Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Putin awaambia mama wa wanajeshi wa Urusi anayahisi maumivu yao
"Tunayahisi maumivu yenu ," Rais wa Urusi Vladimir Putin ameliambia kundi la mama wa wanajeshi wa Urusi ambao wamekuwa wakipigana vita - na ambao baadhi yao wameuawa – nchini Ukraine.
"Hakuna kitu chochote kinachoweza kulinganishwa na kumkosa mtoto wako wa kiume", alisema katika hotuba yake ya ufunguzi, iliyoonyeshwa kwenye vyombo vya habari vya taifa la Urusi.
Akina mama kadhaa ni wajumbe wa vuguvugu linalounga mkono utawala wa Urusi. Wakosoaji wanasema akina mama hao walichaguliwa kwa uangalifu.
Ndani ya Urusi, upinzani dhidi ya uvamizi wa Ukraine umekuwa ukiendelea kuongezea.
Kote nchini Urusi, makundi ya akina mama wa wanajeshi wanaohudumu wamekuwa wakilalamika wazi kwamba watoto wao wa kiume wanapelekwa katika vita huku wakiwa na mafunzo duni ya kijeshi na hawapewi silaha zinazofaa na nguo, hususan wakati huu ambapo msimu wa baridi kali unakuja.
Baadhi pia walilishutumu jeshi la Urusi kwa kuwageuza wale waliolazimishwa kuingia vitani "vifaa vya kutumiwa", kufuatia kushindwa vibaya kwa jeshi katika miezi ya hivi karibuni.
Wanajeshi wapatao 100,000 wa Urusi na wanajeshi 100,000 wa Ukraine wameuawa au kujeruhiwa tangu vita vilipoanza tarehe 24 Februari, kulingana na Jenerali wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani, Mark Milley.
Katika taarifa yake ya nadra, Urusi ilikiri kuwa katika mwezi Septemba makosa waliyoyafanya ni ari yake ya kuwaingiza jeshini wanajeshi wa akiba.
Katika mkutano wa Ijumaa uliofanyika katika makazi yake ya kitaifa yaliyopo karibu na mji mkuu Moscow, Bw Putin alionyeshwa akiwa amekaa kwenye meza moja na kikundi cha akina mama 17. Baadhi yao walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi kichwani – ishara ya kuomboleza.
"Ninataka ninyi mjue kuwa mimi mwenyewe binafsi, na uongozi wote wa nchi, tunahisi maumivu haya ," rais alisema.
Aliwaambia mama mmoja kuwa mwanaye wa kiume alikuwa "amefikia lengo lake" na " hakufa bure".
Bw Putin alisema kuwa alitaka kukutana na mama hao ana kwa ana kusikiliza kutoka kwao wenyewe kuhusu hali ya mambo katika maeneo yao.
Ana alifichua kuwa mara kwa mara amekuwa akizungumza moja kwa moja na wanajeshi wa Urusi walioko katika uwanja wa mapigano, akiwaelezea kama "mashujaa".
Rais pia aliwataka akina mama hao kutoamini taarifa "feki" na "uongo" kuhusu vita vinavyoendelezwa kweye televisheni na intaneti.
Huku ikiwa ni vigumu kupata taarifa zisizoegamia upande wowote kuhusu hali nchini Ukraine ni vigumu, nchini Urusi kwasababu ya udhibiti wa vyombo vya habari wa utawala wa Kremlin, watu wengi wanapata habari kwa kutumia mitandao binafsi ya habari (VPNs) kukwepa ukandamizaji wa vyombo vya habari.
Katika taarifa kuhusu mkutano huo iliyochapishwa na ofisi ya Rais saa kadaa baadaye, baadhi ya wanawake walitambuliwakama wanawake ambao ni sehemu ya vuguvugu linalomuunga mkono Putin.
Wanawake hao walikuwa kutoka sehemu mbali mbali za Urusi, ilisema taarifa, huku mmoja wao akitoka katika jimbo lililojitangaza kama Jamuhuri ya watu wa Luhansk katika mashariki mwa Ukraine, ambalo Urusi ilitangaza kulitwaa mapema mwaka huu.
Mjumbe wa kundi la All-Russian Popular Front linaloungwa mkono na utawala wa Urusi pia alikuwa pale pamoja na washiriki kutoka Shirika la Combat Brotherhood , ambalo hukusanya misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wanajeshi wa Urusi.