoti hii.
Nini cha kufanya ikiwa unapata hedhi kwenye anga za mbali?
NASA ilikabiliwa na maswali sawa na hayo ilipomtuma mwanaanga wa kwanza wa kike wa NASA, Sally Ride, katika anga za mbali.
Wanaanga wakati huo walisema tusiwe na wasiwasi juu hilo hadi shida itakapojitokeza. Lakini wahandisi walilazimika kufanya mipango yote. Walipaswa kukadiria ni padi (visodo) vingapi vya za usafi ambavyo mtu angehitaji.
Wakati huo, ilikadiriwa kuwa vitambaa hivyo vya usafi 100 hadi 200 vinge hitajika kwa wiki. Baadaye, niligundua kuwa sikuhitaji visodo vingi.
Hivi sasa, wanaanga wa kike hutumia tembe za kudhibiti uzazi ili kukomesha hedhi zao. Maadamu wana afya njema, hakuna shida katika kuzitumia.
"Pia natafiti njia za kuepuka kupata hedhi."
Mamia ya wanaanga kutoka nchi tofauti tayari wamekwenda angani, wakiwemo wanawake.
Mwanamke wa kwanza kwenda angani alikuwa Valentina Tereshkova kutoka Muungano wa Usovieti. Alipewa jukumu hili mwaka 1963.
Miaka 20 tu baadaye, shirika la anga za juu la Marekani NASA lilimtuma mwanaanga wake wa kwanza wa kike, Sally Ride, katia anga za juu.
Haya ndiyo maswali ambayo vyombo vya habari vilimuuliza Sally Ride alipoingia angani kwa mara ya kwanza.
Je, anga za mbali huwaathiri wanawake na wanaume kwa namna tofauti?
Jibu la Varsha Jain kwa hili lilikuwa, "Kuzoea mazingira ya anga ni sawa kwa wanawake na wanaume. Hata hivyo, kuna tofauti fulani."
Wanawake wanahisi kiwango fulani cha uchovu au kuishiwa nguvu wanapoenda angani. Hivi ndivyo inavyotokea kwa wanaume wanaporudi duniani.
Wanaume wana uwezekano mkubwa wa kupata matatizo ya kuona na kusikia baada ya kurudi kutoka anga za juu, wakati wanawake wana uwezekano mkubwa wa kupata matatizo ya shinikizo la damu.
"Bado haijajulikana ikiwa hii inatokana na tofauti za kisaikolojia na homoni. Uchunguzi wa kina kuhusu masuala haya utaleta uelewa mzuri wa mabadiliko ya afya yanayosababishwa na safari ya anga ya muda mrefu."
Je, una tatizo na vyoo?
"Kuna vyoo viwili kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga cha Juu. Hata hivyo, havikuundwa kwa kuzingatia masuala ya hedhi pia."
Mkojo wako hautapotea angani. Husindikwa tena na kutumika kutengeneza maji safi.
Hii ni kwasababu damu ya hedhi inachukuliwa kuwa ngumu. Vyoo kwenye kituo cha anga za juu haviwezi kutenganisha maji kutoka kwa hedhi, kwa hivyo maji ndani yake hayawezi kusindikwa tena.
"Kwa kuongeza, kuna baadhi ya vikwazo juu ya matumizi ya maji. Pia ni vigumu kudumisha usafi wa kibinafsi wakati wa hedhi unapokuwa katika anga za mbali."
Je, usafiri wa anga huathiri uzazi?
Dk. Varsha Jain anasema, "Hakuna ushahidi kwamba usafiri wa anga una athari yoyote katika uzazi."
Kuna wanawake na wanaume wengi ambao wamesafiri kwenda angani na wamepata watoto baada ya kurudi.
Hata hivyo, hatupaswi kusahau kwamba umri wa wastani wa wanawake wanaoanza safari ya anga za mbali ni miaka 38.
Ni uamuzi wao binafsi kuhifadhi mayai na mbegu zao za uzazi kwa ajili ya mimba zijazo. NASA haijaweka sheria zozote katika suala hili.
Wanaanga wako katika hatari ya kupata mionzi angani. Lakini hakuna habari juu ya athari kwenye uzazi.
Ubora wa mbegu za uzazi hupungua wakati wa kusafiri angani, lakini huongezeka tena baada ya kurudi Duniani. Madhara yake ya muda mrefu bado hayajajulikana.
"Wanawake huzaliwa na idadi ndogo ya mayai ambayo wanayo katika maisha yao yote. NASA inaunga mkono sana wanaanga ambao wanataka kuhifadhi mayai yao kabla ya misheni ya angani."
Je, unaweza kwenda katika anga za mbali?
"Nisingependa kutumia muda mwingi katika anga za juu kwasababu najua ya mabadiliko makubwa ya mwili yanayoweza kutokea ."
Mwili wa mwanadamu unaonekana kuzeeka haraka zaidi angani. Uzito wa mfupa hupungua. Haijalishi ni unajitunza vizuri kiasi gani au ni matibabu gani unayopata baada ya kurudi Duniani, bado huwezi kuepuka athari fulani.
Dk. Varsha Jain alisema, "Pia nataka kuiona Dunia kutoka angani. Hata hivyo, naiona kama lengo la muda mrefu. Kwa sasa, ninafanya kazi yangu ninayoipenda duniani."