Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 28.08.2023

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo wa Wolves Matheus Nunez

Manchester City wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Matheus Nunes baada ya kuwasilisha ofa iliyoboreshwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Express)

Mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ureno Joao Felix, 23, ametambuliwa na Liverpool kama mbadala wa Mohamed Salah wa Misri, iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 atahamia Saudi Arabia. (A Bola – In Portugueese)

Mchezaji anayelengwa na Manchester United Marcus Alonso "amefanya uamuzi wake" juu ya uhamisho unaowezekana wa kwenda Old Trafford kutoka Barcelona, huku Mashetani Wekundu wakimuona Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 32 kama mbadala wa Luke Shaw aliyejeruhiwa. (Express)

Alonso yumo kwenye orodha fupi ya United ambayo pia inamjumuisha beki wa pembeni wa Chelsea na Uhispania Marc Cucurella, 25. (Daily Star)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marcos Alonso

Beki wa Tottenham Hotspur Sergio Reguilon, 26, ni jina lingine kwenye orodha hiyo, lakini Fulham wako mbele ya Manchester United katika harakati za kumsaka Mhispania huyo. (Telegraph – Sunscription Required)

Mshambulizi wa Ureno Beto, 25, yuko mbioni kukamilisha uhamisho wa £24m kutoka Udinese ya Serie A kwenda Everton, huku Toffees wakitamani kufanya biashara zaidi kabla ya tarehe ya mwisho ya kuhama Ijumaa. (iNews)

AS Monaco wamerejea kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa Uingereza Tosin Adarabioyo, 25, kutoka Fulham na mazungumzo yanaendelea. (Fabrizio Romano)

Everton wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa Borussia Dortmund na Uswizi Nico Elvedi, 26. (Gianluca di Marzio)

.

Chanzo cha picha, BBCsport

Maelezo ya picha, Romelu Lukaku

Roma wameibuka kuwa vinara wanaowania kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 30. (Fabrizio Romano)

Tottenham Hotspur wanatazamia kuzindua uhamisho wa pauni milioni 50 kumnunua mshambuliaji wa Nottingham Forest na Wales Brennan Johnson, 22. (Evening Standard)

Marco Verratti yuko mbioni kuhama kutoka Paris St-Germain hadi Al-Arabi, baada ya klabu hiyo ya Saudi Arabia kukubaliana ada na timu hiyo ya Ufaransa kwa ajili ya kiungo huyo wa kati wa Italia mwenye umri wa miaka 30. (Soka Italia)

Nottingham Forest inavutiwa na mlinda mlango wa Wolves Jose Sa, 30, huku mchezaji anayelengwa kwa muda mrefu Dean Henderson akikaribia kuhamia Crystal Palace. (Football Insider)

Fulham wanatafuta kumsajili beki wa pembeni wa Ubelgiji Timothy Castagne, 27, kutoka Leicester City. (Fabrizio Romano)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Amrabat

Napoli watashindana na Manchester United kumnunua kiungo wa Fiorentina na mchezaji wa kati wa Morocco Sofyan Amrabat, 27. (Marca - in Spanish)