Anga za mbali, uwanja wa mapigano usioonekana katika vita nchini Ukraine

Chanzo cha picha, Science Photo Library
Vita nchini Ukraine vimeonyesha ongezeko la umuhimu wa anga za mbali kwa wanajeshi walioko ardhini.
Katika mahojiano na BBC, Mkuu wa kikosi cha anga za mbali cha Marekani, Jenerali Jay Raymond, anaelezea kuwa "vita vya kwanza ambapo uwezo wa kibiashara wa anga za mbali umechangia jukumu kubwa ". Pia ni mzozo mkubwa wa kwanza ambapo pande zote zinazohusika na mzozo zimetegemea sana anga za mbali.
Jenerali Raymond - ambaye huduma yake ni tawi jipya zaidi la jeshi la Marekani - anaepuka kutoa maelezo halisi ya kina kuhusu jinsi Marekani na washirika wake wamekuwa wakiisaidia Ukraine.
Lakini anatoa dalili ya wazi ya kile ambacho kimekuwa kikifanyika. "Tunatumia anga za mbali kusaidia kushambulia kwa kulenga kwa usahihi, tunatumia anga za mbali kutoa tahadhari za makombora, ya tisho lolote ambalo linaweza kuja kwa Marekani au kwa washirika wetu ," anasema.

Tayari kuna zaidi ya setilaiti 5,000 katika anga za mbali - nyingi kati yake zinafanya kazi za malengo ya kibiashara.
Lakini miongoni mwake kuna mamia ya setilaiti za kijeshi - Marekani, Urusi na China zikiwa na idadi kubwa zaidi ya setilaiti hizo.
Ukraine haina hata moja. Lakini imepokea usaidizi mkubwa kutoka kwa mataifa ya Magharibi kwa njia mbali mbali.
UPELELEZI

Ya kwaza ni kutoa ujasusi, uchunguzi wa karibu na utambuzi wa kile kinachoendelea - au ISR.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ukraine ina uwezo wa kupata kiwango ambacho haijawahi kupata cha picha za setilaiti za kibiashara.
Katika mkutano wa hivi karibuni, mkurugenzi wa Shirika la taifa la ujasusi wa anga za mbali la Marekani - A Geospatial-Intelligence Agency, alisema imeongeza mara dufu picha za setilaiti kuhusu Ukraine kutokana na vita.
Makamu mwenyekiti wa safari za kijeshi za anga za mbali Paul Godfrey, ambaye anaongoza kituo cha kijeshi cha anga za mbali, anasema kwamba pamoja na picha zakibiashara na kiraia ambazo ISR ilitoa kwa Ukraine "kuna nchi nyingi ajabu zenye uwezo wa kijeshi katika anga za mbali -wanaiangalia Ukraine pia".
Space ISR kilisaidia kutambua kuongezeka kwa idadi yawanajeshi wa Urusi mwanzo kabla ya uvamizi wa Urusi tarehe 24 Februari na kusafiri kwa vikosi na zana za kijeshi.
Setilaiti zimekuwa zikitumiwa kufuatilia meli za kivita za Urusi katika Bahari Nyeusi, ikiwa ni pamoja na manoari ya kivita ya Moskva ambayo ilizamishwa na Ukraine.
Rada ya mapema ya tahadhari - kubwa kama ile iliyopo katika RAF Fylingdales katika North Yorkshire - zimekuwa na uwezo wa kuyatambua mashambulio ya makombora ya ballistic.
Naibu mkuu wa kikosi cha anga Godfrey anasema setilaiti za ISR pia zimekuwa muhimu kwa "kueleza ukweli" kuhusu vita.
Anatoa mfano wa mauaji ya kikatili katka Bucha , karibu na mji mkuu Kyiv. Anasema madai ya Urusi kwamba miili ya raia waliokufa tayari ilikuwa kwenye mitaa wakati walipowasili yalikuwa ni kinyume na muda uliojitokeza kwenye picha za setilaiti ambao ulionyesha kinyume.
Mashirika ya habari, ikiwa ni pamoja na BBC, pia yameweza kupata picha za setilaiti za kibiashara ambazo hazikuwahi kupatikana awali, ambazo yamekuwa yakizitumia kutatmini madai yaliyotolewa.
Hii ni pamoja na kutambua makaburi ya watu wengi au shambulio la hivi karibuni la Ukraine kwenye ngome ya kijeshi ya Urusi iliyopo katika jimbo la Crimea, eneo la kusini mwa Ukraine lililonyakuliwa na Urusi mwaka 2014.
Tahadhari za mapema kutoka kwenye mtambo wa rada pia zimeweza kubaini mashambulio ya makombora ya balistiki ballistic kabla hayajatokea.
Marekani pia kwa sasa iko katika mazungumzo ya kina kuhusu kuweka rada zaidi kubwa nchini Uingereza ili kufuatilia kile kinachoendelea katika anga za mbali.
Na waukraine wanaojitolea kusaidia nchi yao katika vita hivi karibuni wamechanga pesa za kutosha kununua setilaiti nzima ili kulisaidia jeshi la nchi hiyo kutambua maeneo yanayolengwa na Urusi.
Sar (Synthetic Aperture Radar) setilaiti ya kampuni ya Finland -ICEYE imeonyesha kuwa muhimu - katika siku mbili tu za matumizi yake ambao imewezesha uharibifu wa mali upande wa Urusi wenye thamani ya dola milioni16 – zaidi ya gharama ya ununuzi wa setilaiti , maafisa wa Ukraine wanasema.
MAWASILIANO
Anga za mbali zimekuwa muhimu pia katika mawasiliano katika kipindi chote cha vita.
Mwanzoni mwa vita Urusi ilifanya msururu wa nashambuli ya kijeshi ya anga na mashambulio ya kimtandao ili kuharibu mitambo muhimu ya mawasiliano ya Ukraine.
Naibu mkuu wa jeshi la anga Godfrey anamsifu Elon Musk kwa "kupata kuwezesha upatikanaji wa intaneti katika vita nchini Ukraine " – ambayo yalipatikana kutokana na ombi la upatikana ji wa huduma ya mawasiliano ya mtandao ya Twitter lililotolewa na Waziri wa manbadiliko ya kidigitali, Mykhailo Fedorov.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Elon Musk ametuma maelfu ya viunganishi vya intaneti nchini Ukraine ambayo yanatoa fursa ya kukuwasiliana na uzio wa setilaiti ya chombo cha anga za mbali cha SpaceX.
Yamekuwa muhimu katika kulipatia jeshi la Ukraine mawasiliano salama na uelewa wa hali katika kipindi chote cha vita .
Nimeshuhudia yakitumiwa kuanzia kwenye ngome za Ukraine zilizopo katika maeneo ya mwambao katika jimbo la mashariki mwa nchi la Donbas.
SILAHA ZINAZOLENGA MAENEO KWA USAHIHI

Chanzo cha picha, Reuters
HALI YA BAADAYE YA VITA KATIKA ANGA ZA MBALI
Kuongezeka kwa utegemezi wa anga za mbali kunaibua hofu kwamba mzozo unaweza kusambaa mbali ya ardhi, bahari na anga .
Urusi na China kwa pamoja zimefanya majaribio ya kuangamiza setilaiti zao wenyewe, na Mkuu wa majeshi wa uingereza Admiral Tony Radakin, hivi karibuni aliionya kwamba Urusi inaweza kufanya mashambulio katika maeneo ya nchi za Magharibi katika anga za mbali.
Jenerali Raymond anasema "kuna wigo kamili wa vitisho vya mashambulizi ambao tunauhofia ". orodha ya GPS na kuvurugika kwa mawasiliano, silaha za nguvu za moja kwa moja kama mionzi, au makombora kurushwa kutoka ardhini ambayo vinaweza kutumiwa kulenga setilaiti.
Anasema Marekani na washirika wake wakataka kuhakikisha kuna usalama kila mara na kuwa na tabia ya uwajibikaji katika anga za mbali – lakini akaongeza kuwa "kile ninachokihofia zaidi ni kwamba sio kila mtu ana mtizamo sawa unaofanana na wangu".
Kiuhalisia juhudi za kuzifanya anga za mbali kuwa eneo la kijeshi zinaendelea vizuri.












