Kwanini Michael Jordan hawezi kuuza jumba lake la kifahari kwa $29m

Chanzo cha picha, John Eckert
Kuwa mmoja watu tajiri zaidi na mchezaji aliyependwa zaidi na watu kuwahi kushuhudiwa haimaanishi kwamba Michael Jordan anaweza kuepuka matatizo ambayo wengi wetu tunakabiliana nayo katika kuuza malizetu.
Kwa miaka kumi, mchezaji huyo maarufu wa mpira wa kikapu amekuwa akijaribu kuuza jumba lake la kifahari lililopo katika Highland Park, mji uliopo katika jimbo la Marekani la Illinois, karibu kilomita 40 kutoka Chicago.
Jumba hilo lililojengwa na kukamilishwa katika mwaka 1995, lilikuwa ni makazi ya Jordan katika miaka ya 1990 , wakati alipoongoza timu ya Chicago Bulls kuchukua mataji matatu ya Shirikisho la mpira wa kikapu la taifa (NBA) na kupata malipo makubwa zaidi ya nyingi kupitia mikataba minono ya udhamini.
Jumba la kifahari la Highland Park ni jumba linalovutia hata kwa viwango vya watu maarufu. Likiwa na vyumba tisa na bafu 19 lina ukubwa eneo la mita za mraba 5,000 na lina maeneo muhimu kama vile sinema, eneo la mazoezi (gym), kiwanja cha tenisi, na uwanja kamili wa mpira wa kikapu

Chanzo cha picha, Getty Images
Pia kuna gereji kwa ajili ya magari 14.
'Densi ' nyingine sokoni
Jordan, ambaye alistaafu mchezo wa mpira wa kikapu mwaka 2003 na kwa sasa anaishi katika jumba jingine la kifahari katika Jupiter - mji uliopo katika jimbo la Florida, ametangaza wazi, kwamba jumba lake lililopo katika jimbo la Illinois limekuwa likitafutiwa mnunuzi tangu mwaka 2012.
Mwanzoni alitaka malipo ya dola milioni 29, lakini tangu wakati huo bei yake imepungua na kufikia hadi dola milioni 14, kama inavyoonyeshwa kwenye orodha ya wavuti wa Compass, mawakala wa makazi ambao wanajaribu kuuza jumba hilo la kifahari.

Chanzo cha picha, John Eckert
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Hatahivyo, jaribio la kwanza la kuliuza katika mnada kwa bei ya chini katika mwaka 2013 (dola milioni 13 ) pia lilishindikana.
Hata baada ya Jordan kupata mafanikio makubwa katika makala ya msururu wa kipindi cha Netflix -The Last Dance -ambapo alionyeshwa katika msimu uliopita kama mchezaji wa Chicago Bulls - haikumsaidia kuwapata wanunuzi.
Wataalamu wa makazi nchini Marekani wanaamini wanajua ni kwanini jumba lake la kifahari la Highland Park linaonekana kuwa "laana".
Mojawapo ya sababu zilizoelezwa kwa miaka mingi ni kwamba Highland Park yenyewe ni kikwazo: eneo lenyewe haliko karibu na katikati ya mji wa Chicago na halina hadhi ya bei inayofaa likilinganishwa na maeneo mengine katika eneo kama vile "Windy City".
Katika mahojiano na wavuti wa masuala ya kifedha wa Marketwatch, mshauri wa mali za kifahari Adam Rosenfield pia alisema kuwa jumba la kifahari la Jordan lilijengwa kwa hali ambayo haiwezi kumvutia kila mnunuzi. "Wakati unapokuwa na mali ya kipekee ya aina hiyo ambayo imejengwa kwa kuzingatia vigezo vya kibinafsi sana, itakuletea matatizo zaidi," alisema.
'Ni sawa na kununua sanaa'

Chanzo cha picha, John Eckert
Mtaalamu mwingine wa makazi, Michael Nourmand, alimueleza mwandishi wa jarida la Hollywood kwamba uthamanishaji wa mali za kifahari na zilizojengwa kulingana na jinsi mmiliki binafsi alivyotaka huwa changamoto kupata mnunuzi.
"Ni sawa zaidi na kununua sanaa," alisema.
"Ni sawa na kununua maziwa, ambapo unaweza kutazama mtandaoni na kuona ni kiasi gani ambacho kila mtu anauza ," Nourmand aliongeza.

Chanzo cha picha, John Eckert
Akikadiriwa kuwa na utajiri wa dola biloni 1.7 katika jarida la givi karibui la Forbes la orodha ya matajiri duniani na uwekezaji unaojumuisha ule alionao katika timu ya NBA ya Charlotte Bobcats, Jordan anakabiliwa na shinikizo la hadhi kuuza mali yake ya Illinois.
Bao alijiunga na orodha ya watu maarufu ambao wakati mwingine kupata kwamba nyumba za ndoto yao huwa haziwavutii watu wanaoweza kuzinunua.
Mchezaji filamu Tom Cruise alipata uzoefu kama huo baada ya kutangaza kuwa makazi yake ya Colorado dola milioni 59 mwaka 2014 . Aliweza kuyauza, lakini ni baada ya miaka saba baadaye na kwa bei ya chini zaidi ya ile aliyokuwa akiitaka yeye - aliuza kwa dola milioni 39.5 tu.












