Je Israel itafanya nini baada ya kuiangamiza Hamas? elewa mpango mzima katika hatua 3

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Israel inasema lengo la muda mrefu la operesheni yake ya kijeshi huko Gaza ni kukata uhusiano wote na eneo hilo.

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Galant alitangaza siku ya Ijumaa kuwa Israel inakusudia kusitisha wajibu wote kwa watu wanaoishi katika Ukanda wa Gaza mara tu Hamas itakaposhindwa.

Kabla ya mzozo kati ya pande hizo mbili, Israel ilitoa mahitaji mengi ya nishati ya Gaza na kudhibiti uagizaji wa bidhaa katika eneo hilo.

Kauli ya Gallant inakuja wakati ambapo mashambulizi ya anga ya Israel yanaendelea huko Gaza.

Shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na Hamas nchini Israel liliua karibu watu 1,400 na kuwachukua mateka 200. Israel inalipiza kisasi kwa mashambulizi ya anga. Israel sasa inajiandaa kuanzisha mashambulizi ya ardhini dhidi ya Gaza.

Israeli itaifanya nini Gaza: Mpango wa Awamu 3

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Gallant alitangaza kwa kamati ya bunge siku ya Ijumaa kuwa:

  • Awamu ya kwanza ya kampeni itakuwa kuharibu miundo ya Hamas.
  • Pia aliongeza kuwa mpango wa mwisho utafanya 'operesheni za chini kabisa' ili kuondoa 'maeneo ya waasi'.
  • Katika awamu ya tatu , "wajibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza lazima ukomeshwe na kuundwa kwa utawala mpya wa usalama kwa ajili ya raia wa Israel."

Ni muhimu kukumbuka kuwa mnamo 2005, Israeli iliondoka Gaza. Umoja wa Mataifa unaichukulia Gaza kama eneo linalokaliwa kwa mabavu, pamoja na Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki, na kuiwajibisha Israel kukidhi mahitaji ya kimsingi ya watu wa eneo hilo.

Hapo awali Israel iliwaruhusu Wagaza kuvuka mpaka kufanya kazi. Pia ilidhibiti mauzo ya nje kwa kanda na kuhakikisha kuwa silaha hazifikii Hamas.

Je Gaza imepokea misaada ya kibinadamu?

Israel ilikata umeme hadi Gaza tangu shambulio la Oktoba 7. Kando na hayo, usambazaji wa maji, chakula na dawa pia ulisimamishwa. Lakini sasa msafara wa misaada umefika Gaza. Umoja wa Mataifa ulieleza hali hii kuwa mbaya sana.

Marekani na Misri zimefikia makubaliano ambayo yataruhusu baadhi ya misaada kuingia Gaza.

Msafara wa kwanza wa lori 20 uliingia kusini mwa Gaza Ijumaa iliyopita na kutumwa kupitia kivuko cha mpaka cha Rafah hadi mpaka wa Misri.

Wakati huo huo, mashirika ya kibinadamu yanasema kwamba msaada zaidi unahitajika huko Gaza.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitembelea kivuko cha mpaka siku ya Ijumaa na kusisitiza kuwa lori ziruhusiwe kuingia katika eneo hilo.

Alisema, “Hili si lori la kawaida tu. Ni nyenzo ya kuokoa maisha. Ugavi misaada ni uhai na kifo kwa watu wengi huko Gaza. Tunataka liruhusiwe kuingia.”

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati huo huo, rais wa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina, ambayo inasimamia Ukingo wa Magharibi, Mohammad Abbas, amezungumza juu ya kuwa na maoni tofauti na Hamas, na wakati huo huo, alishiriki pia katika mkutano huo unaofanyika huko Cairo siku ya Jumamosi. Mkutano huu ulifanyika kwa lengo la kusitisha mapigano.

Mkutano huo uliandaliwa na Rais wa Misri, Abdel Fattah el Sisi.

Mfalme Abdullah II wa Jordan, Mfalme wa Bahrain, Mwanamfalme wa Kuwait na Emir wa Qatar, Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Ulaya na maafisa wakuu wa Japan, Russia, China na Umoja wa Ulaya pia walishiriki katika mkutano huu.