Mfahamu Mwanamke wa Kihindi aliyeukonga moyo wa Nelson Mandela

Na, Rehan Faza

Mwandishi BBC, New Delhi

.

Nelson Mandela aliwahi kutania, 'Ikiwa wanawake wataniona na kunipenda, sio kosa langu. Kusema kweli, nisingepinga kamwe.'

Nelson Mandela, ambaye alikuwa ameoa mara tatu, aliendelea kuvutia wanawake kutoka duniani kote hata katika uzee wake.

Lakini kulikuwa na mwanamke mmoja ambaye alikataa kuolewa na Nelson Mandela. Jina la mwanamke huyo wa Kihindi lilikuwa Amina Chachalya.

Kwa nini Amina alikataa kuolewa na Nelson Mandela?

Alizaliwa mwaka wa 1930, Amina alichukuwa na nafasi muhimu katika harakati dhidi ya sera za ubaguzi wa rangi za serikali ya Afrika Kusini ya wakati huo.

Alipokuwa na umri wa miaka 21 tu, Amina aliwahi kumtembelea Nelson Mandela gerezani.

Amina aliolewa na Yusuf Chachalya ambaye alifariki mwaka 1995. Wakati huo, Nelson Mandela alikuwa ameanza mchakato wa kumtaliki mke wake wa pili.

"Tulijua kuwa Mandela na wazazi wangu walikuwa marafiki wazuri sana," anasema Ghalib Chachalya, mtoto wa Amina.

Mara nyingi alikuja nyumbani kwetu.'

"Mara moja katika miaka ya 90 mama yangu alituita mimi na dada yangu na akatuambia kuwa Nelson Mandela alikuwa anataka kumuoa ambapo angelikataa," anasema.

Wakati huo, Nelson Mandela alikuwa na umri wa miaka 80 na Amina alikuwa na miaka 68.

Nilimuuliza Ghalib kwa nini mama yake alikataa posa ya mtu mashuhuri namna hii.

Jibu la Ghalib lilikuwa kwamba 'Mama yangu alimpenda Nelson Mandela, lakini hakuwa tayari kumsahau baba yangu pia.

Baba yangu alikuwa na umri wa miaka 15 zaidi. Labda baada ya kifo chake hakutaka mtu mwingine yeyote aje maishani mwake.

Mwanamke mrembo na mcheshi

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mwanahabari mashuhuri Saeed Naqvi anasema kwamba alipata fursa ya kukutana na Amina kwa mara ya kwanza wakati Nelson Mandela alipoachiliwa kutoka gerezani.

Mume wa Amina Yusuf alikuwa hai wakati huo.

Alipoenda kukutana na Nelson Mandela baada ya kutoka gerezani, alimwona Amina akiwa amekaa karibu na Mandela.

Saeed Naqvi anasema, mara tu 'nikimtazama Amina, nilihisi kwamba lazima alikuwa mrembo sana, mwenye kuvutia, na mcheshi.

Utu wake ulikuwa na kila kitu ambacho shujaa anatafuta.

Alifanya kazi African National Congress. Alikuwa rafiki wa Nelson Mandela na kiwango chake cha akili pia kilikuwa sawa na cha Nelson Mandela.

Cha kufurahisha ni kwamba, Keith Miller, mshiriki wa timu ya kriketi ya Australia ambaye ilizuru Afrika Kusini mnamo 1948, pia alimpenda Amina.

Wakati huo hakuwa ameolewa na Keith Miller alikuwa mwanamichezo maarufu duniani.

Saeed Naqvi anasema kwamba wawili hao walikutana kwenye sherehe ambapo Keith Miller alianza kumpigia simu Amina mchana na usiku.

Jambo la kufurahisha ni kwamba angeweza kupiga simu tu lakini hakuweza kuja kukutana naye.

.

Chanzo cha picha, GHALEB CHACHALYA

Maelezo ya picha, Amina alikuwa na watoto wawili, binti Coco na mtoto wa kiume Ghalib

Tatizo moja lilikuwa kwamba Amina aliishi katika eneo la Wahindi.

Amina na Nelson Mandela walikuwa na mikutano kadhaa mbele ya Saeed Naqvi, lakini walipokwenda Afrika Kusini mwaka 1995, mume wa Amina Yusuf alikuwa tayari amefariki.

Ilitokea mara kadhaa ambapo Saeed Naqvi alipoenda kukutana na Amina, alikuta yuko na Nelson Mandela.

Saeed Naqvi anasema, 'Kisha nikajua kutoka kwake kwamba Nelson Mandela alikuwa amefanya kile ambacho Keith Miller hangeweza kufanya.

Na taratibu kila mtu akaja kujua kwamba Nelson Mandela alikuwa ameanza kufanya uamuzi wa kumuoa.'

.
Maelezo ya picha, Mwanahabari mwandamizi Saeed Naqvi akiwa na Rehan Fazal katika Studio za BBC

Amina alimtengezea Mandela samosa

Amina baadaye alitoa mahojiano ambapo alisema kwamba kumbukumbu yake kubwa na Nelson Mandela ni kwamba alifika nyumbani kwake mara moja baada ya kuwa rais.

"Alikuwa amekaa kwenye kiti jikoni kwangu huku nikipika samosa," Amina alisema kwenye mahojiano hayo.

Amina anaandika katika wasifu wake kwenye kitabu 'Van Hope and History Rhyme' kwamba ‘’Mara moja, baada ya ndoa yake ya tatu na Grace Mitchell, Nelson Mandela alikuja kwenye gorofa yangu Johannesburg na kueleza waziwazi upendo wake kwangu.’’

‘’Nilipingana naye nikisema kwamba umefunga ndoa. Mimi niko huru lakini wewe hauko huru. Hapo Nelson Mandela alikasirika na licha ya kusema mara kwa mara kwamba nimekupikia samaki, alifunga mlango na kutoka nje.’’

.

Chanzo cha picha, GHALEB CHACHALIA/FACEBOOK

Amina anaandika zaidi katika wasifu wake kwamba 'Nelson Mandela hakuwa na mguso wa mahaba.

Labda alikuwa amepoteza hisia kwa sababu ya miaka yake aliyofungwa gerezani.

"Nilimpenda lakini si jinsi nilivyompenda marehemu mume wangu hata katika uzee wake. "

"Ilifikiriwa kuwa Nelson Mandela angekuwa bora kumuoa" Grace Mitchell, mjane wa rais wa Msumbiji, badala ya mwanamke wa Kihindi, na polepole akaelekea upande huo, anasema Saeed Naqvi.

Kulingana na yeye, madai haya hayawezi kuthibitishwa. Nani alimkubali na nani alimkataa mwenzake, lakini kwa hakika kulikuwa na kitu kati yao. Baada ya kuwaona kwa karibu, naweza kusema kwamba moto ulikuwa sawa kwa pande zote mbili.