Maji huingiaje kwenye nazi au dafu? Fahamu mchakato wake wa ajabu

Chanzo cha picha, Getty Images
Je, umewahi kushangaa kuona maji ndani ya nazi unapoivunja? Umewahi kujiuliza jinsi maji hayo yalivyoingia ndani?
Je, maji matamu, baridi ndani ya ganda la nazi juu ya mti yakoje?
Maji safi yana virutubishi ambavyo hukata kiu na kutoa nishati papo hapo wakati wa kiangazi.
Nazi changa, yenye rangi ya kijani kibichi, ina maji mengi ukilinganisha na nazi iliyokomaa, ambayo hugeuka rangi ya kahawia.
Muundo wa nazi

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnazi unaitwa 'mti wa uzima' kwa sababu kila sehemu ya mnazi ni muhimu kwetu kwa namna fulani.
Miti ya nazi hupatikana katika maeneo ya nchi za kitropiki kote duniani.
Kabla ya kuelewa jinsi maji huundwa ndani ya ganda la nazi, tunahitaji kujua muundo wake.
Nazi ina matabaka matatu kwa jina exocarp, mesocarp, na endocarp.
Exocarp ni safu ya nje ya tunda hilo ambalo ni kijani na laini.
Sehemu ya nyuzi chini ya safu ya kijani inaitwa mesocarp. Endocarp ni msingi wa ndani - inalinda 'nyama' nyeupe na laini ndani ambayo hubadilika na kuwa mgumu nazi inapokomaa.
Ya pili ni maji ndani. Maji huingia wakati nazi inapokua.

Chanzo cha picha, Getty Images
Je, maji huingia vipi ndani ya nazi?
Kulingana na utafiti wa Kituo cha Kitaifa cha Habari za Bayoteknolojia cha Marekani, maji kwenye nazi ni kioevu kilichochujwa.
Utafiti huo unapendekeza kuwa maji hutoka kwenye mizizi hadi kwenye nazi kupitia mfumo wa mishipa (mfumo wa kusafirisha maji na virutubisho) kwenye mti.
Utafiti huu ulielezea mchakato wa uundaji wa maji ndani ya ganda la nazi.
Mizizi ya nazi huenea kutoka ardhini hadi katika kina cha mita 1 hadi 5. Mizizi hii inachukua maji ya chini ya ardhi yenye virutubisho kutoka kwenye udongo unaozunguka. Kisha maji haya hubebwa juu kupitia shina lake na hatimaye kufikia mnazi.
Muundo wa 'endocarp' wa nazi uhifadhi maji haya.
Utomvu huu wa maji wenye virutubishi hutengeneza koko nyeupe (nazi) inapokomaa.
Maji ya nazi baadaye huingia katika nazi.
Je, ni kiwango gani cha maji kilichopo katika nazi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kuna sababu nyingi zinazoathiri kiasi na ubora wa maji katika nazi.
Mojawapo ni umri wa nazi. Nazi changa imejaa maji. Nazi ambazo zina umri wa miezi sita hadi minane huchukuliwa kuwa changa. kwasababu zina 300 ml kwa lita moja ya maji.
Nazi zilizokomaa, ikimaanisha zile zilizo na umri wa miezi 12 au zaidi, zina maji kidogo. Zina maji kidogo kwa sababu endosperm, eneo la ndani, hufyonza maji.
Mvua pia ina jukumu katika hili. Mvua nyingi inamaanisha maji mengi hufika kwenye nazi. Wakati minazi inakua katika maeneo kame, maji kidogo hufika kwenye nazi, na hivyo kusababisha maji kidogo kuzalishwa ndani yake.
Miti iliyopandwa kwenye udongo wenye madini mengi hupokea maji ya hali ya juu na yenye virutubisho.
Ikiwa udongo hauna madini mengi au hauwezi kusafirisha virutubisho kutoka kwenye mizizi hadi kwenye matunda, ubora wa maji utakuwa wa wastani.
Miti isiyo na afya, yenye magonjwa hutoa matunda madogo na huwa na maji kidogo sana.
Kwa kufuata kanuni za kilimo endelevu, kama vile kupima udongo na kutumia mbolea asilia, tunaweza kuhifadhi virutubisho kwenye minazi, na hivyo kuzalisha maji safi yenye ubora.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












