Jinsi watu tajiri na maarufu wanavyolinda nyumba zao?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kufuatia kufungwa jela Ijumaa kwa mmoja wa wezi katika nyumba ya mchezaji wa zamani wa soka Ashley Cole- ambapo yeye na mwenza wake walifungwa na waya- tunaangalia je matajiri wanaomiliki nyumba wamejizatiti vipi kulinda nyumba zao?
"Tunatafutwa sana hilo ni kweli ," anasema John Moore, ambaye ni mkuu wa kampuni ya usalama - Westminster Security, kampuni ya kibinafsi inayofanya usalama wa kulinda nyumba katika maeneo ya kifahari kama vile Holland Park.
Eneo kama vile la Kensington, ambako majengo meupe ya kifahari yanauzwa mamilioni ya pesa, yamekuwa "kitovu hasa cha shughuli za uhalifu", anasema Bw Moore.
"Karibu kila usiku pale kuna tukio ... watu wakizurura kuanzia kama saa tisa usiku hadi asubuhi, kusema kweli bila malengo mazuri

Chanzo cha picha, Reuters
Nyumba ya mchezaji soka wa zamani wa England David Beckham na nahodha wake na mke wake Victoria ambaye ni mbunifu wa mitindo ya mavazi ilivamiwa wakati walipokuwa ndani yake na binti yao mwenye umri wa miaka 10. Polisi wa London walisema mali kadhaa ziliripotiwa kuibiwa.
Tukio hili lilifuatiwa na tukio jingine ambapo jumba la Tamara muuzaji wa vipuli ghali liliporwa na wgenge la wezi wa vipuli, walioiba vipuli, pesa, almasi na mawe ya samani yenye thamani ya pauni milioni 25.
Bw Moore anakadiria kuwa huwagarimu kiasi cha pauni kati ya £250,000 hadi £500,000 kwa mwaka – lakini kodi hupunguza gharama ya usalama iwapo tisho la usalama lijatokana na ajira ya mtu.
Alieleza kuwa : "Hakuna kupinga kwamba kulinda usalama ni ghali’’
"Wengi wa wateja wetu wanaona ulinzi kama uwekezaji, kwahiyo huwekeza katika usalama wa familia zao ."

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshawishi wa mitandao ya kijamii Molly-Mae Hague anaripotiwa aliimarisha usalama baada ya kupoteza mali ya thamani ya £800,000 mwaka jana katika makazi ya Manchester anamoishi na mpenzi wake mwanandondi, Tommy Fury.
Alisema "bila shaka ni kitu kibaya zaidi ambacho kimetokea kwake "katika video ya YouTube akitoa machozi.
Molly-Mae Hague mwenye umri wa miaka 22 alisema kutuma kwenye mtandao wa kijamii taarifa na picha za maisha yake ya kifahari huenda kulionyesha wafuasi wake na usalama wake.
Tangu wakati huo amesema hataonyesha kwenye mitandao yake ya kijamii ‘nyumbani kwake kamwe.
'Mbwa hawezi kupewa hongo'
Watu maarufu kadhaa wameweka mbwa wanne kulinda nyumba zao, akiwemo mwanamuziki wa rap Stormzy na wachezaji soka Jack Grealish na Jesse Lingard.
Robert Metcalfe, ambaye anaendesha kampuni ya mbwa wa ulinzi binafsi katika Nottingham, huwapatia mafunzo mbwa kuwalinda wat una mali zao.
Pia huuza mbwa wa ulinzi wa watu wa aina ya German Shepherds wenye thamani ya £10,000 kwa watu kama wanamitindo na Wan awa wafalme wa Kiarabu wanaoishi jijini London.

Chanzo cha picha, Personal protection dog
"Iwapo utanunua mbwa wa kijilinda binafsi, haiwezi kupewa hongo ," Bw Metcalfe anaelezea. "haiwezi kupokea pesa itoweke usiku
"Nilikuwa na ombi kutoka kwa mteja wiki moja iliyopita na akauliza bajeti
"Wakasema hawana bajeti- mali yake kwa ujumla ni ya thamani ya pauni bilioni mbili ."
Na ninini kinatokea wakati mbwa wa ulinzi wa kibinafsi anapomiga risasi mvamizi? "Unataka ibweke na iwazuie," alisema Bw Metcalfe.












