Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Man City wamuwinda Rodrygo

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rodrygo
Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester City wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 24 Rodrygo, ambaye thamani yake ni pauni milioni 87. (Fabrizio Romano)

Nottingham Forest wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City James McAtee, 22. (Subscription requires)

Chelsea na RB Leipzig wamemjadili mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku, 27, wakati wa mazungumzo kuhusu mshambuliaji wa Uholanzi Xavi Simons, 22. (Talksport)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alexander Isak

Mshambulizi wa Uswidi Alexander Isak, 25, atafikiria tu kujumuishwa tena Newcastle au kusaini mkataba mpya ikiwa Liverpool watamjulisha moja kwa moja kuwa mpango hauwezekani msimu huu wa joto. (Givemesport)

West Ham wanaandaa ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Southampton mwenye umri wa miaka 21 wa Ureno Mateus Fernandes, ambaye thamani yake ni pauni milioni 30. (Guardian)

Monaco wana nia ya kumsajili beki wa zamani wa Newcastle mwenye umri wa miaka 34 Kieran Trippier. (Sky Sports)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rasmus Hojlund

Inter Milan, Roma, Juventus na Napoli wameungana na AC Milan kuonyesha nia ya kutaka kumnunua Rasmus Hojlund, huku Manchester United wakiwa tayari kufikiria dau la £30m-£40m kwa mshambuliaji huyo wa Denmark mwenye umri wa miaka 22. (Subcription required)

Uhamisho wa mkopo wa kiungo wa kati wa Uingereza Jack Grealish kutoka Manchester City kwenda Everton unajumuisha chaguo la pauni milioni 50 kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 msimu ujao wa joto.(Subcription required)

Chelsea wametuma ofa ya pauni milioni 43 kwa beki wa kati wa Liverpool na Ufaransa Ibrahima Konate, 26 . (Defensa Central -in Spanish)

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bilal El Khannouss

Newcastle pia wanavutiwa sana na kiungo wa kati wa Leicester City na Morocco Bilal El Khannouss, 21, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Leeds. (Telegraph)

Brentford na Newcastle wako kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Stade Rennais Mfaransa Arnaud Kalimuendo, huku The Bees wakiwa wamesonga mbele kidogo katika mazungumzo ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (L'Equipe - In French)

Everton wanavutiwa na winga wa Leicester Mghana Abdul Fatawu mwenye umri wa miaka 21 baada ya kushindwa katika ombi nyingi za kumnunua winga wa Southampton mwenye umri wa miaka 19 wa England aliye na umri wa chini ya miaka 21 Tyler Dibling. (Sky Sports)

g

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Maelezo ya picha, Dominic Calvert-Lewin

Dominic Calvert-Lewin amemfuta kazi wakala wake alipokuwa akijaribu kutafuta klabu mpya. Mshambulizi huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28 amefanya mazungumzo na Manchester United, Newcastle na Leeds. (Sport)

Chelsea wanafikiria kumnunua mlinzi wa Bayer Leverkusen na Ecuador Piero Hincapie, 23, kufuatia beki wa kati wa England mwenye umri wa miaka 22 Levi Colwill kuumia vibaya goti. (Caughtoffside)

Wolfsburg wanavutiwa na beki wa pembeni wa Sunderland wa Ireland Kaskazini Trai Hume, 23. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 34, ana nia ya kusalia Manchester City hadi mwisho wa dirisha la usajili la majira ya joto licha ya Galatasaray kumtaka. (Football Insider)

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi