Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Jumapili: Marcus Rashford akubali mkataba na FC Barcelona
Mshambuliaji wa England, Marcus Rashford (28), amekubali mkataba wa miaka mitatu na FC Barcelona, na klabu hiyo ya Hispania inapanga kulipa kipengele cha kuachiliwa cha takribani pauni milioni 26 ili kubadilisha mkopo wake kutoka Manchester United kuwa uhamisho wa kudumu majira ya kiangazi.(Sport - in Spanish)
Mshambuliaji wa Senegal mwenye umri wa miaka 24, Nicolas Jackson, ambaye yuko kwa mkopo katika Bayern Munich, pamoja na mshambuliaji wa Guinea, Serhou Guirassy (29) wa Borussia Dortmund, ni miongoni mwa wachezaji ambao AC Milan inawania kuwasajili.(Gazzetta dello Sport - in Italian)
Aston Villa pia inavutiwa na Jackson huku ikipanga kumruhusu mshambuliaji wa England mwenye umri wa miaka 30, Ollie Watkins, kuondoka majira ya kiangazi.(Football Insider)
Real Madrid inataka kumsajili kiungo wa Manchester City mwenye umri wa miaka 29, Rodri, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania akitarajiwa kugharimu takribani pauni milioni 44.(Radio Marca)
Winga wa England, Anthony Gordon (25), amehusishwa na Arsenal FC, lakini badala ya taarifa kuwa amebakiwa na miaka miwili katika mkataba wake na Newcastle United, ukweli ni kwamba ana miaka minne.(Sky Sports)
Atlético Madrid na Juventus FC zimeungana na Newcastle katika nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uruguay mwenye umri wa miaka 26, Darwin Núñez, ambaye amepoteza nafasi yake katika klabu ya Al-Hilal ya Ligi Kuu ya Saudia.(Football Insider)
Juventus imemfanya mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27, Randal Kolo Muani, ambaye yuko kwa mkopo Tottenham Hotspur kutoka Paris Saint-Germain, kuwa lengo lake kuu la usajili majira ya kiangazi.(Tuttosport, via Football Italia)
Kocha wa zamani wa England, Gareth Southgate, amehusishwa na kuchukua nafasi ya ukufunzi Manchester United lakini amesema "hatafuti nafasi ya hiyo kwa sasa."(Football Boardrrom Podcast, via Star)
Kocha wa AC Milan, Massimiliano Allegri, amepuuza taarifa zinazodai kuwa anafikiria mustakabali wake katika klabu hiyo ya Serie A.(Football Italia)