Iran: Uwepo wa ndege za kivita za Marekani aina ya B-52 hautaathiri mipango yetu ya kujilinda

Muda wa kusoma: Dakika 4

Ismail Beqaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba, kuwepo kwa ndege za kivita za B-52 katika eneo hilo hakutaathiri azma ya Iran ya kujilinda.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitangaza jana kuwa imetuma ndege hizo za kimkakati katika eneo hilo kama onyo kwa Iran.

Idadi na eneo zilizopo ndege hizo halijawekwa wazi .

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia alisema kuwa Iran itajibu "kwa nguvu zake zote"uingiliaji wowote au ukiukaji wowote wa usalama wa taifa hilo na uingiliaji wa ardhi yake " na itajitayarisha kwa kila kitu kinachohitajika kwa "ulinzi".

Ismail Beqaei pia alisema kwamba mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani yaliyohusu suala la nyuklia, yamesitishwa katika wiki mbili au tatu zilizopita.

.Hossein Salami, kamanda wa Jeshi la Iran amezionya Israel na Marekani katika ujumbe wake wa kuadhimisha tarehe 13 Novemba kwamba watajibu vikali kupitia jeshi la Iran.

Amesema "Mapambano ya Kiislamu katika eneo hilo... yatajibu vikali kila uovu, na kwa namna hii, makabiliano ya Iran yataimarishwa kwa kila kinachohitajika ili kukabiliana na kumshinda adui’’

Pia unaweza kusoma

Rais Masoud Bishikian pia alisema katika kikao cha jana cha Serikali kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitaacha kujibu"ukiukaji wwowote wa usalama wa taifa hilo kutoka nje njia yoyote ile.

Sambamba na hayo amesema iwapo viongozi wa Israel watazingatia upya mienendo yao, kukubali usitishaji vita na kuacha kuwaua watu wasio na hatia wa eneo hilo, kunaweza kuvutia hatua kali kutoka kwa taifa hilo.

Iran ilishambulia Israel kwa makombora na ndege zisizokuwa rubani na mara moja kwa mamia ya makombora. Wiki iliyopita, Israel ilianzisha mashambulizi ya anga katika maeneo kadhaa ya ulinzi wa anga na vifaa vinavyohusiana na utengenezaji wa makombora ya balistiki nchini Iran.

Katika siku za hivi karibuni, mamlaka nchini Iran zimeahidi kujibu shambulio hili, ambalo limepewa jina maarufu "Sadegh 3".

Mkutano wa Kamanda wa Centcom na Mkuu wa Jeshi la Israeli

Mkuu wa Jeshi la Marekani Mashariki ya Kati) alikutana na kamanda wa jeshi la nchi hiyo, Herzi Halevi, nchini Israel.

Bw. Holloway alikuwa msimamizi wa operesheni ya kijeshi ya Israel dhidi ya Iran wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Israel, katika mkutano huu uliofanyika siku ya Alhamisi, pande hizo mbili zilijadili "matishio ya kikanda, hasa kutoka Iran".

Wakati wa safari yake nchini humo, kamanda wa Centcom pia alitembelea mfumo wa ulinzi wa makombora wa Tad Ham ambao Jeshi la Marekani lilituma hivi karibuni nchini Israel.

Jeshi la Marekani pia limetangaza kwamba ndege kadhaa za kimkakati za B-52 zimetumwa Mashariki ya Kati, siku moja baada ya Pentagon kutangaza kutumwa Iran kama "onyo".

Katika ujumbe kwenye mtandao wa X siku ya Jumamosi, Marekani ilithibitisha kuwasili kwa washambuliaji hao kutoka Minet Air Base hadi eneo linalodhibitiwa na CENTCOM, lakini haikutaja idadi eneohasa la washambuliaji hao.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin aliamuru kutumwa kwa washambuliaji hao pamoja na vifaa vingine Korea.

Bwana Austin ameonya kuwa Marekani itachukua hatua zozote zinazohitajika iwapo Iran itawalenga wafanyakazi wa Marekani au maslahi yake katika eneo hilo.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Martha Saranga na kuhaririwa na Dinah Gahamanyi