Rais Zelensky: Raia wa Urusi wanaandaliwa kwa vita vya kinyuklia

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema maafisa wa Urusi wameanza "kutayarisha jamii yao" kwa uwezekano wa matumizi ya silaha za nyuklia, lakini akaongeza kuwa haamini kuwa Urusi iko tayari kuzitumia.
Katika mahojiano na BBC, Rais Zelensky alikanusha kuwa alihimiza mshambulizi dhidi ya Urusi, akidai kuwa matamshi ya hapo awali yalitafsiriwa vibaya.
"Lazima utumie mateke ya kuzuia," alisema, akimaanisha vikwazo, "sio mashambulizi".
Katika wiki za hivi karibuni, jeshi la Ukraine limekomboa tena maeneo makubwa ya ardhi katika mashambulizi yaliyofaulu ambayo yamewalazimu wanajeshi wa Urusi kuacha maeneo walioshikilia kwa muda mrefu.
Katika kile Kyiv inachokielezea kama jibu la Moscow kwa kushindwa kwake, Rais Vladimir Putin amejumuisha mikoa minne inayokaliwa kwa mabavu ya Ukraine.
Hatua hiyo iliopuuzwa na wengi kuwa haramu, imeibua hofu ya uwezekano wa kuongezeka kwa vita hivyo vilivyodumu kwa miezi saba.
Rais Putin na maafisa wengine wakuu wa Urusi wamependekeza kuwa silaha ndogo za kinyuklia na zile za kimbinu - zinaweza kutumika kutetea maeneo hayo, ingawa maafisa wa Magharibi wanasema hakuna ushahidi wowote Moscow iko tayari kufanya hivyo.
Akizungumza kwa lugha ya kiingereza katika afisi yar ais mjini Kyiv , rais Zelensky alisema: wanaanza kuandaa jamii yao. Hiyo ni hatari sana.Hawako tayari kuitumia lakini wanaaza kuwasiliana hawajui iwapo wataitumia au la . nadhani ni hatari sana hata kuizungumzia.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Halafu akizungumza kwa Lugha ya Ukraine kwa kutumia mfasiri: Tunachoona ni kwamba raia wa Urusi wanataka kusalia madarakani kwa Maisha ndio maana naona hatari ya kutumia silaha ya kinyuklia sio rahisi kama wanavyosema wataalamu , kwasababu wanaelewa hakuna kurudi nyuma baada ya kuitumia, sio tu kwa historia ya taifa lao bali wao wenyewe kibinafsi.
Hatahivyo alikana madai ya kutaka kushambulia Urusi wakati wa hafla moja ya mtandaoni siku ya Alhamisi akisema kwamba neno la Ukraine alilotumia lilieleweka vibaya.
Matamshi hayo ya awali yalipingwa na msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliyesema kwamba kuna mpango wa kuanzisha vita vingine vya dunia, huku Waziri wa masuala ya kigeni nchini Urusi, Sergei Lavrov akisema kwamba hiyo ndio maana Urusi ilikuwa na haki kuanzisha vita nchini Ukraine.
Baada ya ufasiri huo, rais Zelensky alisema, wao Warusi walitumia njia yao , kwa ajili ya manufaa yao wenyewe na kuamua kuifasiri kivyao.
Mahojiano hayo yalifanyika saa chache baada ya rais wa Marekani Joe Biden kusema kwamba tishio la Urusi kutumia silaha za kinyuklia lilileta karibu Armageddon{ mwisho wa dunia} zaidi ya muda wowote ule tangu mgogoro wa silaha nchini Cuba wakati wa vita baridi.
Rais Zelensky alisema kwamba hatua zilihitajika , kwasaabu vitisho vya Urusi vilikuwa hatari kwa dunia nzima . Moscow alisema ilikuwa imepiga hatua tayari kwa kukalia kinu cha kinyuklia cha Zaporizhzhia, ambacho ndio kinu kikubwa zaidi barani Ulaya ambacho rais Putin anajaribu kukifanya mali ya Warusi.
Takriban wanajeshi 500 wa Urusi wamewekwa kwenye kiwanda hicho, alisema, ingawa wafanyikazi wa Ukraine ndio wanaokiendesha.
"Ulimwengu unaweza kukomesha haraka vitendo vya wavamizi wa Urusi," Rais Zelensky alisema. "Ulimwengu unaweza kutekeleza kifurushi cha vikwazo katika masuala kama hayo na kuwalazimu waondoke kwenye kinu cha nyuklia."

Wakiwa wamewezeshwa na silaha za hali ya juu zinazotolewa na nchi za Magharibi, jeshi la Ukraine limepiga hatua kubwa mashariki na kusini, na kukomboa miji na vijiji hata katika maeneo ambayo Kremlin inadai sasa ni sehemu ya Urusi.
Rais Zelensky alisema majeshi ya Urusi yalikuwa yanapanga "mapambano ya kutosha", lakini kwamba Ukraine ilikuwa imepokea silaha - "Sitasema tunazo za kutosha sasa" - na wanajeshi wamepatiwa motisha ya kusonga mbele.
Hatua ya kusukumwa nyuma kwa jeshi la Urusi, jambo la aibu kubwa kwa Rais Putin, imesababisha ukosoaji usio wa kawaida kwa jeshi la nchi hiyo.
Katikati ya hasara hiyo, Rais Putin alitangaza sajili wa mamia kwa maelfu ya askari wa akiba, jambo ambalo lilisababisha maandamano ya kupinga vita nchini Urusi nakusababisha kuondoka kwa msafara mkubwa wa watu wenye umri wa kijeshi kwa mataifa ya kigeni.
Rais Zelensky amewataka Warusi "kupigania miili, haki na roho zao", akisema: "Watoto hao waliosajiliwa kuwa wanajeshi wa ziada sasa, wanakuja bila kitu. Bila bunduki au silaha. Wanatupwa hapa kama lishe ya mizinga ... Ikiwa wanataka kuwa. kebabs - sawa, waache waje Lakini ikiwa ni watu baada ya yote na wanafikiri kuwa hii ni maisha yao, wanapaswa kupigana.
"Kila kitu Putin anaogopa, na sio silaha ya nyuklia, anaogopa jamii yake," alisema. Anaogopa watu wake. Kwa sababu watu hao tu ndio wenye uwezo wa kuchukua nafasi yake siku hizi. Ondoa nguvu zake na kumpa mtu mwingine."
Alipoulizwa iwapo Rais Putin anaweza kunusurika katika ushindi wa mwisho wa Ukraine katika vita hivyo, alisema: "Sijali."












