Watu 38 miongoni mwao watoto waliofariki katika shambulio la shule ya chekechea

Chanzo cha picha, Reuters
Polisi wa zamani amewauwa watu 38, wengi wao wakiwa ni watoto, katika shambulio la bunduki na kisu katika shule ya chekechea kaskazini -mashariki mwa Thailand.
Polisi inasema baada ya kuwauwa alijiua mwenyewe na familia yake baada ya msako kufuatia shambulio hilo lililotokea katika jimbo la Nong Bua Lamphu.
Watoto na watu wazima ni miongoni mwa waliouawa katika kituo hicho cha chekechea - polisi wanasema polisi aliwapiga risasi na kuwatunga kisu wahanga kabla ya kutoroka kutoka kwenye eneo la tukio.
Afisa huyo wa zamani wa polisi mwenye umri wa miaka 34, alifutwa kazi kwa kutumia madawa ya kulevya mwezi Juni, polisi ilisema.
Mwalimu ambaye alinusurika na aliiambia televisheni ya Thailand-Thairath TV kwamba mshambuliaji alikuwa akimleta mtoto katika shule hiyo ya chekechea na alionekana mtu muungwana. Sababu ya shambulio hilo haijajulikana wazi.
Takriban watoto 22 walikuwa ni miongoni mwa watu waliokufa katika mauaji hayo ya watu wengi katika mji wa Utthai Sawan.
Baadhi ya wahanga walikuwa ni watoto wadogo wenye umri wa miaka miwili ambao walishambuliwa walipokuwa wamelala. Watu kumi na mbili waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya A Nong Bua Lamphu.

Chanzo cha picha, EPA
"Mshambuliaji alikuja majira ya saa za chakula cha mchana na kuwapiga risasi maafisa wanne au watano katika kituo hicho kwanza," afisa wa eneo, Jidapa Boonsom, aliyekuwa akifanya kazi karibu, aliliambia shirika la habari la w Reuters .
Mmoja wao alikuwa ni mwalimu ambaye alikuwa ana ujauzito wa miezi minane.
"Kwanza watu walifikiria ni milio ya baruti," alisema, na kuongeza kuwa mwanaume huyo aliingia kwa nguvu skatika chumba kilichofungwa ambako watoto walikuwa wamelala.
Video zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wazazi waliokuwa wanalia na wenye mkanganyiko na jamaa wa wale waliouawa, wakati walipokuwa wakikusanyika nje ya kituo hicho.
Maafisa wa polisi waliofika baada ya shambulio walikumbana na matukio ya kuogofya, miili ya watu wazima na watoto, baadhi yao wakiwa ni wadogo sana, ikiwa imelala ndani na nje ya jengo.
Waziri mkuu wa Thailand Prayuth Chan-ocha alielzea tukio hilokama "tukio la kushtua".

Polisi imesema Kamrab alirejea nyumbani, akampiga risasi mke wake na mtoto wakee wa kiume kanla ya kujiua mwenyewe.
Ufyatuaji wa risasi dhidi ya watu wengi nchini Thailand ni wa nadra, ingawa viwango vya umiliki wa bunduki ni vya juu katika kanda hiyo. Umiliki wa silaha kinyume cha sheria pia ni jambo la kawaida kmwa nchi hiyo ya kusini- mashariki mwa Asia, kulingana na shirika la habari la Reuters.
Shambulio shule ya chekechea linakuja chini ya mwezi mmoja baada ya afisa wa jeshi kumpiga risasi na na kumuua mwanajeshi mwenzake katika ngome ya kijeshi mjini Bangkok.
Katika mwaka 2020 mwanajshi aliwauwa watu 29 na kuwajeruhi wengine 12 zaidi katika mji wa Ratchasima.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Chanzo cha picha, EPA
Polisi imesema Kamrab alirejea nyumbani , akampiga risasi mke wake na mtoto wakee wa kiume kanla ya kujiua mwenyewe.
Ufyatuaji wa risasi dhidi ya watu wengi nchini Thailand ni wa nadra, ingawa viwango vya umiliki wa bunduki ni vya juu katika kanda hiyo.
Umiliki wa silaha kinyume cha sheria pia ni jambo la kawaida kmwa nchi hiyo ya kusini- mashariki mwa Asia, kulingana na shirika la habari la Reuters.












