Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Wirtz kufanyiwa vipimo Liverpool

Chanzo cha picha, Getty Images
Florian Wirtz anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya Liverpool baada ya kufikiwa makubaliano ya awali na Bayer Leverkusen kwa ajili ya kiungo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 22, kujiunga na Liverpool kwa thamani ya pauni milioni 127 ikiwa ni pamoja na nyongeza mbalimbali. (Fabrizio Romano)
Arsenal wamekubaliana ada ya takriban pauni milioni 59 na Real Sociedad kwa ajili ya kiungo wa Uhispania Martin Zubimendi, mwenye umri wa miaka 26, ambapo uhamisho huo utatekelezwa baada ya tarehe 1 Julai ili kusaidia kutimiza masharti ya kanuni za Kifedha (Financial Fair Play - FFP). (AS - in Spanish)
Manchester United wanatathmini ofa kwa ajili ya mshambuliaji wa Napoli raia wa Nigeria Victor Osimhen, mwenye umri wa miaka 26, kwa kumtumia mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 24, kama sehemu ya dili hilo. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko mwenye umri wa miaka 22 anayechezea RB Leipzig anayehusishwa na Arsenal, alikataa kujiunga na klabu ya Saudi Arabia ya Al-Hilal kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Jumanne. (Star)
Leipzig wanasisitiza kulipwa ada kamili ya kuvunja mkataba wa Sesko, ambayo sasa inaeleweka kuwa ni zaidi ya pauni milioni 65. (Independent)
Beki wa kushoto raia wa Hungary Milos Kerkez, 21, yuko karibu kuhamia Liverpool kwa pauni milioni 45 baada ya Bournemouth kukubali kumsajili beki wa kushoto wa Ufaransa Adrien Truffert, 23, kutoka Rennes. (Telegraph)
Newcastle United wameanzisha mazungumzo na Burnley kuhusu kumsajili kipa wa Kiingereza James Trafford, mwenye umri wa miaka 22. (Times)
Gianluigi Donnarumma anataka kubaki na Paris St-Germain licha ya Manchester United na Inter Milan kuonesha nia ya kumsajili kipa huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 26. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Brighton wako tayari kupokea ofa ya kati ya pauni milioni 50 hadi 60 kwa ajili ya mshambuliaji wa Brazil Joao Pedro mwenye umri wa miaka 23, ambaye ni chaguo muhimu la Newcastle United. (Football Insider)
Chelsea wako tayari kupokea ofa kwa Benoit Badiashile, 24, pamoja na beki mwingine wa Ufaransa Axel Disasi, mwenye umri wa miaka 27. (Football Insider)
Inter Milan wana nia ya kumsajili kiungo wa Paraguay Julio Enciso mwenye umri wa miaka 21 kutoka Brighton msimu huu wa joto. (Teamtalk)
Jaribio la Al-Hilal kumsajili kiungo wa Ufaransa N'Golo Kante, mwenye umri wa miaka 34, kwa mkataba wa muda mfupi kutoka kwa wapinzani wao wa Saudi Arabia Al-Ittihad kwa ajili ya Kombe la Dunia la Klabu linaweza kuvunjika kutokana na upinzani kutoka kwa mashabiki. (Talksport)















