Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Man Utd yajutia uamuzi wa Rashford
Klabu ya Manchester United inajutia uamuzi wake wa kukubali kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford kwa Barcelona kwa £26m kwa sababu wanaamini kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 sasa ana thamani ya takriban £50m. (Star)
Beki wa Bournemouth na Argentina Marcos Senesi, 28, anataka kujiunga na kalabu ya Barcelona msimu huu wa joto baada ya kuamua hatasaini mkataba mpya na Cherries. (Team Tal)
Mshambuliaji Muingereza Liam Delap, 23, huenda akaondoka Chelsea msimu huu wa joto, na hivyo kuzua shauku kutoka kwa vilabu vikiwemo Manchester United, Newcastle na Everton. (Caughtoffside)
Manchester United wako tayari kumwachia winga wa Uingereza Jadon Sancho, 25, kuondoka bila malipo mwishoni mwa msimu huu. (Sun)
West Ham inaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Canada Promise David mwenye umri wa miaka 24 kutoka Union Saint-Gilloise. (Team Talk)
Tottenham huenda ikatumia fedha nyingi katika usajili wa msimu huu wa joto huku tetesi zikiibuka kwamba inanyatia kiungo wa Aston Villa Muingereza Morgan Rogers mwenye umri wa miaka 23. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Tottenham Richarlison anaweza kukihama klabu hicho, huku Flamengo na Atletico Madrid zikionyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 28. (Fichajes - kwa Kihispania)
Bayer Leverkusen wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Leon Goretzka kutoka Bayern Munich msimu huu wa joto, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 angependelea kuhamia Uingereza, huku Arsenal ikionyesha nia ya kimsajili. (Bild - kwa Kijerumani)
AC Milan ina imani kuwa kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric, 40, atasaini walau mkataba wa mwaka mmoja mwishoni mwa msimu huu. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)