Rafiki aliyemuongoza Shamima Begum kujiunga na IS alimdhihaki kama asiyeamini

g
Maelezo ya picha, Sharmeena Begum, alitoroka kutoka Uingereza na kwenda Syria miezi miwili kabla ya Shamima Begum

Sharmeena Begum, alitoroka kutoka Uingereza na kwenda Syria miezi miwili kabla ya Shamima Begum.

Rafiki mkubwa wa Shamima Begum, ambaye anasema alimshawishi kujiunga na IS, amefuatiliwa na BBC baada ya kutoroka kutoka kwenye kambi ya mahabusu nchini Syria.

Sharmeena Begum, hakuna uhusiano, alimpuuza rafiki yake wa zamani ambaye anataka kurudi Uingereza kwa "kuishi maisha yasiyo na faida"na kudhihakiwa naye kama mtu asiye amini.

BBC pia ilibaini kuwa Sharmeena alikuwa anachangisha pesa mtandaoni kwa ajili ya wajumbe wa kundi la ugaidi la IS, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Kamanda wa ngazi ya juu wa Syria anahofia kuwa pesa kama hizo zinaweza kulisaidia kundi la IS kujikusanya tena.

Akijionyesha kama mtu anayewahurumia Islamic State(IS), mwandishi wa habari katika hadithi ya podcast ya Shamima aliwasiliana na Sharmeena kweye intaneti baada ya kutoroka kutka kambi ya Syria ya inayofahamika kama gereza la Camp Hol kwa ajili ya wanawake waliokuwa na IS, pamoja na watoto wao.

Sharmeena bado yuko nchini Syria, mafichoni na anatumia utambulisho tofauti.

Alikuwa anasoma katika shule moja na Shamima Begum, katika Bethnal Green, mashariki mwa London, wakati katika mwezi wa Decemba 2014, Sharmeena ghafla alipotea. Alitoroka na kwenda kujiunga na kikundi cha magaidi cha Islamic State nchini Syria.

Kupatikana katika mtandao wa kijamii

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Miezi miwili baadaye Shamima na marafiki wengine wawili walimfuata mwanafunzi mwenzao katika kile kinachoitwa caliphate ambacho kilianzishwa na IS.

Shamima alienda kuolewa na mpiganaji wa IS na akazaa naye watoto watatu ambao wote walifariki. Baada ya kuanguka kwa IS katika mwaka 2019 alipatikana akiwa anaishi katika kambi nchini Syria, akiwa amevuliwa uraia wa Uingereza.

Shamima anasisitiza kuwa ni Sharmeena ambaye alimshawishi ajiunge na IS na akafuata nyayo zake.

BBC ilimfuatilia baada ya kupewa taarifa ya siri kuhusu akaunti ya mtandao wa kijami anaoutimia.

Wakati wa mazungumzo na yeye, Sharmeena alidai kuwa aliyewahikuwa rafiki yake wakati mmoja alikuwa " tu mtu ambaye alikuwa anaishi kwa kuzingatia" ambaye hakuchangia lolote kabisa.

Anasema Shamima alikuja Syria tu kwasababu "alifuata tu rafiki zake katika kile kilichogeuka na kuwa majonzi makubwa ya maisha yake ".

Licha ya tetesi kwamba Shamima Begum alikuwa akifanya kazi katika Hisba – polisi ya kidini ya IS – na kutengeneza fulana za kulipua mabomu ya kujitoa mhanga, Sharmeena anasema nadharia za aina hiyo ni "matusi".

Anasema Shamima hakuwahi kuondoka nyumbani kwa mume wake isipokuwa wakati mume wake alipokuwa mbali kwasababu asingemruhusu kwenda nje ya nyumba.

g
Maelezo ya picha, Shamima Begum, aliwa na umri wa miaka 15 wakati alipojiunga na Islamic State, akimfuata rafiki yake Sharmeena

Katika mazungumzo na BBC, alimdhihaki Shamima kama mtu aliyeshindwa na mkosa Imani, akisema aliharibu sifa ya wanawake ambao walijiunga na IS.

Mjumbe wa zamani wa IS ameiambia BBC kuwa Sharmeena ni shabiki tu hata kwa viwango vya IS. Alipoulizwa iwapo anajutia kujiunga na IS, Sharmeena alikwepa jibu, akisema tu kwamba hataki kurudi Uingereza na kwenda gerezani.

Ni vigumu kuelewa kiasi gani maelezo ya Sharmeena kumhusu rafiki yake ni ya kweli kuhusiana na shughuli zake, ikizingatiwa kuwa Shamima amejaribu kurejea Uingereza kisheria.

Kwa upande wake, Shamima anasema rafiki yake wa zamani alikuw ana mchango mkubwa katika kumshawishi kusafiri kwenda syria.

"Sharmeena alikuwa, unafahamu, akizungumza nasi ana kwa ana, unajua, kuhusu kuja katika ISIS. "nilirubuniwa kufikiri kwamba hiki kilikuwa ni kitu sahihi cha kufanya na nilidanganywa kwa uongo kuhusu kule ambako nitakwenda na kile nitakachokuwa nakifanya.

"Ninamaanisha, kwa maoni yangu, hata kama labda Sharmeena huenda bado ana itikadi kali. Ninaweza kusema pia alikuwa muathiriwa wa ISIS."

Shamima binafsi awali alikubali kuwa alijiunga na kundi la ugaidi wakati alipotoroka Uingereza na anaelewa hasira ya umma dhidi yake.

Wakati akiwa mafichoni , Sharmeema Begum amekuwa akichangisha pesa ambazo ziliangukia mikononi mwa IS. Amekuwa akituma taarifa za video kwa njia ya mitandao ya kijamii na majukwaa ya jumbe, kuhusu hali katika makambi ya mahabusu , ana kutoa wito wa watu kutuma Bitcoin.

g

Chanzo cha picha, JOSH BAKER

Maelezo ya picha, Shamima Begum alivuliwa uraia wa Uingereza baada ya kujiunga na kundi la Islamic State

Mikanda ya vilipuzi

Haijabainika wazi ni kiasi gani cha pesa alizochangisha, lakini akaunti moja ilifichua kusafirishwa mara 29 kwa pesa ambapo jumla ya $3,000 (£2,450) zilichangishwa. Pia anatumia akaunti nyingine na cryptocurrencies.

Tulipouliza ni kwanini anachangisha pesa kwa ajili ya kundi la ugaidi, Sharmeena alidai alikuwa "tu anawalisha na kuwavalisha wanawake na watoto ambao ni masikini".

Kamanda wa vikosi vya Syria- Syrian Democratic Forces , ambavyo vinalinda kambi ya Hol, alisema kuwa IS inajikusanya tena katika makundi na inaiba pes ana kuziingiza ndani ya makambi, ambazo zinaweza kutumiwa kununulia silaha, na kujaribu kutoroka na mashambulio.

"Tukitazama…katika makambi, kuna watoto wachache wadogo ambao wana umri wa miaka michache, na wanakuzwa na fikra za jinsi ya kuua," alisema Jenerali Newroz Ahmed. Anasema watu wake ni miongoni mwa wale wanaolengwa na kuuawa.

Kambi hiyo inawahifadhi watu zaidi ya 65,000 na wanatoka katika mataifa 57 , na walinzi pale wanasema wamekuwa wakipata grunedi na mikanda ya vilipuzi ambavyo vimekuwa vikiingizwa ndani ya kambi. Wanasema watu 50 wamekwishauawa pale katika kipindi cha miezi sita.

Mwezi Januari, Marekani na Uturuki zilitangaza hatua ya pamoja ya kuvuruga usafirishaji wa pesa kwa kikundi cha Islamic State.