Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanajeshi wa Urusi walio vitani kuruhusiwa kugandisha mbegu zao za kiume bure -TASS
Wanajeshi wa Urusi ambao wamekuwa katika sehemu ya harakati za operesheni za kijeshi nchini Ukraine watakuwa na haki ya kupata mbegu zao za kiume zigandishwe bure, shirika la serikali la TASS liliripoti Jumatano.
Ikimnukuu Igor Trunov, rais wa Muungano wa Wanasheria wa Urusi, TASS iliripoti kwamba Wizara ya Afya ilijibu ombi lake la usaidizi wa bajeti kufanikisha mpango huo.
Wizara "iliamua uwezekano wa msaada wa kifedha kutoka kwa bajeti ya shirikisho kwa uhifadhi wa bure wa seli za vijidudu (spermatozoa) kwa raia waliopelekwa kushiriki katika operesheni maalum ya kijeshi ya 2022-2024", Trunov alinukuliwa akisema
Familia pia zinaweza kutumia vifaa vya kibayolojia (Biomaterial)iliyohifadhiwa bila malipo ikiwa bima yao ya matibabu ya lazima itaonyesha wanaweza kufanya hivyo.
Urusi iliwaita zaidi ya askari wa akiba 300,000 kuunga mkono kile inachoita "operesheni yake maalum ya kijeshi" nchini Ukraine katika harakati ya uhamasishaji iliyozinduliwa mwezi Septemba.
Hatua hiyo ilisababisha mamia kwa maelfu ya wanaume wa Urusi kukimbia kutoka nchini humo ili kukwepa kujiunga na jeshi, na kuzua maandamano makubwa zaidi dhidi ya Kremlin tangu Urusi ilipotuma wanajeshi wake nchini Ukraine mwezi Februari.
Vita hivyo, ambavyo Ukraine na washirika wake wa Magharibi wanaviita uchokozi usiozuiliwa wa kunyakua ardhi viko katika mwezi wake wa 11, vikiwa vimeingia katika hatua ya polepole huku hali ya hewa ya baridi kali ikianza.