"Unaangalia nini, mjinga": Simulizi kuhusu hasira za Lionel Messi ambayo imeenea mitandaoni

.

Chanzo cha picha, MEAN PA

Maelezo ya picha, lionel Messi

"Unaangalia nini, mjinga. Nenda huko."

Maneno haya ambayo Lionel Messi alitamka Ijumaa iliyopita wakati wa mahojiano baada ya mechi kati ya timu za Argentina na Uholanzi katika robo fainali ya Kombe la Dunia yameenea kwa kasi katika siku za hivi karibuni.

Kwa kiasi kwamba yamewekwa katika kila aina ya vyombo vya habari: memes, video za TikTok, nyimbo, kofia, t-shirt, au vikombe .

Lakini, je, tusi la nyota huyo wa Argentina lililonaswa na kamera za televisheni lilielekezwa kwa nani?

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Weghorst

Mvutano ndani na nje ya uwanja

Mechi kati ya Waajentina na Waholanzi iliyomalizika kwa ushindi wa mikwaju ya penalti iliambatana na mvutano katika dakika za mwisho za muda wa kawaida, huku bao la Wout Weghorst likiisawazishia Uholanzi 2-2 na kuifanya mechi kuamuliwa na muda wa ziada.

Kulikuwa na makabiliano kadhaa kati ya wachezaji wa timu zote mbili na baadhi ya rabsha mwishoni mwa mechi ambayo Waajentina walionekana kushinda lakini hadi dakika ya 100..

Baada ya mechi Leo Messi alifanya mahojiano na kituo cha michezo cha TyC na kabla ya kuanza kujibu maswali alionekana kwenye video akiangalia upande mmoja kwa mbali na kusema: "Unaangalia nini wewe mjinga? Unaangalia nini wewe mjinga? nenda huko."

Katika picha hizo haikuonekana matamshi ya nahodha huyo wa Argentina yalikuwa yakielekezwa wapi.

Baadaye ilifahamika kutokana na video nyengine iliorekodiwa kwa wakati kwamba Messi alikuwa akizungumza na Weghorst, mchezaji aliyechangia magoli mawili ya Uholanzi.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 1

Hatahivyo, mwisho wa mechi Weghorst alimwendea Messi, kulingana na yeye, kwa nia ya kumpa mkono na kumuomba shati lake, lakini Messi alikataa.

Katika picha hizi za pili mchezaji wa Uholanzi anaonekana akigombana na Waajentina Lautaro Martínez na 'Kun' Agüero, ambaye yuko Qatar mchanganuzi .

Kulingana na Agüero, wakati nahodha huyo wa Argentina alipokuwa akijiandaa kufanya mahojiano yake, Weghorst katika mtazamo wa uchochezi alimtazama kwa mbali na kusema 'Hey, Messi, hey, Messi'.

Hapo ndipo nyota huyo wa Argentina alipomwambia "Unaangalia nini, mjinga".

Weghorst pia alitoa toleo lake la kile kilichotokea baada ya tukio katika mahojiano.

"Nilitaka kumpa mkono baada ya mchezo, namheshimu sana kama mchezaji wa mpira, lakini alitupa mkono wangu kando na hakutaka kuzungumza nami. Kihispania changu sio kizuri sana lakini alisema maneno ya dharau. kwangu na hilo linanikatisha tamaa, nimesikitishwa sana,” mchezaji huyo alisema.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 2