Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afrika inaweza kuvunja kizuizi cha nusu fainali 'ikiwa tutawaunga mkono makocha wetu'
Timu za Afrika zitavunja kizuizi cha nusu fainali endapo bara hilo litakuwa na na imani na makocha wao, kulingana na kulingana na kocha wa klabu yenye sifa zaidi barani Afrika Pitso Mosimane.
Kwa mara ya kwanza tangu Kombe la Dunia lianze mwaka wa 1930, kutakuwa na makocha wa Afrika wote kwa timu kutoka bara katika fainali za kimataifa nchini Qatar.
Uteuzi wa Walid Regragui kama mkufunzi wa Morocco kuchukua nafasi ya Vahid Halilhodzic, inamaanisha kuwa mechi zote tano za kufuzu za Afrika zitaongozwa na kocha wa ndani.
Kocha wa zamani wa Wydad Casablanca anaungana na Jalel Kadri wa Tunisia na wachezaji wa zamani wa kimataifa Otto Addo (Ghana), Aliou Cisse (Senegal) na Rigobert Song (Cameroon) huku maandalizi ya michuano hiyo yakizidi kupamba moto kwa mechi za kirafiki.
"Kuwa na imani na makocha wa Kiafrika ni hatua kubwa na inaashiria hali nzuri ya ukuaji katika bara ambayo lazima iendelezwe," Mosimane aliiambia BBC Michezo Afrika.
“Hii si kampeni dhidi ya makocha wa kigeni bali ni pongezi kwa watoa maamuzi katika vyama vyetu vya kitaifa.
“Watu wengi wanauliza kwa nini timu za Afrika hapita hatua ya nane bora au kugombea taji lenyewe la Kombe la Dunia, na ninaamini hii ni hatua kubwa kuelekea kufikia lengo hilo.
"Kwa hakika Afrika inaweza kuvunja kizuizi hicho cha nusu fainali ikiwa tutawaunga mkono makocha wetu ambao wanaelewa kweli mawazo, changamoto za kitamaduni na mbinu zinazohitajika kufanya kazi."
Timu tatu tu za Afrika zimetinga robo fainali ya Kombe la Dunia kabla; Cameroon mwaka 1990 chini ya Valery Nepomnyashchy (Soviet Union, sasa Urusi), Senegal mwaka 2002 ikinolewa na Mfaransa Bruno Metsu na kisha Ghana mwaka 2010 na Mserbia Milovan Rajevac.
Mjadala wa kukosekana kwa nafasi kwa makocha wa Kiafrika katika nchi zao umekuwa kwa muda mrefu, huku mashirikisho mengi ya soka barani yakiangazia mataifa ya kigeni wakati wa kuteua kocha wa kitaifa.
Lakini hatua ya kuteua makocha wa nyumbani wakati huu ni mabadiliko makubwa kwa wenyeji, ambao wamegubikwa kwa muda mrefu na makocha kutoka Ulaya na Amerika Kusini kwenye fainali.
Kuongezeka kwa makocha wazawa
Kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya makocha wa Kiafrika wanaofanya alama zao katika bara lao.
Regragui ambaye anaongoza Morocco mara 45, natimiza umri wa miaka 47 siku ya Ijumaa, anachukua mikoba ya Atlas Lions baada ya kuwa na msimu mzuri katika ligi kuu ya Morocco ambapo aliiongoza Wydad kutwaa Ligi ya Mabingwa Afrika na kushinda taji la nyumbani.
Nahodha wa zamani wa Senegal Cisse amekuwa akiinoa Lions of Teranga tangu 2015 na kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 alisaidia Waafrika Magharibi kupata mafanikio ya kwanza katika bara mapema mwaka huu kabla ya kufuzu kwa mara ya pili mfululizo katika Kombe la Dunia.
Kadri, mwenye umri wa miaka 50, asaidia Tunisia kushinda Mali katika mechi ya mchujo na kutinga fainali ya sita baada ya kuchukua jukumu la kufuzu kwa hatua ya 16 bora kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu.
Baada ya kuichezea Cameroon katika Fainali nne za Kombe la Dunia, Song aliteuliwa kuwa Kocha wa Indomitable Lions mnamo Februari na kufanikiwa kufuzu kwa mara ya nane kwa fainali za kimataifa kufuatia ushindi wa mchujo dhidi ya Algeria.
Beki huyo wa wa zamani, 46, anatarajiwa kuwa Mcameroon wa pili, baada ya marehemu Leonard Nseke mwaka 1994, kuliongoza taifa hilo la Afrika ya Kati katika mashindano ya kimataifa.
Addo aliichezea Ghana katika mashindano ya 2006, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 47 alichukua mikoba ya Black Stars baada ya kutoka katika hatua ya makundi kutoka Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari.
Aliiongoza timu hiyo kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 2014 baada ya kuwashinda wapinzani wao wakali Nigeria kwa sheria ya bao la ugenini.
“Makocha wetu wanaokwenda Kombe la Dunia wamefuzu na wamejipanga vya kutosha kwa ajili ya jukumu hilo kwa sababu haliko nje ya uwezo wao,” alisema Mosimane.
Mmoja wa watu mashuhuri wa kandanda barani Afrika, nahodha wa zamani wa Super Eagles Stephen Keshi anasalia kuwa mmoja wa watu wawili pekee walioshinda Kombe la Mataifa ya Afrika kama mchezaji na kocha.
Ndiye Mwafrika pekee aliyefuzu mataifa mawili tofauti kwenye fainali za Kombe la Dunia - Togo mwaka 2006 na Nigeria 2014 - na kupata mafanikio ambapo Wazungu, mara nyingi huajiriwa kwa gharama kubwa, wameshindwa.
Katika fainali zilizofanyika Brazil mwaka wa 2014 aliiongoza Nigeria hadi raundi ya pili, na Keshi anasalia kuwa kocha pekee Mwafrika aliyeingia katika awamu ya muondoano ya Kombe la Dunia.
Keshi, ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 54 Juni 2016, aliwahi kuisuta Afrika kwa kuwategemea makocha wa kigeni, akisema ni kuua mchezo huo barani Afrika na kwamba wanapewa muda zaidi kuliko wenzao wa asili.
Kwa jumla, shindano kuu la kandanda barani Afrika - Kombe la Mataifa - limeshindwa na kocha wa njyumbani mara 16, na makocha wa kigeni wameshinda mara 17.
Kiwango hicho cha mafanikio kimemfanya Mosimane aondoe dhana ya muda mrefu kwamba hadhi ya makocha wa Kiafrika bado iko chini na hawapati heshima kutoka kwa wachezaji kama kocha wa kigeni.
"Alichofanya Keshi kwa kuwashinda mameneja wa kigeni alipokuwa akielekea kwenye mafanikio ya bara ni kuvunja dhana hiyo ya kocha Mwafrika," aliongeza.
"Pia aliweka msingi kwa wengine kufuata nyayo. Nadhani mafanikio yake ya hatua ya 16 pia yalipaza sauti ya uwezo wa makocha wa Afrika kote duniani.
"Washindi wawili wa mwisho wa Kombe la Mataifa ni Waafrika [Djamel Belmadi wa Algeria na Cisse wa Senegal] ambayo inaonyesha kuwa makocha wengi wa Kiafrika wamehitimu kama wenzao wa kigeni.
“Inachekesha kwamba watu wanaendelea kushikilia imani kuwa ni wageni pekee ndio wanaofaa kwa timu za Afrika, makocha hawa pia walichezea timu kubwa za Ulaya na kwingineko – wanafichuliwa na mawazo ya kisasa na wanastahili heshima ya wachezaji wetu, mashabiki, vyombo vya habari na wabishi wengine."
Mosimane, 58, aliiongoza Al Ahly kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa mara baada ya kujiunga nayo 2020, pamoja na mafanikio yake ya awali katika mashindano hayo akiwa na Mamelodi Sundowns mwaka 2016.
Kocha huyo wa zamani wa Afrika Kusini pia alifanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu mfululizo katika Kombe la Dunia la Klabu, ikiwa ni pamoja na toleo la 2021 lililochezwa Februari.
Kati ya timu tano za kitaifa zilizowakilisha Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018, ni Senegal na Tunisia pekee ndizo zilikuwa na makocha wazawa - Cisse na Nabil Maaloul.
Ingawa hakuna timu ya Kiafrika iliyofuzu hatua ya makundi nchini Urusi, Mosimane anaamini timu za bara hilo mara nyingi zinakabiliwa na maandalizi duni na usumbufu unaoweza kuepukika.