Tetesi za soka Ulaya Jumamosi:PSG wanatarajia ofa kwa ajili ya Donnarumma

Donnarumma

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Paris St-Germain wanatarajia ofa kutoka kwa Chelsea, Manchester United au Inter Milan kwa ajili ya mlinda lango wa Italia Gianluigi Donnarumma, 26. (ESPN)

Newcastle wanajipanga kuwasilisha ofa ya pauni milioni 30 kumnunua mshambuliaji wa Brentford mwenye umri wa miaka 28 kutoka DR Congo Yoane Wissa. (Times)

Newcastle wameanza mazungumzo na PSG kuhusu mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 26. (Florian Plettenberg)

Randal Kolo Muani

Chanzo cha picha, Getty Images

The Magpies pia wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Porto na Uhispania Samu Aghehowa, 21, ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji. (Athletic)

Mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, angependelea kusalia katika Ligi ya Premia ikiwa ataondoka Chelsea msimu huu wa joto na uwezekano wa kwenda Newcastle. (Sun)

Jackson angependa kuondoka Chelsea mwezi huu, huku AC Milan na Juventus pia zikiwa na nia ya kumsajili. (Mail)

Nicolas Jackson

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United inataka kumsajili kiungo mkabaji na mlinda lango mpya sasa wamekamilisha kumsaka mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, 22, kutoka RB Leipzig. (Telegraph)

Southampton wanahitaji angalau pauni milioni 50 kwa winga wao wa chini ya miaka 21 wa England Tyler Dibling, 19, huku Everton wakitarajia kufanya mchakato wa kumpata. (Liverpool Echo)

Klabu ya Ufaransa ya Lille inalenga kumnunua kwa mkopo mlinda langi wa Spurs raia wa Czech Antonin Kinsky. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 yuko kwenye rada iwapo mlinda mlango chaguo la kwanza, Mfaransa Lucas Chevalier, 23, atajiunga na PSG. (L'Equipe )

Antonin Kinsky

Chanzo cha picha, Getty Images

Brentford wana nia ya kumsajili winga wa Bournemouth Dango Ouattara. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Burkina Faso mwenye umri wa miaka 23 alicheza mechi 32 za Premier League akiwa na Cherries msimu uliopita. (Sky Sports)

Leeds United iliyopanda daraja hivi karibuni inavutiwa na kiungo wa kati wa Brighton mwenye umri wa miaka 20 Facundo Buonanotte. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina pia anasakwa na Borussia Dortmund.(Yorkshire Evening Post)