Zifahamu nchi ambazo wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja hunyongwa

Watu wawili wa mwisho kunyongwa nchini Irani wanaweza kuwa ni Mehrdad Karimpour na Farid Mohammadi, walionyongwa mwishoni mwa Januari mwaka huu.

Karimpour alikuwa na umri wa miaka 32 na Mohammadi alikuwa na umri wa miaka 29. Walishtakiwa na mamlaka za Irani kwa makosa ya kulawiti, ambapo walikaa miaka sita kwenye hukumu ya kifo, kwa mujibu wa mtandao wa Wanaharakati wa Haki za Kibinadamu nchini Iran (HRAI), ambao unaripoti juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Iran.

Ugumu wa kupata data rasmi hufanya iwe vigumu kujua kama Mehrdad na Farid ndio waathirika wa hivi karibuni, lakini kinachowezekana ni kwamba hawatakuwa wa mwisho.

Septemba iliyopita, wanawake wawili wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, Zahra Sedighi-Hamadani na Elham Choubdar, pia walihukumiwa kifo nchini Iran kwa tuhuma zilizotajwa kuwa ni za "ufisadi" na biashara ya kusafirisha binadamu. Kwa sasa haijajulikana ni lini hukumu hiyo ambayo imelaaniwa na Umoja wa Mataifa itatekelezwa.

Katika Jimbo la Bauchi, kaskazini mwa Nigeria, mahakama ya Kiislamu iliwahukumu wanaume watatu hukumu ya kifo kwa kupigwa mawe kwasababu ya kujihsisha na apenzi ya jinsia moja. Ilikuwa mwezi Julai, ingawa hakuna kinachojulikana kama hukumu hiyo itatekelezwa au la.

Kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu wa jinsia moja kunaweza kuadhibiwa kwa adhabu ya kifo katika nchi kumi na moja duniani kote, kulingana na taarifa kutoka vyama tofauti na mashirika ya haki za binadamu.

Mapenzi ya jinsia moja unatajwa ni"Uhalifu" na hupewa majina tofauti kulingana na nchi na nchi, kwa mfano "uhalifu usio wa asili", "sodoma" au "matendo ya ushoga".

Adhabu pia inatekelezwa kwa njia tofauti: kunyongwa, kukatwa kichwa au kupigwa mawe. Katika baadhi ya maeneo inaonekana kutumika zaidi kwa wanaume.

Katika nchi sita za Brunei, Iran, Mauritania, Nigeria, Saudi Arabia na Yemen - kuna uhakika wa kisheria kwamba adhabu ya kifo ni adhabu iliyowekwa kisheria kwa vitendo vya ngono za jinsia moja.

Hii imeelezwa katika kanuni zao za adhabu, ingawa, kwa upande wa Nigeria, ni majimbo 12 tu ya kaskazini mwa nchi yanayosimamia adhabu hiyo na, huko Brunei, ambayo kwa sasa yanaomba kusitishwa.

Katika nchi nyingine tano - Qatar, Afghanistan, Pakistan, Somalia na Umoja wa Falme za Kiarabu - adhabu ya kifo inawezekana, kutokana na tafsiri yake ya sharia au sheria ya Kiislamu, ingawa sio uhakika wa kisheria na inaweza kupingwa, kwa mujibu wa jumuia ya watu wanaojihusisha na apenzi ya jinsia moja ya ILGA.

Iran na Saudi Arabia

Iran na Saudi Arabia ndizo nchi zinazoitumia mara kwa mara sheria ya kunyonga watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, Julia Ehrt, mkurugenzi mkuu wa ILGA World, anaelezea BBC Mundo.

Hata hivyo, kati ya nchi zinazoilazimisha adhabu hiyo, ni vigumu kujua ni ngapi zinazoitekeleza. Mbali na waathiriwa wa Irani, kuna takwimu kwamba mnamo Aprili 2019, angalau wanaume watano walinyongwa nchini Saudi Arabia kwa vitendo hivyo.

Walikuwa sehemu ya mauaji ya halaiki yaliyoratibiwa katika maeneo ya umma kote nchini ambapo wanaume 37 waliuawa. Wengi wao walituhumiwa kuwa majasusi au magaidi wanaofanya kazi nchini Iran, mashtaka ambayo ILGA na mashirika mengine yanaamini yanatokana na kuwepo kwao kwenye maandamano ya kuipinga serikali mwaka 2012.

Kulingana na nyaraka zilizoonekana na CNN, mmoja wa wanaume waliohukumiwa kwa ulawiti, alikiri chini ya mateso kwa kuwa na mahusiano na wengine wanne.

Nchi zinazoadhibu mapenzi ya jinsia moja

Ukiacha adhabu ya kifo, nchi 68 duniani zinakataza mapenzi ya jinsia moja, huku kukiwa na hukumu kuanzia miezi michache hadi miaka mingi jela, au hata adhabu ya viboko kama vile kuchapwa viboko hadharani. Hata hivyo, ni takwimu ambayo, kulingana na Julia Ehrt, inapungua kila mwaka.

“Kuna maendeleo katika suala la adhabu, hali inaboreka, na huu ni mwelekeo ambao tumeuona katika miaka ya hivi karibuni na hata miongo kadhaa,” anaeleza mkurugenzi huyo mtendaji wa ILGA World.

Katika muongo uliopita, nchi 16 zimeacha kuwashitaki watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ikiwa ni pamoja na Antigua na Barbuda, Saint Kitts na Nevis, Angola, Msumbiji, na hivi karibuni, Singapore.

Caribbean, kwa mfano, ndio eneo pekee katika bara zima la Amerika inaadhibu watu wenye mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja, ingawa kuna kesi za kisheria kupinga adhabu hizo. Indonesia imeacha kabisa kuadhibu

Kwa mujibu wa hesabu ya ILGA, nchi 63 wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa sasa zina sheria zinazolaani mapenzi ya jinsia moja, ukiongeza na maeneo mawili ambayo hayako huru: Gaza na Visiwa vya Cook. Aidha, nchi nyingine mbili, Misri na Iraq, zinaadhibu ingawa haiko kisheria. Indonesia ni nambari 68, ingawa bado haijabainika jinsi sheria yake mpya itakavyotafsiriwa.

Picha moja isiyofanana

Ingawa vyama vinakubali kwamba hali imeboreka ulimwenguni kote katika suala la haki za watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGTBI), picha haiko sawa.

Barani Afrika, ambapo nchi 35 bado zinaharamisha mahusiano ya jinsia moja, "na ambayo inachukuliwa kuwa moja ya maeneo magumu zaidi kwa watu wa LGTBI, kumeonekana kuna hatua ya kweli," anasema Alistair Stewart, mkuu wa uraghibishi na utafiti kutoka Human Dignity Trust, shirika la msaada wa kisheria lililopo Uingereza.

Stewart anataja Angola, Lesotho, Botswana, Msumbiji na Ushelisheli, nchi ambazo zimeacha kuadhibu ushoga.

Hata hivyo, Ghana, ambako tayari ni kinyume cha sheria, inazingatia sheria mpya ambayo inaenda mbali zaidi, na inaweza kupiga marufuku sio tu mapenzi ya jinsia moja lakini inawalenga pia wanaojitokeza kama wapenzi wa jinsia moja au wanaoonyesha uungaji mkono kwa jumuiya ya LGTBI.

Ikiwa itaendelea, jamaa, waajiri, wamiliki wa nyumba au marafiki wa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja wanaweza kuhukumiwa ikiwa hawataripoti kwa mamlaka.

Ingawa hali ya kisheria au ya kijamii ni tofauti sana kati ya nchi na nchi, anasema mwanaharakati wa Human Dignity Trust, wale wanaopinga haki za LGTBI hutumia maneno na hoja sawa, na hii inaonekana katika ukweli kwamba sheria inayozingatiwa nchini Ghana Inafanana sana kwa vipengele na sheria ambayo imeidhinishwa nchini Urusi.