Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Manchester City inawataka Florian Wirtz na Bruno Guimaraes
Manchester City inawataka Florian Wirtz na Bruno Guimaraes, Chelsea na Liverpool wanavutiwa na Milos Kerkez, na Je, Dusan Vlahovic anaelekea Arsenal Januari?
Kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 21, na kiungo wa kati wa Newcastle wa Brazil Bruno Guimaraes, 27, wanafuatiliwa na Manchester City. (Times - subscription required)
Kocha wa Man City Pep Guardiola pia atapata uungwaji mkono kumsajili kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi mwenye umri wa miaka 25. (ESPN)
Chelsea na Liverpool wanatazamiwa kumwinda mlinzi Milos Kerkez, 21, lakini Bournemouth watafanya kila wawezalo kumbakisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia. (Football Insider)
Mikel Arteta anataka kumuongeza mlinzi wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic, 24, kwenye kikosi chake cha Arsenal mwezi Januari. (Caught Offside)
Real Madrid wamejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mlinzi wa AC Milan Theo Hernandez, 27, na kurahisisha kazi kwa Manchester United wanaomtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. (Fichajes - in Spanish)
Gary O'Neil ana mechi ya Jumamosi dhidi ya Ipswich Town ili kuokoa kazi yake kama kocha wa Wolves. (Football Insider)
Bournemouth wanataka meneja Andoni Iraola atie saini mkataba mpya kutokana na hofu kwamba klabu nyingine za Ligi ya Primia zinaweza kumlenga Mhispania huyo. (TBR Football)
RB Leipzig wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi wa Paris St-Germain Xavi Simons, 21, kwa mkataba wa kudumu, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Liverpool. (Caught Offside)
Manchester United wamefikia makubaliano ya mdomo na Cerro Porteno kumnunua beki wa pembeni wa Paraguay, Diego Leon, 17. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 32, anaweza kuuzwa na Manchester United mwezi Januari iwapo kutapatikana ofa ya kuvutia. (Florian Plettenberg)
Everton wanapanga kumnunua winga wa Lyon na Ghana Ernest Nuamah, 21, mwezi Januari. (Football Insider)
Kundi linaloongozwa na Dan Friedkin linakaribia kufikia makubaliano ya kuinunua Everton, huku ununuzi ukikamilika wiki ijayo. (Times - subscription required)
Kocha wa Everton Sean Dyche hatarajiwi kufutwa kazi mara moja baada ya Kundi la Friedkin kununua klabu hiyo. (Football Insider)
Tottenham hawana mpango wa kuchagua kumsajili kwa mkopo kwa mkataba wa kudumu mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 28, kutoka RB Leipzig mwishoni mwa msimu. (GiveMeSport)
Imefasiriwa na Asha Juma