Tetesi za soka Ulaya Jumapili 26.05.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Kevin de Bruyne huenda akasalia Manchester City, huku Sir Jim Ratcliffe akishindwa kutoa hakikisho kuhusu mustakabali wa meneja wa Manchester United Erik ten Hag...
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne anatarajiwa kuongeza mkataba wake Manchester City , licha ya washauri wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kufanya mikutano na vilabu vya Saudi Arabia. (Mirror)
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Deco anavutiwa na winga wa Liverpool Luis Diaz na klabu hiyo ya Uhispania inaweza kumuuza fowadi wa Brazil Raphinha ili kuwezesha kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia, 27. (AS - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mmiliki mwenza wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe hakujibu swali alipoulizwa iwapo meneja Erik ten Hag atasalia katika kazi yake kufuatia ushindi wa timu yake katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City. (Mail)
Mshambuliaji wa England Jarrod Bowen anataka kusalia West Ham huku Newcastle United ikihusishwa na kutaka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Mirror)
Kambi ya kiungo wa kati wa Uingereza Emile Smith Rowe itafanya mazungumzo na Arsenal kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 katika klabu hiyo kufuatia muda wake mdogo wa kucheza msimu wa 2023-24. (CaughtOffside)

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona wamewasiliana na kiungo wa kati wa Uhispania Thiago Alcantara, ambaye ataondoka Liverpool mkataba wake utakapokamilika Juni 30, ili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 kuwa kocha mchezaji na msaidizi wa anayetarajiwa kuwa meneja mpya wa Barca Hansi Flick. (AS - in Spanish)
Paris St-Germain wametoa ofa ya euro 100m (£85m) kwa mshambuliaji wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 na Napoli zikiwa bado kuafikiana kuhusu kuongezwa kwa mkataba mpya. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
PSG wanahofia kuwa nyuma ya Liverpool , Manchester United na Real Madrid katika mbio za kumsajili beki wa kati wa Lille Mfaransa Leny Yoro, 18, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2024-25. (L'Equipe - in French, subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle wanatazamia kukamilisha usajili wa walinzi wawili wa Uingereza kwa uhamisho huru - Lloyd Kelly wa Bournemouth, 25, na Tosin Adarabioyo wa Fulham , 26. (Football Insider)
Manchester United wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Port Vale Baylee Dipepa, 17. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza chini ya umri wa miaka 17 pia anasakwa na Newcastle United, West Ham, RB Leipzig, Borussia Dortmund na Aston Villa. (Mail)
Napoli wanawasiliana na Antonio Conte kuhusu kocha huyo wa zamani wa Tottenham na Chelsea kuchukua nafasi ya meneja wao mpya. (Sky Sports Italia)

Chanzo cha picha, Getty Images
Aston Villa wameweka bei ya kati ya £6-8m kwa kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 31, lakini pia watakuwa tayari kwa mkataba wa mkopo. (Rudy Galetti)
Leicester City wanatafuta kumnunua beki wa kati wa Feyenoord na Slovakia David Hancko, 26, huku wakijiandaa kurejea Ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao. (Mail)
Beki wa pembeni wa Uhispania Lucas Vazquez, 32, ambaye pia anaweza kucheza kama winga, anakaribia kukubali kuongezwa mkataba na Real Madrid ambao utamweka katika klabu hiyo hadi angalau Juni 2025. (Marca).















