Ni nchi gani ambazo mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria?

Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris amekuwa akikosolewa na maafisa kwa kutoa hotuba zinazopigia debe haki za wapenzi wa jinsia moja wakati wa ziara yake ya siku tatu katika bara la Afrika iliyokamilika hivi karibuni.

Bi Kamala alitembeleanchi tatu za Afrika Ghana, Tanzania na Zambia ambazo kwa pamoja zinawezimepiga marufuku mapenzi ya jinsia moja.

Bi Harris alilitaka bunge la Ghana kuwa na usawa kwa watu wote.

Bunge la Ghana limepitisha sheria inayoharamisha haki za uanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja na kupendekeza kifungo cha jela kwa wale wanaojitambulisha kama wapenzi wa jinsia moja au wanaotaka kubadilisha jinsia yao kinyume na ile waliyozaliwa nayo.

Spik awa bunge la Ghana, Alban Bagbin, alikosoa kauli ya Bi. Harris akiitaja kuwa ni kinyume na demokrasia na akawataka wabunge kutojali ushawishi wa mtu yeyote.

Nchini Tanznaia, waziri wa zamani a;likosoa uungaji mkono wa Marekani wa haki za wapenzi wa jinsia moja, na nchini Zambia, wanasiasa wa upinzani waitishia kuandamana kupinga ziara ya Bi Harris nchini humo.

Mapenzi ya jinsia moja na jinsi yasivyokubalika kisheria Afrika

Unapotazama taarifa kuhusu jinsi mapenzi ya jinsia moja yalivyopingwa miaka ya nyuma katika nchi hizi tatu za Kiafrika, ina uhusiana na namna hali halisi ya nchi tatu duniani ziivyoharamisha kisheria mapenzi ya jinsia moja.

Kwasababu kati ya nchi 60 zilizoharamisha mapenzi ya jinsia moja, nusu yake ziko katika bara la Afrika.

Nchi 32 za Afrika zina sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja, nyingi kati yake zikiwa ni za Kaskazini na Mashariki mwa Afrika.

Hathivyo, katika miaka ya hivi karibuni, baadhi yan chi katika bara la Afrika zimefanya mageuzi kuhusiana na haki za ngoni ya jisnia moja, na hadi nchi 223 zimeharalisha mapenzi ya jinsia moja.

Lakini wakati huo huo, baadhi ya nchi za Afrika zimeanza kutambua kisheria mapenzi ya jinsia moja kama uhalifu.

Hali ya sheria za mapenzi ya jinsi amoja barani Afrika

Mnamo mwezi wa Februari, 2021, rais wa Angola , Joao Llorenko, alifanya marekebisho kwenye sheria ili kuruhusu mapenzi ya kingono ya jinsia moja na kusaini sheria inayozuia ubaguzi wenye misingi ya mwelekeo wa kingono, mtu anaoamua kuuchukua.

Kuhusu Gabon, kulikuwa na sheria ambayo iliyafanya mapenzi ya jinsia moja kuwa uhalifu na kuwalazimisha wapenzi wa jinsia moja kufungwa kwa miezi 6 na kulipa faini kubwa, lakini sheria hiyo ilifutwa mwaka 2020.

Mahakama ya juu zaidi nchini Botswana iliamua kuwa mapenzi ya jinsia moja sio uhalifu tena, na Msumbiji na Ushelisheli zimerekebisha sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja katika miaka ya hivi karibuni.

Kuna nchi za Afrika ambako haki za mapenzi ya jinsia moja zimeboreshwa hivi karbuni, lakini pia kuna nchi za Afrika ambazo zimeimarisha zaidi sheria za kupinga mapenzi ya jinsia moja.

Kwa mfano katika nchi za Nigeria na Uganda zina sheria kali, na Uganda imekuwa ikikosolewa vikali kwa kupitisha sheria zinazopinga haki za matembezi ya wapenzi wa jinsia moja.

Katika baadhi ya nchi za Afrika, majaribio ya kuyatambua kisheria mapenzi ya jinsia moja kama kitendo kisicho cha uhalifu yamefeli.

Mwezi Mei 2019, Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya iliamua kuwa uhalifu wa mapenzi ya jinsia moja bado upo, na Februari 2023, iliamua kwamba marufuku dhidi ya haki za kukusanyika kwa wapenzi wa jinsia moja sio kosa, lakini ikasema mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja yataendelea kuwa haramu kisheria.

Mabadiliko ya hivi karibuni ya haki za wapenzi wa jinsia moja nje ya Afrika

Myanmar pia ni nchi ambamo mapenzi ya jinsia moja hayakubaliki kisheria na wanaobainika kushiriki huadhibiwa kwa kifungo cha miaka 10 gerezani.

Katika Asia, Singapore ilifanya marekebisho kuhusu marufuku ya ngono kati ya wanaume mwezi Disemba, 2022.

Katika mwezi huo huo, kisiwa cha nchi ya Barbados kiliondoa sheria inayoyafanya mapenzi ya jinsia moja kuwa uhalifu.

Taifa jingine la taifa la kisiwa, la Antigua na Barbuda, pia kilifanya mabadiliko mwezi Julai 2022 kwa kuharamisha kisheria mapenzi ya jinsia moja na kuyafanya kuwa kinyume cha sheria.

Unapotazama hali kimataifa, tunaona kwamba uhalalishaji wa kisheria wa mapenzi ya jinsia moja unaendelea kuongezeka, na kuna nchi 33 duniani ambazo zinatambua mapenzi ya jinsia moja sawa na ndoa ya watu wa jinsia tofauti, idadi ambayo sio kubwa sawa na ndoa za jinsia tofauti.

Afrika Kusini ni nchi pekee ya Afrika ambayo inatambua ndoa ya jinsia moja South isipokuwa visiwa vya Mayotte na Reunion.

Je kuna sheria dhidi ya mapenzi ya jinsia moja zilizobaki kwasababu ya ukoloni?

Nyingi kati yan chi ambazo kwa sasa zimezuia kisheria mapenzi ya jinsia moja zimekuwa na sheria hizi tangu nyakati zake za ukoloni.

Kati ya nchi 53 zilizokuwa makoloni ya Uingereza, ni nchi 29 ambazo zinasheria zinazopinga mapenzi ya jinsia moja.

Asilia, Sheria ya Uingereza inazuia tu mapenzi ya jinsia moja baina ya wanaume, lakini katika baadhi ya nchi huru, imezuia ngono ya jinsia moja baina ya wanawake.

Kulingana na sheria asilia ya Uingereza, ngono ya watu wa jinsia moja iliadhibiwa kwa kifo hadi kufikia mwaka 1861, na nchi ambazo bado zina adhabu ya kifo kwa watu wa jinsia moja ni Brunei, Iran Mauritania Saudi Arabia, Yemen na baadhi ya majimboya kaskazini mwa Nigeria yanaendelea kutoa hukumu ya kifo.

Nchini Sudan, koloni la zamani la Uingereza, mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja bado ni kinyume cha sheria, lakini adhabu ya kifo iliondolewa mwaka 2020.