Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vituo vya nyuklia vya Iran viko wapi na ni vipi vilivyoshambuliwa?
Siku ya Ijumaa, Juni 13, 2021, Israel ilifanya mashambulizi kote nchini Iran, ikiwa ni pamoja na kulenga vituo vya nyuklia vya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Iran, vituo vya Natanz na Arak vilikuwa miongoni mwa walengwa wa mashambulizi haya.
Makala haya yanaangazia vituo muhimu zaidi vya nyuklia vinavyojulikana nchini Iran
Kituo cha nyuklia cha Natanz
Kituo cha nyuklia cha Natanz, ambacho ndio kituo kikubwa zaidi cha kurutubisha madini ya uranium nchini Iran, kinapatikana takriban kilomita 250 kusini mwa Tehran.
Kituo hiki kina sehemu mbili: Kituo cha Majaribio cha Urutubishaji wa Mafuta (PFEP) na Kituo Kikuu cha Kurutubisha Mafuta (FEP), ambacho kimejengwa chini ya ardhi kustahimili mashambulizi ya angani.
Kumekuwa na mijadala kwa miaka mingi kuhusu uharibifu unaowezekana wa mashambulizi ya anga ya Israel kwenye kituo hicho.
Kituo kikuu cha Natanz kilijengwa kwa uboreshaji wa kiwango cha kibiashara na kina uwezo wa kushikilia takriban 50,000 centrifuges.
Hivi sasa, takriban centrifuge 14,000 zimewekwa huko, ambazo karibu 11,000 zinafanya kazi, na kurutubisha uranium hadi asilimia 5 ya usafi.
Chini ya mapatano ya nyuklia ya mwaka 2015 (JCPOA), Iran ilikubali kupunguza urutubishaji wake wa uranium hadi asilimia 67.3, lakini baada ya Marekani kujitoa katika mapatano hayo chini ya Rais Donald Trump mwaka 2018, Iran ilianza kurutubisha viwango vya juu zaidi, na hatimaye kufikia asilimia 60.
Kizingiti cha kurutubisha uranium kwa silaha za nyuklia ni asilimia 90
Kabla ya shambulio la Ijumaa la Israel, Natanz ilikuwa ikilengwa na mashambulizi na hujuma mbalimbali za mtandaoni, vikiwemo virusi vya Stuxnet, vilivyogunduliwa mwaka 2010 na vinavyojulikana kuwa operesheni ya pamoja ya Marekani na Israel, pamoja na mlipuko uliotokea mwaka 2021, ambao Iran iliilaumu Israel.
Kituo hiki, pia kinajulikana nchini Iran kama Kiwanja cha Uboreshaji cha Shahid Ahmadi Roshan, kiko katikati ya mazungumzo ya kimataifa na hutembelewa na kukaguliwa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki.
Mostafa Ahmadi Roshan alikuwa naibu mkurugenzi wa kibiashara wa tovuti ya nyuklia ya Natanz ambaye aliuawa mjini Tehran Januari 2011.
Kama "wanasayansi wengine wa nyuklia," mauaji yake yamehusishwa kwa kiasi kikubwa na Israeli.
Kituo cha urutubishaji cha Fordow
Kituo cha Urutubishaji cha Mafuta cha Fordow ni kituo cha urutubishaji cha urani kinacholindwa sana, chini ya ardhi karibu na eneo la Qom, takriban kilomita 160 kusini mwa Tehran.
Ujenzi wake wa siri, ndani kabisa ya mlima, ulifichuliwa mwaka wa 2009, na kuibua wasiwasi wa kimataifa kuhusu malengo ya Iran ya nyuklia.
Fordow imeundwa kuhifadhi karibu centrifuges 3,000 na kwa kiasi kikubwa kinastahimili mashambulizi ya angani.
Kwa kusaini JCPOA, Iran ilikubali kugeuza Fordow kuwa kituo cha utafiti na kusimamisha shughuli za kurutubisha uranium kwa miaka 15.
Hata hivyo, baada ya Marekani kujitoa katika makubaliano hayo, Iran ilianza tena shughuli za kurutubisha madini ya uranium katika kituo hicho, na kuongeza hadi asilimia 20 kufikia mwaka 2021.
Mnamo Novemba 2022, Iran iliongeza kiwango cha urutubishaji wa uranium katika kituo cha Fordow hadi 60% na kutangaza nia yake ya kuongeza kwa kiasi kubwa uwezo wake wa kurutubisha.
Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki hufuatilia kituo hicho, lakini ongezeko la shughuli za uboreshaji wa Fordow na uwezo wake na teknolojia yake ya hali ya juu inaendelea kutoa changamoto kwa juhudi za kimataifa za kuzuia uundaji wa silaha za nyuklia
Kituo cha Fordow pia kinajulikana kama "Martyr Alimohammadi Enrichment Complex."
Masoud Alimohammadi, profesa wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Tehran na, kulingana na maafisa na vyombo vya habari vya Iran, mmoja wa "wanasayansi wa nyuklia" ambaye aliuawa Januari 2009 kaskazini mwa Tehran.
Kituo cha maji mazito cha Khandab {Arak}
Kituo cha nyuklia cha Khandab, ambacho zamani kilijulikana kama Arak , ni kituo kilicho karibu na mji wa Khandab katika Mkoa wa Markazi.
Kikiwa kimeundwa kama kinu cha utafiti, kituo hicho kimekuwa chanzo cha wasiwasi juu ya mpango wa nyuklia wa Iran kwa sababu ya uwezo wake wa kuzalisha plutonium, ambayo inaweza kutumika kutengeneza silaha za nyuklia.
Chini ya makubaliano ya JCPOA, Iran ilisitisha ujenzi wa kinu, ikaondoa msingi wake, na kuujaza saruji ili kisiweze kutumika.
Kinu hicho kilipaswa kuundwa upya ili kupunguza uzalishaji wa plutonium na kukifanya kisiweze kutumika kwa utengenezaji wa silaha.
Iran imefahamisha Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki kwamba inapanga kufanya mtambo huo kufanya kazi ifikapo 2026.
Mustakabali wa kituo hicho bado ni suala nyeti katika shughuli za nyuklia za Iran.
Kituo cha Nyuklia cha Isfahan
Kituo cha Isfahan ni sehemu moja ya mpango wa nyuklia wa Iran ambao unalenga kubadilisha uranium kuwa mafuta na kifaa cha urutubishaji.
Kituo cha Usindikaji cha Isfahan kinazalisha uranium hexafluoride (UF6), ambayo ni muhimu kwa uboreshaji katika Natanz na Fordow.
Eneo hilo pia linazalisha mafuta kwa vinu vya nyuklia, ikiwa ni pamoja na kituo cha nguvu cha Bushehr.
Mnamo Februari 2023, Iran ilitangaza kuwa imeanza ujenzi wa "kinu cha nne cha utafiti" katika kituo hiki.
Wakati ukaguzi wa IAEA unaendelea huko Isfahan, kuna wasiwasi kuhusu shughuli zinazohusiana na uzalishaji wa madini ya urani, ambayo yanaweza kuwa na matumizi ya kijeshi.
Wigo wa shughuli za nyuklia huko Isfahan unaonyesha lengo la Iran la kufikia nishati ya nyuklia.
Kiwanda cha nguvu za nyuklia cha Bushehr
Kiwanda cha Nishati ya Nyuklia cha Bushehr ndicho kinu pekee cha nishati ya nyuklia cha Iran, kilichoko kwenye pwani ya Ghuba ya Uajemi kusini mwa mji wa Bushehr.
Ujenzi wa mtambo huo ulianza mwaka 1975 kwa usaidizi wa Ujerumani na kukamilishwa na Urusi baada ya kuchelewa kwa muda mrefu.
Kiwanda hicho kilianza kufanya kazi mnamo 2011 na kinatumia uranium inayotolewa na Urusi.
Mafuta yake yaliyotumika yanarudishwa nchini Urusi ili kuzuia yasichakatwe tena kuwa nyenzo ambazo zinaweza kutumika katika silaha za nyuklia.
Ingawa Bushehr ni kituo cha uzalishaji wa nishati ya kiraia na chini ya usimamizi kamili na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, kuna wasiwasi kuhusu viwango vya usalama na ukaribu wa mtambo huo na maeneo yanayokumbwa na tetemeko la ardhi.
Kituo cha utafiti cha Tehran
Kituo hiki cha utafiti cha Tehran ni kituo kidogo cha utafiti na utengenezaji wa isotopu za matibabu.
Kilijengwa mwaka wa 1967 kwa usaidizi wa Marekani, awali kinu hicho kilifanya kazi kwa kutumia urani iliyorutubishwa kuzalisha isotopu za matibabu.
Hathivyo, mwaka 1987, kilibadilika na kutumia uranium iliyorutubishwa kidogo ili kupunguza hatari ya kuenea kwa nyuklia.
Kinu hicho kilikabiliwa na uhaba wa mafuta hadi 2009, na kusababisha Iran kuanza kurutubisha uranium hadi 20% ili kuongeza mafuta.
Mnamo mwaka wa 2012, Iran ilizalisha na kupakia vijiti vyake vya kwanza vya mafuta vilivyotengenezwa nchini kupitia kituo hicho cha Utafiti cha Tehran.
Kituo cha Jeshi cha Parchin
Kituo cha Parchin, kilichopo kusini mashariki mwa Tehran, ni kituo cha siri cha kijeshi ambacho, kulingana na ripoti za hapo awali za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, kimekuwa kikishukiwa kuhusishwa na uwezekano wa mwelekeo wa kijeshi kwa mpango wa nyuklia wa Iran.
Iran inakanusha shughuli zozote za nyuklia na kusema Parchin ni ya matumizi ya kijeshi ya kawaida pekee, na ufikiaji wa ukaguzi umepunguzwa.
Ziara ya mkurugenzi wa wakati huo wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki mnamo 2015 haikuondoa wasiwasi juu ya kituo hicho na iliacha maswali wazi juu ya mwelekeo wa kijeshi wa mpango wa nyuklia wa Iran.
Mnamo Mei 2022, mlipuko katika Parchin, kituo kikuu cha kijeshi cha Iran na maendeleo ya silaha mashariki mwa Tehran, uliua mhandisi na kumjeruhi mwingine.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla