Afya:Ufahamu ugonjwa ambao husababisha macho kutoka nje

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika shingo letu kuna tezi yenye umbo la kipepeo (thyroid) yenye aina mbili za homoni - T3 na T4 . Tezi hii huamua jinsi viungo vyetu tofauti vya mwili vinavyofanya kazi haraka.
Lakini wakati kuna hitilafu katika tezi hii - au ya TSH, homoni iliyotengenezwa na ubongo ambayo hutuma amri kwa tezi kufanya kazi - mwili unaweza kupata majeraha.
Unapopatwa na marathi haya , dalili unazoweza kupata ni kupungua kwa uzani wa mwili, kuvimbiwa, matatizo ya kumbukumbu, uchovu mwingi, hedhi isiyo ya kawaida, kupungua kwa kasi ya mapigo ya moyo na kupotea kwa nywele.
Hata hivyo, wakati T3 na T4 zinazalishwa kupita kiasi, mtu huweza kupata baadhi ya usumbufu kama vile mapigo ya kasi ya moyo, wasiwasi, kutokwa na jasho na hata kutetemeka kwa mwili.
Lakini kuna kuna athari ya nadra ambayo haijajulikana sana kuhusiana na hali hii inayohusishwa kitendo cha tezi kuzalisha homoni kupita kiasi hali inayojulikana na kama hyperthyroidism, hali ambayo inaweza kuwa na matokeo mabaya juu ya afya na ubora wa maisha. Miongoni mwa athari hizi ni ugonjwa wa tezi ya macho ambao pia unajulikana kama orbitopathy ya Graves au ophthalmopathy.
Katika hali hii, uvimbe ambao unajitokeza nyumba tundu la jicho husukuma macho mbele, na kusababisha usumbufu unaoweza kusababisha kupoteza uwezo wa kuona.
Habari njema ni kwamba kuna njia za kutibu hali hiyo - na wataalam kutoka Ulaya na Marekani hivi karibuni waliungana pamoja kufafanua njia bora za kupambana na ugonjwa huu. Katika miezi ya hivi karibuni, dawa mpya maalum dhidi ya ugonjwa wa orbitopathy ya Graves pia imeidhinishwa nchini Brazil.
Ni nadra au haijulikani kidogo?
Daktari wa wa macho Stefânia Diniz, mtaalamu wa oculoplasty – au kitengo kinachohusika na matibabu ya , kope, ducts za machozi na uso - anakadiria kuwa karibu 30% ya wagonjwa walio na kiwango kikubwa cha uzalishwaji wa homoni kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa jicho la tezi.
Uchunguzi wa kimataifa unaonyesha kuwa ugonjwa huu huathiri kati ya 0.5% na 2% ya idadi ya watu duniani.
Kwa hiyo, hesabu ya msingi inabainisha kuwa uzalishaji wa T3 na T4 huathiri Wabrazil kati ya milioni 1 na milioni 4 – na miongoni mwao , 300,000 hadi milioni 1.2 pia wanakabiliwa na ugonjwa wa tezi ya macho.
Ikumbukwe kwamba takwimu hizi ni makadirio tu, kwani hakuna tafiti maalum zilizochapishwa juu ya suala hili nchini.
"Ni ugonjwa, ambao unaweza kujidhihirisha kupitia dalili kali na zisizo maalum, kama vile ukavu au wekundu wa jicho, hadi usumbufu mkubwa ambao unaathiri uwezo wa kuona," anaelezea Diniz.
"Kwa bahati mbaya, ugonjwa wa macho ya tezi huchelewa kugundulika kwasababu ya ukosefu wa maarifa juu yake miongoni mwa watu wengi na miongoni mwa madaktari," analalamika mtaalamu.
Lakini baada ya yote, tatizo linaloathiri tezi linaweza kuwa na athari katika eneo maalum kama nyuma ya jicho?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ni muhimu kuelezea kwamba ugonjwa wa jicho la tezi ni ugonjwa wa autoimmune. Kwa maneno mengine, hii inamaanisha kuwa vitu vinavyozalishwa na mfumo wa ulinzi yenyewe huanza kushambulia sehemu maalum za mwili.
Katika hali hii , antibodies (protini zinazoukinga mwili kushambuliw) fulani huharibu kazi ya macho.
"Seli zilizoathirika huanza kuzalisha vitu vinavyoitwa glycosamines, ambavyo huvutia maji. Hii kwa upande wake huunda uvimbe ambao husababisha jicho kuwa kubwa na kutoka mbele ," anaelezea
"Baada ya muda, seli hizi zinaweza kutofautisha na kuzalisha tishu zaidi za adipose [mafuta] au misuli katika eneo hilo," daktari anaongeza.
Kwa maneno mengine, eneo la obiti ya macho- ambalo tayari ni la kawaida - linakusanya vitu vingi ambavyo havipaswi kuwa hapo.
Idadi kubwa ya visa vya ugonjwa huu wa macho zinahusishwa na utengenezwaji wa ziada wa homoni.
Lakini baadhi ya wagonjwa hupata ugonjwa huo , hata kutokana na tezi yenye afya.
Katika hali mbaya zaidi, macho huvimba au hata kupoteza uratibu wa harakati (kile kinachoitwa strabismus katika duru za matibabu). Baadhi ya wagonjwa wanakabiliwa tatizo la kuona vitu mara mbili mbili au hata hushindwa kabisa kufunga tena kope zao.
Villagelin inakadiria kuwa 80% ya wagonjwa wana aina kali zaidi za ugonjwa wa macho ya tezi, huwa na dalilizi za kuwasha au wekundu wa macho – huhisi kana kwamba wana mchanga juu ya uso wao .
Lakini tunawezaje kuzuia tatizo kama hili kufikia hatua kali zaidi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Utambuzi wa mapema
Diniz anasema kuwa ugonjwa wa jicho la tezi umegawanywa katika awamu mbili tofauti: unaoweza kutibika na sugu.
Wakati wa matibabu ya ugonjwa unaoweza kutibika, ambayo kwa ujumla huchukua kati ya miezi 6 na 18, mchakato wa uchochezi unaendelea na usumbufu unaendelea kidogo kidogo. Lakini katika hali ya ugonjwa kuwa sugu, tishu zilizokusanywa huanza kuunda makovu.
"Ugonjwa sugu, au wenye makovu, awamu ni mgumu zaidi kuutibu, kwa hivyo kadri ugonjwa unavyogundulika mapema hugunduliwa, bora," anasema.
Daktari wa ophthalmologist pia anasisitiza kuwa utambuzi unaweza kufanywa ofisini, kupitia uchunguzi wa dalili na ripoti ya mgonjwa - wakati mwingine, wataalamu huagiza mgonjwa- afanyiwe uchunguzi wa maabara au vipimo vya picha ili kuondoa sababu zingine za matatizo katika eneo hilo, kama vile uvimbe.
Mara tu ugonjwa wa tezi la jicho unapogunduliwa, matibabu yanaweza kuanza - ambayo yatatofautiana kulingana na ukali wake.
Sgarbi na Villagelin wanasema kuwa hatua ya kwanza ni kuimarisha utengenezwaji wa homoni katika tezi na dawa ambazo husaidia kudhibiti uzalishaji wa homoni ya tezi.
"Mwongozo wa pili ni kumuomba mgonjwa aache kuvuta sigara, kama inawezekana," anaongeza Villagelin.
Utafiti uliochapishwa katika miongo kadhaa iliyopita umegundua kuwa utabiri wa ugonjwa wa tezi la jicho ni mbaya zaidi kwa wavutaji sigara.
Sababu bado hazijajulikana kwa uhakika, lakini madaktari wanashuku kuwa sigara huongeza hali ya uchochezi wa mwili, ambayo ina athari kwenye tundu la jicho.
Pia kuna matibabu maalum ya kutibu ugonjwa wa orbitopathy yenyewe. Baadhi ya matone ya jicho na vilainishi vya macho husaidia kulainisha macho na kupunguza usumbufu wa haraka, kama vile kuwasha kunakosababishwa na ugumu wa kufunga kope.
"Kulingana na ukali, tunaweza kutumia dawa za kupambana na homoni za ziada, kupitia tiba ya mionzi, au kufanyiwa upasuaji," anasema Diniz.
Lengo ni hasa kuacha uvimbaji wa jicho na kuongezeka kwa kaboni ambayo hujilimbikiza katika sehemu ya ndani ya jicho. Katika hali kama hii upasuaji wa tishu zilizokusanywa hufanyika ili kuziondoa ili kupunguza shinikizo na kurekebisha kasoro za jicho.
Dawa zinazotumiwa zaidi katika muktadha huu ni za aina ya corticosteroids.

Chanzo cha picha, Getty Images
Sgarbi anaelezea wasiwasi juu ya uvumbuzi wa dawa. " hufika kwenye soko kwa bei ya juu sana," anasisitiza.
Nchini Marekani, matibabu ya ugonjwa huu yanagharimu mamia ya maelfu ya dola - na, ingawa thamani ya dawa hiyo nchini Brazil bado haijawekwa wazi.
Diniz anasisitiza kuwa upatikanaji wa rasilimali zaidi za matibabu hufanya iwezekane kubinafsisha matibabu na kutumia zana bora kulingana na maelezo ya kila mtu anayesumbuliwa na ugonjwa huo.
"Tunaweza kuzungumza na mgonjwa, kuwasilisha chaguzi za matibabu ya ugonjwa huo na kuamua pamoja juu ya chaguo bora," anaamini.
"Mara nyingi, watu wenye ugonjwa wa tezi ya macho huja kwetu na tatizo la unyanyapaa sana, ambalo huathiri ubora wa maisha yao."
"Kwa hiyo tunahitaji kuongeza uelewa miongoni mwa watu kuhusu ugonjwa huu na njia sahihi ya kutambua na kuutibu," anahitimisha daktari.















