Tyson Fury v Anthony Joshua: Ni pambano lenye mvuto kimataifa?

Fury-Joshua

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwaka mmoja uliopita, Tyson Fury v Anthony Joshua lilikua pambano kubwa lililovutia mashabiki wa Uingereza, na bila shaka ulimwengu wote wa ndondi, ulitamani sana lifanyike. Pambano hilo la hadhi ya juu kwa mabondia hao waingereza kuwania mikanda yote mikubwa ya uzito wa juu lilikiwa likiwakutanisha mabingwa hao wa dunia wenye haiba mbili tofauti. Mambo yalikuwa tayari, maelezo zaidi yalikubaliwa, huku Saudi Arabia ikipangwa kuandaa pambano hilo mnamo Agosti 2021. Lakini Fury badala yake aliamriwa na kikao cha usuluhishi kumkabili kwanza Deontay Wilder kwa mara ya tatu.

Kuanzia hapo ni kama maendeleo ya mabondia hao yanechukua njia tofauti, inaonekana kama pambano la Fury-Joshua - au Joshua-Fury kulingana na utii wako - ni kama meli inayozama. Kama pambano la kawaida kiasi.

Fury-Joshua

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Fury

Joshua amepoteza mapambano matatu kati ya matano ya mwisho aliyipigana na hana taji la dunia, huku Fury asiyetabirika - ambaye wiki iliyopita alionekana katika ulimwengu wa burudani wa World Wrestling Entertainment - aliwahi kutangaza kustaafu kwa zaidi ya mara moja. Lakini katika hali ambayo haikutarajiwa, bingwa wa WBC Fury alijitikeza na kumpa 'chalenji' Joshua kupitia mitandao ya kijamii tarehe 5 Septemba. Siku ya Jumanne, Joshua, kulingana na kampuni yake ya usimamizi, alikubali masharti ya kupigana na Fury mnamo 3 Desemba. Kama pambano hilo litafanyika kama ilivyopendekezwa, je bado litakuwa ni pambano kubwa la zama za kisasa? Au mvuto wake unepungua, na je, kuna mapambano mengine makubwa zaidi ya kufanyika badala ya hili?

Usyk-Fury ni pambano kubwa kuliko Fury-Joshua?

Fury-Joshua

Chanzo cha picha, Getty Images

Hakuna ubishi pambano linalowakutanisha mabingwa wasiopingika katika uzito wa juu zaidi duniani, lilikuwa na mvuto mkubwa mwaka jana.

Hakujawa na bingwa wa uzani wa juu asiyepingika tangu enzi ya mikanda minne ilipoanza mwaka wa 2004. Lennox Lewis alikuwa bingwa wa mwisho wa uzito wa juu asiyepingwa miaka 22 iliyopita.

Baadhi ya mashabiki, hata hivyo, wanaona bora kumuona Fury akikabiliana na bingwa wa WBA, IBF na WBO Usyk.

Huo kwao ni pambano linalowakutanisha mambondia wakali wawili ambao hawajashindwa, walio na na tabia "tabia tata" za kipekee.

Wengine wangeuliza maswali ya fitina zaidi; Je, Fury ni mkubwa sana, na je, Usyk anahitaji kujidhihirisha kama gwiji wa uzani mzito akiwa amepambana na wapinzani watatu pekee kwenye uzani huo tangu ahamie kutoka uzani wa cruiser? Fury-Joshua linasalia kuwa pambano kubwa lenye kivutio kikubwa kibiashara na kwa mashabiki wa ndondi duniani kote, lakini Fury-Usyk anaweza kuvutia hadhira ya kimataifa zaidi. Hata hivyo, kwa kuwa Usyk alisema hatarejea ulingoni hadi mwaka 2023, labda pambano la Fury-Joshua kwa sasa ni pambano lenye kuleta maana zaidi.

Je Joshua "kaisha"?

Fury-Joshua

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Joshua alichapwa na Usky hivi karibuni

Mnamo Juni 2019, Joshua alipitia usofurahisha alipopigwa kwa mara ya kwanza kama bondia wa kulipwa na bondia Andy Ruiz Jr wa Mexico aliyeondoka na ushindi wa kushangaza huko New York. Msbindi huyo wa medali ya dhahabu ya ndondi ya Olimpiki ya London 2012, alitolewa katika raundi ya saba kwenye ukumbi maarufu wa Madison Square Garden.

Hata hivyo, miezi sita tu baadaye alirejesha ubingwa wake wa duni kwa ushindi wa pointi moja katika mechi ya marudiano. Baada ya ushindi wa kawaida dhidi ya Kubrat Pulev mnamo Desemba 2020, Joshua alisema pambano na Fury linaweza kuwa kubwa zaidi katika historia ya ndondi ya Uingereza. Lakini mnamo Septemba 2021, alipoteza mataji yake tena - wakati huu dhidi ya mpinzani aliyepaswa kuzichapa nae kwanza Usyk huko London.

Pambano dhidi ya Fury kumpaisha AJ?

Fury-Joshua

Chanzo cha picha, Getty Images

Hali ya kimwili ya Joshua ndiyo mada ya mjadala mkubwa kwa sasa. Bingwa wa zamani wa uzito wa juu Carl Froch alihoji kama Joshua amekuwa "mtu aliyekata tamaa" tangu kupoteza pambano lake dhidi ya Ruiz Jr. Baada ya kuchapwa na Usyk huko Jeddah, gadhabu na hisia za Joshua katika mahojiano ya baada ya pambano pia ulisababisha ukosoaji mkubwa. Hata hivyo kuanzia chapa za nguo hadi vinywaji vya kuongeza nguvu, hear phones hadi watengenezaji wa magari, Joshua ana ahadi nyingi za ufadhili na kuingiza pesa za matangazo.

Lakini watu wengine, kama vile Froch, wanahisi moyo wake unaweza kuwa haupo tena kwenye mchezo huo. Ikiwa hivyo ndivyo, pengine ukubwa wa pambano la Fury - ambalo hakika litateka, angalau, mawazo ya umma wa Uingereza - linaweza kuwa chanzo cha kumsaidia Joshua kurejea kwenye hadhi yake.