Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 10.04.2024

TH

Chanzo cha picha, EPA

Tottenham inamfuatilia mshambuliaji wa Athletic Bilbao mwenye umri wa miaka 21 Nico Williams, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 42.8 katika mkataba wake. (Telegraph - usajili unahitajika)

Williams anaweza kusalia kwa msimu mwingine Athletic Bilbao kabla ya Barcelona kujaribu kumsajili msimu wa joto wa 2025(Sport -Kwa Kihispania)

Mazungumzo ya Newcastle United na kiungo wa kati wa Brazil Joelinton yanaendelea vyema na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anakaribia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Tyneside. (Telegraph)

Beki Mfaransa Raphael Varane, 30, na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 32, wanatarajiwa kuongoza orodha ya wachezaji ambao Manchester United itawauza msimu wa joto.(Talksport)

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool wako tayari kumruhusu Mohamed Salah kuhamia Saudi Pro League msimu huu ikiwa fowadi huyo wa Misri mwenye umri wa miaka 31 ataweka wazi kuwa anataka kuondoka. (HITC)

Manchester City wanavutiwa na winga wa Wolves Pedro Neto lakini huenda wakakabiliana na ushindani kutoka kwa vilabu vya Saudi Arabia kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 24(Teamtalk)

Crystal Palace na Fulham wanalenga kumnunua mlinzi wa Union Berlin Mholanzi Danilho Doekhi, 25. (Football Insider)

Mshambulizi wa Real Madrid Rodrygo, 23, anasema alikataa kuhamia Liverpool mwaka wa 2017, ingawa Reds walikuwa na ofa ya euro milioni 3 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil iliyokubaliwa na Santos. (90 Min)

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal itashindana na Manchester United kumsajili kiungo wa kati wa Wolves na Brazil Joao Gomes, 23, msimu huu wa joto. ( O Dia - kwa Kireno)

Mlinzi wa pembeni wa kulia wa Bayer Leverkusen wa kimataifa wa Uholanzi Jeremie Frimpong, 23, anavutiwa na Liverpool katika hatua ambayo inaweza kumfanya Trent Alexander-Arnold kuhamia katikati ya uwanja. (Football Insider)

Manchester United bado hawajakubali mkataba wa fidia na Newcastle kwa ajili ya Dan Ashworth na huenda ikalazimika kusubiri miezi kadhaa kabla ya kumteua kama mkurugenzi wao wa michezo.(Guardian)

Paris St-Germain na Barcelona wanavutiwa na mshambuliaji wa Liverpool Luis Diaz, ambaye wakala wake alimtembelea mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia, 27 hivi majuzi. (Telegraph - usajili unahitajika)

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah