Mashambulizi ya Makiivka: Je ndiyo yaliyosababisha vifo vingi zaidi vya wanajeshi wa Urusi kwa wakati mmoja?

Chanzo cha picha, Reuters
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imethibitisha vifo vya askari wake 63 wakati wa shambulio la makombora katika shule ya ufundi huko Makeyevka. Lakini mamlaka za Ukraine zilidai wanajeshi 400 waliuawa, Je, hili ni shambulio lililosababisha madhara makubwa zaidi katika jeshi la Urusi?
Idara ya jeshi la Urusi hapo awali imeripoti madhara hadharani mara mbili tu - mwanzoni mwa Machi na mwishoni mwa Septemba 2022. Katika visa vingine vyote, Wizara ya Ulinzi haikutoa takwimu na maelezo yoyote ya ziada juu ya vifo vya wanajeshi.
Hata hivyo, matukio kuuawa kwa wakati mmoja wanajeshi wa Urusi yanajulikana kwa uhakika.
Takwimu za madhara katika taarifa hii inatokana na orodha ya watumishi wa Kirusi waliothibitishwa kufa, ambayo BBC inazibeba kwa kushirikiana na Mediazona (unaotambuliwa nchini Urusi kama "wakala wa vyombo vya habari vya kigeni") na timu ya watu wa kujitolea kulingana na vyanzo mbalimbali vya wazi.
Mashambulizi katika uwanja wa ndege wa Gostomel: Angalau wanajeshi 27 waliuawa
Katika siku ya kwanza ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, askari wa miamvuli walitua kwenye uwanja wa ndege wa Gostomel karibu na Kyiv. Idadi kamili ya Warusi waliokufa wakati wa operesheni hii haijulikani. Wavamizi hao walipata madhara katika siku ya kwanza ya shambulio hilo.
Lakini kutokana na data iliyochunguzwa na BBC, askari wa miamvuli wa Urusi walidhurika zaidi ya mara moja huko Gostomel mnamo Machi 6, wakati wanajeshi na maafisa 27 wa vikosi vya anga waliuawa.
Kimsingi, walikuwa wakihudumu katika Brigade ya 31 ya Airborne. Idadi halisi ya vifo siku hii inaweza kuwa kubwa zaidi. Wizara ya Ulinzi ya Urusi haijaweka wazi idadi ya waliouawa wakati wa dhoruba ya Gostomel.

Chanzo cha picha, MAKEEVKA ADMINISTRATION
Kuzama kwa cruiser "Moskva": Angalau wanajeshi 22 walikufa
Usiku wa Aprili 13-14, jeshi la Kiukreni liliishambulia meli ya kombora ya Moskva, ambayo ilikuwa kwenye Bahari Nyeusi. Kama matokeo ya uharibifu wa shambulio hilo, meli ilizama. Ni watu wangapi walikuwa kwenye meli na mabaharia wangapi walikufa haijulikani kwa hakika.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema kwanza kwamba bendera ya Meli ya Bahari Nyeusi ya Urusi ilizama wakati ikivutwa hadi bandarini "katika hali ya mawimbi ya dhoruba" na kukiri kifo cha mtu mmoja.
Watu 27 walitajwa kupotea. Kulingana na data wazi kutoka kwa BBC, Mediazone (iliyojumuishwa na mamlaka ya Urusi katika rejista ya mawakala wa vyombo vya habari-kigeni) na watu waliojitolea waliweza kuainisha majina ya wafanyakazi 22 wa Moskva ambao walikufa wakati meli hiyo ilipozama.
Mnamo Novemba, 2022 mahakama ya Kirusi ilitangaza kuwa mabaharia 17 wa meli ya Moskva wamefariki, lakini haikuhusisha hili na vita vya Ukraine. Wakati huu wote, mabaharia waliokufa waliorodheshwa kama "waliopotea."
Mapambano katika kijiji cha Moshchun: Angalau wanajeshi 21 walikufa
Katika siku za kwanza za mwezi Machi, jeshi la Urusi liingia mji wa Kyiv kutoka pande kadhaa. Moja ya umwagaji damu zaidi ilikuwa vita katika kijiji cha Moshchun katika wilaya ya Buchansky ya mkoa wa Kyiv.
Mnamo Machi 6, askari na maafisa wa Marine Corps walipoteza angalau maafisa 21 waliuawa walipokuwa wakijaribu kuchukua udhibiti wa makazi haya. Wengi wa waliokufa walihudumu katika Brigade ya 155 ya Wanamaji.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi haikuripoti hasara yoyote wakati wa mapambano haya kwenye kijiji hiki.
Kushambuliwa kwa Kikosi maalum "Mercury". Angalau maafisa 18 walikufa

Chanzo cha picha, EPA
Mnamo Julai 19, Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine vilishambulia jengo ambalo lilikuwa ngome ya kikosi maalum cha Walinzi wa Urusi "Mercury".
Waandishi wa habari wa Ukraine waliripoti kuwa maafisa 18 walikufa, hakukuwa na ripoti rasmi kutoka upande wa Urusi. Lakini jamaa za waliofariki walitaja idadi hiyo hiyo. Makumi ya watu zaidi walijeruhiwa.
BBC ilifanikiwa kuthibitisha majina ya makomando 10 wa Mercury waliofariki. Wizara ya Ulinzi ya Urusi haikutoa maoni yoyote juu ya shambulio hili.
Kwa kuzingatia ukosefu wa habari kutoka upande huo, ni ngumu kusema ikiwa makombora ya PTU huko Makeyevka ndio yaliyosababisha madhara ama vifo vingi zaidi vya wanajeshi wa Urusi. Lakini tukio hili la sasa ni dhahiri limesababisha madhara makubwa ya wakati moja na yanaayotambuliwa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi.












