Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Jumatano: Milango iko wazi kwa Toney kurejea ligi ya Primea
Mshambuliaji wa England mwenye miaka 29 Ivan Toney wa Al-Ahli anaweza kurejea kwenye ligi ya Premia.(Sky Sports)
Liverpool FC hawana mpango wa kumuuza kiungo wa Hungary mwenye miaka 25 Dominik Szoboszlai, licha ya kuhusishwa na Real Madrid CF, huku mazungumzo ya mkataba mpya yakiendelea.(Teamtalk)
Mshambuliaji wa Ujerumani mwenye miaka 24 Nick Woltemade hana furaha Newcastle United FC na angependa kurejea VfB Stuttgart au kujiunga na FC Bayern Munich.(Bild - in German)
Manchester United FC hawana nia ya kupunguza bei ya pauni milioni 26 kwa mshambuliaji wa England mwenye miaka 28 Marcus Rashford, ambaye yuko kwa mkopo FC Barcelona.(Mail)
Nicolas Jackson na Chelsea FC wataamua kuhusu mustakabali wake majira ya kiangazi kwa sababu FC Bayern Munich hawatarajiwi kumnunua mshambuliaji huyo wa Senegal mwenye miaka 24baada ya mkopo wake.(Mail)
Sunderland AFC wanataka kusajili mshambuliaji mpya kuchukua nafasi ya Mfaransa mwenye miaka 25 Wilson Isidor, ambaye anataka kuondoka.(Football Insider)
Atlético Madrid wanataka mshambuliaji wa Argentina mwenye miaka 26 Julián Álvarez asaini mkataba mpya, lakini klabu anayopendelea ni FC Barcelona.(Sport - in Spanish)
Tottenham Hotspur FC, Crystal Palace FC na West Ham United FC zinavutiwa na beki wa Ujerumani mwenye miaka 32 Antonio Rüdiger wa Real Madrid CF.(Fichajes - in Spanish)
Everton FC wanatarajiwa kukataa ofa yoyote kwa kiungo wa England mwenye miaka 27 Kiernan Dewsbury-Hall, anayevutiwa na Tottenham Hotspur FC.(Football Insider)
Mshambuliaji wa zamani wa England mwenye miaka 33 Jesse Lingard yuko karibu kujiunga na klabu ya Brazil Clube do Remo baada ya kuondoka FC Seoul Januari.(Sun)