Mwanajeshi aliyezikwa bila ubongo wake

o

Chanzo cha picha, Libby MacRae

Maelezo ya picha, Donnie MacRae alikulia Gairloch na alikuwa fundi nguo
    • Author, Emily Esson
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Mwanajeshi wa Scotland, Donnie MacRae alikufa akiwa mfungwa wa vita huko Ujerumani wakati wa Vita vya Pili vya Dunia baada ya karibu miaka 80 familia yake ndipo ilipogundua alizikwa bila ubongo wake.

Donnie alikufa katika hospitali ya PoW mwaka 1941 na kwa sababu alikuwa na tatizo katika mfumo wa mishipa ya fahamu, maiti yake ilifanyiwa uchunguzi.

Wakati wa uchunguzi wa maiti, ubongo wake na sehemu ya uti wa mgongo vilitolewa na kupelekwa katika Taasisi ya Kaiser Wilhelm ya Magonjwa ya Akili huko Munich ili kutumika kwa utafiti.

Mwili wake ulizikwa na Wajerumani na baadaye kuzikwa tena na Jeshi Washirika (Uingereza, Marekani, Sovieti, na China), katika makaburi ya Commonwealth War Graves huko Berlin lakini hakuna aliyejua ubongo wake ulikuwa umetolewa.

Kwa jumla, takribani vipande vidogo 160 vya ubongo na uti wa mgongo wa Donnie vilihifadhiwa katika kituo cha utafiti cha Munich, na kisha baadaye kituo hicho kikabadilishwa jina kuwa Max Planck Society.

Historia ya Donnie

kj

Chanzo cha picha, Libby MacRae

Maelezo ya picha, Donnie MacRae alikufa akiwa mfungwa wa vita na akazikwa huko Berlin

Donnie MacRae alikulia huko Gairloch katika mji wa pwani wa magharibi ya Scotland. Mwaka 1939, nchi hiyo ikiwa ukingoni mwa vita, Donnie alijiunga na Jeshi la Akiba na aliitwa kupigana.

Alikuwa kuruta katika kikosi cha Seaforth Highlanders na alikamatwa kama mfungwa wa vita alipokuwa akipigana huko St Valery, Ufaransa, Juni 1940. Alikufa mwaka uliofuata, akiwa na umri wa miaka 33, katika hospitali ya wafungwa wa vita.

Ingawa familia yake ilijua kuhusu kukamatwa na kifo cha Donnie, hawakuwahi kuelezwa kuhusu uchunguzi wa maiti, au kuhusu sampuli kuchukuliwa kutoka katika ubongo wake.

Mwaka 2020, Profesa Paul Weindling kutoka Chuo Kikuu cha Oxford Brookes alipowasiliana na familia yake, ndipo mpwa wa Donnie, aitwaye Libby MacRae alipofahamu kilichotokea baada ya kifo cha Donnie.

Prof Weindling ni sehemu ya kundi la kimataifa la watafiti wanaochunguza rekodi za maelfu ya bongo za watu ambazo zipo katika Kituo cha Max Planck Society nchini Ujerumani. Lengo la mradi huu ni kuwatambua waathiriwa wote na kuwakumbuka ipasavyo.

Alipokamatwa alikuwa amejeruhiwa kwa risasi katika goti la kushoto na mgongoni. Ingawa jeraha lilipona lakini alirudishwa hospitalini baada ya hali yake kudhoofika miezi iliyofuata.

Tafiti za Kisayansi

dsz

Chanzo cha picha, Libby MacRae

Maelezo ya picha, Libby Macrae mpwa wa Donnie
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ugonjwa ulianza kwa kuwa na tatizo la kuona vitu viwili viwili, akitetemeka kwenye vidole vyake na tatizo la kushindwa kuzungumza vizuri. Ugonjwa huo lilisababisha kupooza mikono yote miwili na kushindwa kuongea.

Siku chache kabla ya kifo chake hakuweza tena kutembea. Donnie alifariki tarehe 6 Machi 1941 kutokana na kupooza, kwa sababu ya ugonjwa uitwao Landry's Paralysis - ambapo mfumo wa kinga hushambulia mfumo wa neva.

Wajerumani walitaka kuwa mstari wa mbele katika tafiti za matibabu na ndio sababu iliyofanya ubongo wa Donnie kupelekwa katika taasisi ya Munich.

Uchunguzi wa maiti ulifanyika, na ndipo ubongo wake ulipotolewa. Vipande vya ubongo na uti wa mgongo wa Donnie vilichukuliwa ili vitumike kutafiti ugonjwa wake.

Prof Weindling na timu yake waligundua rekodi za wafungwa wengine wanne wa kivita wa Uingereza ambao waliondolewa ubongo zao kwa madhumuni ya utafiti mwaka 1941.

Patrick O'Connell, Donald McPhail, Joseph Elston na William Lancaster. Walikuwa miongoni mwa watu wapatao 2,000 ambao bongo zao zilichukuliwa kwa utafiti na taasisi za Berlin na Munich wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, zikiwemo bongo za watoto waliouawa wakati wa mauaji ya Holocaust.

Waathiriwa ni pamoja na Wayahudi wa Poland na Wakatoliki, waliokuwa na ugonjwa wa akili, wafungwa wa kisiasa, waasi wa Ubelgiji na wanajeshi wa Ufaransa na Poland. Taasisi nyingine za Ujerumani pia zinajulikana kuwa zimevuna sehemu za mwili kwa ajili ya utafiti.

Dk Hildebrandt anasema matokeo ya tafiti kutoka taasisi za Ujerumani yalikuwa makubwa, na watafiti kote ulimwenguni walikuwa na wivu kutokana na mafanikio hayo.

Baada ya Vita

fc

Chanzo cha picha, Paul Weindling

Maelezo ya picha, Donnie MacRae alizikwa tena katika makaburi ya Vita ya Jumuiya ya Madola huko Berlin

Baada ya vita, Jeshi la Washirika walichunguza uhalifu wa Nazi na kufungua Kesi ya Nuremberg, karibu watu 200 walipatikana na hatia ya uhalifu wa kivita.

Hata hivyo, taasisi za utafiti za Kaiser Wilhelm na zile nyingine waliruhusiwa kuendelea na kazi yao. Ni kutokana na ukweli kwamba, ingawa kwa sasa ni kinyume cha maadili kuchukua tishu za binadamu bila idhini, wakati huo ilikuwa kawaida.

Sampuli za Donnie MacRae zilishikiliwa kwa madhumuni ya utafiti hadi 2015, ndipo zilipowekwa kwenye mkusanyiko wa kumbukumbu.

Hivi karibuni, tume ya Makaburi ya Vita ya Jumuiya ya Madola ilikubali kupokea sampuli ya ubongo na uti wa mgongo wa Donnie kutoka Taasisi ya Max Planck na kuziunganisha na mabaki ya mwili wake ambao tayari umezikwa kwenye kaburi lake huko Berlin.