Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
DRC: Njia inayofaa kulipiza kisasi cha mauaji ya Cirimwami ni kuwamaliza maadui- FRDC
Msemaji wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, anamewatolea wito wanajeshi na wapiganaji wote wanaosaidiana katika vita na wapiganaji wa M23 kummaliza "adui popote alipo" kama mojawapo ya njia za kulipiza kisasi kwa mauaji ya Meja Jenerali Peter Cirimwami Nkuba aliuawa hivi karibuni.
Katika kauli yake aliyoitoa baada ya kikao cha Baraza la usalama la kitaifa na Rais Felix Tshisekedi Ijumaa kuhusu suala la ukosefu wa usalama nchini, Jenerali Sylvain Ekenge aliwapa ujumbe wa wazi wapiganaji la serikali ya DRC linalojulikana kwa jina la Wazelendo kuwa tayari kuliunga mkono jeshi katika mapambano dhidi ya M23. na dhamira iliyo wazi.
"Njia halisi ya kulipiza kisasi kwa mauaji ya Cirimwami ni kuwafukuza maadui hawa na kukomboa maeneo yote waliyoyamiliki hadi sasa. Hili ni jukumu la kizalendo," alisema.
Jenerali Ekenge alisema kuwa Cirimwami "alijeruhiwa, kisha akapelekwa Kinshasa kupata matibabu yanayostahili nje ya nchi, lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia kwa majeraha".
DRC na Umoja wa Mataifa zinaishutumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuchochea uasi wa miaka mitatu wa M23 kwa kutumia wanajeshi wake na silaha. Rwanda inakanusha hili.
Cirimwami anafahamika kuwa na mchango mkubwa katika kuanzisha ushirikiano kati ya jeshi la serikali na washirika wake katika vita dhidi makundi ya uasi kama vile M23, baada ya kuteuliwa mwaka 2023 kuwa gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini, ambalo libakabiliwa na makudi ya waasi hususan M23.
Jenerali Ekenge alisema, katika mkutano huo, "Amiri jeshi mkuu [Rais Tshisekedi] alitoa amri kali kwamba adui aliyetushambulia auawe popote alipo, ashindwe, afukuzwe Goma na kukaliwa hadi maeneo yote yaliyokaliwa yakombolewe ".
Kundi la M23 limekuwa likiendesha vita kwa zaidi ya miaka mitatu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako limedhibiti maeneo kadhaa ya jimbo la Kivu Kaskazini.
Kwa jinsi mambo yalivyo hadi sasa, kuna hofu kwamba huenda vita vya kikanda vikazuka baada ya kundi hili kuukaribia mji wa Sake, ulioko takriban kilomita 20 magharibi mwa barabara kuu ya jimbo la Kivu Kaskazini, kuelekea Goma, mji wa ambao M23 inataka kuuteka..
Hii ni baada ya kundi hilo kuuteka mji wa Minova katika jimbo la Kivu Kusini, takriban kilomita 40 kutoka Goma mwanzoni mwa wiki hii.
Wakati huo huo, DRC imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili mzozo huo wa Mashariki mwa nchi.
Waziri wa mambo ya nje wa Congo Thérèse Kayikwamba Wagner, aliyeko New York alisema matatizo ya nchi hiyo yanatokana zaidi na ukweli kwamba Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa "haliwajibiki licha ya kwamba inajulikana katika ngazi ya kimataifa na kuwa Rwanda iko katika eneo la Congo".
Katika mkutano wake waziri huyo, ambaye anaiwakilisha China katika Umoja wa Mataifa, Kayikwamba alisema: "Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo haiwezi kuendelea kuvumilia maneno tu, na kulitaka Baraza Kuu lichukue vikwazo vikali".
Katika taarifa iliyotolewa tarehe 25 Novemba ,Umoja wa Ulaya (EU/EU) unasema kwamba hauwezi kuvumilia "M23 kuendelea kuchukua hatua za kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano".
Wakati M23 ikionya kuwa inataka kuuteka mji wa Goma, Umoja wa Ulaya unasema kuwa hilo haliwezi kuvumiliwa, na unatoa wito wa kusitisha mashambulizi yake haraka iwezekanavyo na kurudi nyuma.
Muungano wa Ulaya umeitaka Rwanda kusitisha msaada wake kwa M23 na kuondoa wanajeshi wake, na pia unaiomba serikali ya Congo kuacha kufanya kazi na waasi wa FDLR wanaopigana dhidi ya serikali ya Kigali.
Taarifa hiyo ilisema: "EU inalaani vikali uwepo wa jeshi la Rwanda katika ardhi ya Congo kama ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, mikataba ya Umoja wa Mataifa, na uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
"EU inaitaka DRC kusitisha ushirikiano na FDLR na makundi mengine yenye silaha".
Umoja wa Ulaya pia unasema kuwa unaunga mkono kwa dhati ujumbe wa MONUSCO, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kudumisha amani na usalama nchini humo, ukikumbusha kwamba shambulio lolote dhidi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa halitavumiliwa hata kidogo.
MONUSCO inaunga mkono FARDC na SAMIDRC
Vikosi vya Monusco vinasema kuwa vinaendelea kuunga mkono jeshi la Kinshasa katika juhudi zao za kuzima uwepo wa M23 wanaoendelea kukalia eneo hilo.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana usiku, Monusco ilisema kuwa siku ya Alhamisi na Ijumaa ilishambulia kambi ya M23 katika mji wa Sake kwa silaha kali, na kwamba "inarejesha vikosi vyake kwenye maeneo yenye nguvu ili kuendeleza uharibifu." katikati na viunga vya Goma".
Inaendelea kusema: "Ujumbe huu pia unashirikiana na jeshi la Congo katika doria kufanya doria usiku na umesaidia katika uharibifu wa silaha nzito na helikopta za kivita za jeshi la Congo, katika kutwaa vifaa vya M23."
Monusco pia inasema kwamba vikosi vyake maalum (Forces de réaction rapide, QRF), "vimetekeleza jukumu muhimu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, na wameonyesha ujasiri na ujuzi" katika jiji la Sake, ambapo, kama taarifa inaendelea, "wanajeshi wa Umoja watano walijeruhiwa siku ya Ijumaa, huku wengine wanne wakijeruhiwa kidogo siku ya Alhamisi."
Monusco pia inasema inavisaidia vikosi vya nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Umoja wa Afrika (SAMIDRC) ambavyo vimetumwa kulisaidia jeshi la DRC katika masuala ya dawa na vifaa.
Monusco inasisitiza umuhimu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa M23 akiiomba "ikomesha mashambulizi yake na kujiondoa katika maeneo yanayokaliwa kwa mujibu wa makubaliano ya kusitisha mapigano ya Machi 31 (7) 2024".
Inatoa wito kwa pande zote mbili kurejea katika meza ya mazungumzo kutafuta suluhu la kudumu la mzozo huo ambao umesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao.
M23 ndiyo inayotishia jimbo la mashariki nchi hiyo, ambapo tangu mwisho wa mwaka 2021 ilipoanzisha vita hivi mpya, imeteka maeneo mengi katika jimbo la Ruguru Kivu, na sasa inashambulia jimbo la Kivu Kusini.
DRC inaendelea kusisitiza kuwa lilishambuliwa na Rwanda, ambayo imejificha nyuma ya M23, na kwamba kuna matamko ya Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi hii kwamba ilituma wanajeshi 4,000 nchini Kongo kupigana upande wa M23.
Rwanda pia inaishutumu Congo kwa kufanya kazi na kundi la FDLR linaloendesha harakati dhidi ya serikali ya Rwanda, lenye wajumbe wanaotuhumiwa kuua watu katika mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994, na inaonekana ndiyo maana serikali ya Paul Kagame haikatai kuwa ina askari katika madini haya- nchi tajiri zaidi
Akizungumzia suala hili katika hafla ya kuwatakia mwaka mpya mabalozi wa nchi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yanayofanya kazi nchini Rwanda wiki iliyopita, Rais Kagame hakukanusha wala kuthibitisha, lakini aliwaambia:
"Kabla ya kuniuliza swali hilo, unaweza kueleza ni kwanini FDLR iko Congo na kwa nini inaungwa mkono na serikali ya Congo?"
Ndio maana juhudi zote za kujadiliana hata kama hatuna uwezo wa kulifikia ni zile za kuunganisha nchi ya Congo na Rwanda.
Mazungumzo yaliyoitishwa na Angola kati ya Rwanda na Congo mwishoni mwa mwaka jana yalitarajiwa kufikia makubaliano ya amani yaliyoidhinishwa na viongozi wa nchi hizo, lakini mkutano wa Luanda ulifutwa dakika za mwisho.
Rwanda ilisema kuwa mapatano hayo yangekuwepo lakini serikali ya Congo iliapa kutowasiliana na M23.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi