Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Liverpool na Chelsea zaingia katika mbio za kumnunua Murillo wa Nottingham
Liverpool imo katika mpango thabiti wa kumnunua beki wa Nottingham Forest na Brazil Murillo, 23, ingawa Chelsea bado wanaongoza mbio za kumnunua mchezaji huyo. (TeamTalks)
Ripoti kwamba Jurgen Klopp ataacha jukumu lake kama mkuu wa soka duniani katika shirika la Red Bull "ni upuuzi mtupu na hazina msingi kabisa," anasema Mkurugenzi Mtendaji Oliver Mintzlaff. (Sky Sports Ujerumani - kIn Germany)
Mchezaji wa kimataifa wa Serbia Dusan Vlahovic anapendelea kuhamia Barcelona wakati kandarasi yake ya Juventus itakapokamilika msimu huu wa joto, ingawa Tottenham Hotspur na Chelsea bado wanawinda saini ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (TeamTalks)
Arsenal na Manchester City wanafikiria kuweka dau la £30m kumnunua beki wa kushoto wa Atalanta Honest Ahanor. Chelsea pia wanavutiwa na Mnigeria huyo mwenye umri wa miaka 18. (Caught Offside)
Liverpool na Manchester United hawatalipa bei ya Wolves ya pauni milioni 50 kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Mateus Mane mwenye umri wa miaka 18 msimu huu kwa sababu wanamchukulia kiungo huyo kuwa mbichi sana. (Football Insider)
Mshambulizi wa zamani wa Brentford Ivan Toney analenga kushinda mataji nchini Saudi Arabia na klabu ya sasa ya Al-Ahli, lakini Muingereza huyo, 29, hataki kurejea kwenye Ligi ya Premia. (Sportsport)
Mshambulizi Nicolas Jackson anatarajiwa kurejea Chelsea. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal mwenye umri wa miaka 24 alihamia Bayern Munich kwa mkopo msimu uliopita wa joto, lakini mabingwa hao wa Bundesliga hawataki uhamisho wa kudumu. (CFBayernInsider).
Newcastle United inamchunguza mlinda lango wa Brighton na Uholanzi Bart Verbruggen na mlinda lango wa Manchester City James Trafford, wote 23, wakilenga kutafuta mrithi wa muda mrefu wa mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Nick Pope, 33. (The i Newspaper - Subscription Required),
Newcastle United pia inamwangalia winga wa Union Saint-Gilloise Anan Khalaili. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Israel mwenye umri wa miaka 21 amefunga mara tatu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu. (Mail+ - Subscription Required)
Winga wa Liverpool Trent Kone-Doherty, 19, kutoka Ireland Kaskazini, huenda akaondoka hivi karibuni na kujiunga na klabu ya Molde ya Norway licha ya kupewa kandarasi mpya huko Anfield. (Football Insider)
Napoli iliweka kipengele katika mkataba wa uhamisho wa mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen kwenda Galatasaray ambayo ina maana kwamba klabu hiyo ya Uturuki italazimika kuwalipa hadi £60m ikiwa watamuuza mchezaji huyo wa miaka 27 kwa klabu ya Italia. (Gazzetta dello Sport - In Italy)