Rafael Caro Quintero: Mmoja wa wahalifu waliosakwa zaidi na Marekani akamatwa Mexico

Mlanguzi wa dawa za kulevya kutoka Mexico Rafael Caro Quintero, mmoja wa watu wanaosakwa sana nchini Mexico na Marekani, alikamatwa Ijumaa hii katika jimbo la Sinaloa.

Ukamataji huo ulitokea katika operesheni ya pamoja ya Jeshi la Wanamaji na Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri (FGR) katika manispaa ya San Simón (Choix), Sinaloa.

"Lengo lilikuwa kwenye vichaka kwa kutumia mbwa wa taasisi, inayoitwa Max," Jeshi la Wanamaji lilisema katika taarifa.

Kwa upande wa Shirika la Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Marekani (DEA, kwa Kiingereza) lilithibitisha kuhusika kwake katika kumkamata mlanguzi huyo wa dawa za kulevya nchini Mexico, kama ilivyobainishwa na mkurugenzi wa shirika hilo, Anne Milgram, katika barua iliyowaandikia wafanyakazi wake iliyochapishwa Jumamosi.

Kwa kuongezea, Katibu wa Jeshi la Wanamaji aliripoti ajali ya helikopta ya Navy Black Hawk huko Los Mochis, Sinaloa, ambapo watu 14 walifariki na mmoja kujeruhiwa vibaya.

Rais wa Mexico, Andrés Manuel López Obrador, alituma salamu za rambirambi kwenye Twitter na kuhusisha ajali hiyo na kukamatwa kwa mlanguzi wa dawa za kulevya.

 Rais alieleza kuwa helikopta hiyo ilikuwa ikijiandaa kutua "baada ya kutimiza dhamira ya kusaidia wale waliotekeleza agizo la kukamatwa kwa Rafael Caro Quintero."

Jeshi la wanamaji liliamuru uchunguzi ufanyike kuhusu sababu za ajali hiyo.

Kuridhika kwa DEA

Hati mbili za kukamatwa na ombi la kurejeshwa Marekani zilitoa wa kukamatwa kwa uzito Caro Quintero.

Mwanzilishi mwenza wa kundi lililotoweka la Guadalajara anatuhumiwa kwa mauaji ya wakala wa Udhibiti wa Dawa za Kulevya (DEA) Enrique "Kiki" Camarena Salazar, ambayo yalitokea mwaka wa 1985.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani Merrick Garland alitoa taarifa kufuatia habari za kukamatwa kwake:

"Hakuna mahali pa kujificha kwa mtu ambaye huwateka nyara, kuwatesa na kuwaua maafisa wa kutekeleza sheria wa Marekani. Tunashukuru sana mamlaka ya Mexico kwa kukamata na kukamatwa kwa Rafael Caro Quintero," maandishi hayo yanasema.

"Kukamatwa huko leo ni hitimisho la kazi isiyo ya kuchoka ya DEA na washirika wa Mexico kumfikisha Caro Quintero mahakamani kwa makosa yake ya uhalifu, ikiwa ni pamoja na kumtesa na kumnyonga Wakala Maalum wa DEA Enrique "Kiki" Camarena. Arejeshwe nchini Marekani mara moja ili ahukumiwa kwa uhalifu huu katika mfumo ule ule wa mahakama ambao wakala maalum Camarena alikufa akiutetea," anaongeza.

Garland aliomboleza kifo cha wanajeshi hao 14 wa ajali hiyo ya helikopta.

Kwa upande wake mkuu wa DEA Anne Milgram alituma salamu za pongezi kwa wafanyakazi wote wa shirika hilo. 

"Kwa zaidi ya miaka 30, wanaume na wanawake wa DEA wamefanya kazi bila kuchoka kumfikisha Rafael Caro Quintero kwenye vyombo vya sheria. Kukamatwa kwake leo ni matokeo ya miaka ya damu, jasho na machozi. Bila kazi yao, Caro Quintero asingeweza kabiliana na haki. Asante. Ninashukuru kwa kila mmoja wenu."

Hatia na kutoroka

Ingawa alikuwa amezuiliwa tangu 1985 na alihukumiwa kifungo cha miaka 40 jela kwa mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya, Caro Quintero aliachiliwa mwaka wa 2013 kutokana na uamuzi wa mahakama wenye utata ambao ulitaja makosa ya kimamlaka ya kusikiliza kesi ya Camarena.

Siku chache baadaye, hakimu alitoa hati ya kukamatwa ya muda kwa ajili ya kurejeshwa nchini Marekani na Mahakama ya Juu ikabatilisha uamuzi uliomruhusu kuondoka gerezani lakini Caro Quintero hakuweza kupatikana tena.

Tangu wakati huo, serikali za Mexico na Marekani zimemweka kwenye orodha yao ya Wahalifu Wanaotafutwa Zaidi. Na mnamo 2015 alipata alikutwa na hatia kwa mauaji ya Camarena.

Narco wa Narcos

Akijulikana kama Mwana Mfalme au Narco de Narcos , Caro Quintero alikuwa mmoja wa watu mashuhuri katika siku za mwanzo za kupanga uhalifu na ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Mexico.

Kwa kufungwa kwake 1985, umuhimu wake ulipunguzwa, wakati huo huo genge la Guadalajara lilikuwa likipoteza ushawishi katika ulanguzi wa dawa za kulevya kutoka Mexico na Amerika Kusini hadi Marekani.

 Lakini, wakati huo, Caro Quintero alijulikana kama mzalishaji mkuu wa bangi nchini Mexico.

Nguvu zake kabla ya kukamatwa kwake

Katika moja ya mali zake, kufuatia kufanyika kwa operesheni kubwa zaidi dhidi ya dawa za kulevya katika historia ya nchi, zaidi ya tani 10,000 zilizokutwa zimepandwa katika shamba la El Bufalo ziliharibiwa.

Caro Quintero aliamuru kutekwa nyara kwa mtu aliyegundua shehena hiyo, wakala Camarena Salazar pamoja na rubani wa Mexico Alfredo Zavala Avelar.

Wote wawili waliuawa. Kifo cha afisa wa polisi wa Marekani, kilichotokea 1985 kilisababisha mzozo mkubwa zaidi katika uhusiano kati ya Mexico na Marekani.

Lakini pia iliashiria vita dhidi ya dawa za kulevya na serikali ya Washington.

Baada ya kuachiliwa kwake 2013, DEA ilitoa zawadi ya dola milioni 20 kwa habari ambayo ilisaidia kumkamata.

Oktoba 2020, Idara ya Haki ya Marekani ilifungua kesi ya madai katika mahakama ya Brooklyn, New York ili kutaifisha mali nane zilizotambuliwa nchini Mexico ikiwemo majumba ya kifahari, maghala na mashamba.

Wamiliki kadhaa maarufu wa dawa za kulevya, kama vile Joaquín Guzmán Loera, wanatoka katika manispaa hii.

Katika mahojiano aliyopewa mwanahabari Anabel Hernández, Bosi huyu wa dawa za kulevya alisema kuwa familia yake ilikuwa maskini sana na kwamba alilazimika kupanda bangi baada ya kifo cha babake.

Nilikuwa na umri wa miaka 14. Caro Quintero anasema kwamba hakukuwa na njia nyingine ya kuisaidia familia yake.

Badiraguato iko katika eneo la milima kati ya majimbo ya Sinaloa, Chihuahua na Durango na moja ya maeneo ya nchi yenye uzalishaji mkubwa wa bangi na poppy.

Kwa muda mfupi, Caro Quintero aliendelea na biashara

Akiwa na umri wa miaka 30, alikuwa mmoja wa washirika wakuu wa Miguel Ángel Félix Gallardo, anayejulikana kama bosi wa mabosi na kiongozi wa shirika kubwa la ulanguzi wa dawa za kulevya linaloshirikiana na makampuni ya Colombia kama vile Pablo Escobar Gaviria.

DEA iliita shirika lao kuwa kampuni ya Guadalajara baada ya jiji ambalo Mkuu wa Wakuu, Caro Quintero na viongozi wengine wa dawa za kulevya waliishi.

Udhaifu wa Mkuu

Tangu 1975, Guadalajara, mji mkuu wa jimbo la Jalisco umekuwa kimbilio la wafanyabiashara wengi wa dawa za kulevya na familia zao ambao waliwasili kutoka Sinaloa.

Miaka miwili nyuma, Serikali ya Mexico ilikuwa ilianzisha Operesheni Condor katika eneo la Golden Triangle huko milimani, mkakati wa kutokomeza kilimo cha bangi na poppy kutoka eneo hilo kaskazini-magharibi mwa Mexico.

Wakuu wa mashirika hayo, akiwemo Caro Quintero, waliondoka eneo hilo na kuishi katika mji mkuu wa Jalisco. 

Uwepo wa wakuu hao uliishtua serikali ya Marekani, ambayo ilituma timu ya DEA mjini. Enrique Camarena anayejulikana kama Kiki, alikuwa mmoja wao.

Kwa muda fulani viongozi wa dawa za kulevya hawakutambuliwa lakini hali ilibadilika katika miaka ya 1980.

Na moja ya sababu, wanahabari wa ndani kama Felipe Cobián waliiambia BBC Mundo, kulikuwa na wahusika wa ziada kama vile Caro Quintero.

Mlanguzi huyo wa dawa za kulevya alikuwa akiongoza kwa kashfa katika migahawa na vilabu vya usikum na hata alishutumiwa kwa kumteka nyara mpwa wa mwanasiasa mashuhuri wa eneo hilo, Guillermo Cosío Vidaurri, ambaye alikuwa gavana kati ya 1989 na 1992.

Alama ya DEA

Alama ya DEA

Lakini kesi mbaya zaidi ilikuwa mauaji ya Camarena. Afisa huyo alitekwa nyara Februari 1985 alipokuwa akiondoka kwenye ubalozi mdogo wa Marekani huko Guadalajara.

Kisha alipelekwa kwenye nyumba ya jirani pamoja na rubani Zavala Avelar. Wote wawili waliteswa na kisha kuuawa.

 Miili yao iliibuka wiki kadhaa baadaye katika jimbo la jirani la Michoacán

Caro Quintero alikimbilia Costa Rica ambapo alikamatwa Aprili 1985.

 Uchunguzi wa mauaji hayo ulibaini kuwa Mkuu huyo na genge la Guadalajara walikuwa wameunda mtandao mpana wa washirika miongoni mwa wanasiasa, wanajeshi na polisi.

Mauaji ya Camarena yalibadilisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Marekani ilitoa sehemu ya msaada wake kwa Mexico ili kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya.

Mchakato huu wa uidhinishaji, ambao kimsingi hupima kiwango cha ushirikiano wa nchi na serikali ya Marekani ulidumishwa hadi 2002.

Caro Quintero wakati huo alihukumiwa miaka 40 jela lakini aliachiliwa mwaka wa 2013.

Kwa DEA, mauaji ya Enrique Camarena yakawa alama. Kiuhalisia, "Wiki ya Utepe Mwekundu" ilianzishwa kwa heshima yake, kampeni ya kila mwaka ya elimu ya kupambana na madawa ya kulevya.