Je, Iran ilitengeneza vipi kombora la hypersonic ambalo linaweza kufika Israel kwa 'sekunde 400' licha ya vikwazo?

g
Maelezo ya picha, Teknolojia ya kombora la Balistiki ilitengenezwa wakati wa Vita vya Pili vya Dunia lakini ni nchi chache ulimwenguni ambazo zina uwezo kama huo.
Muda wa kusoma: Dakika 8

Na Farzad Seifikaran

Mwandishi wa BBC

Katika giza la usiku wa Aprili 13, 2024, na kuba la dhahabu la Msikiti wa Al-Aqsa kwa nyuma, mwanga wa kombora la balistiki la Iran ulijitokeza kwa mara ya kwanza kwenye picha ambayo pengine ulimwengu utaikumbuka kwa muda mrefu.

Shambulio hilo la kombora na ndege zisizo na rubani na Iran lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuuangusha mfumo maarufu wa ulinzi wa Israel unaojulikana kama Iron Dome.

Makombora ya balestiki na ndege zisizo na rubani zilizorushwa kutoka Iran zilipiga maeneo mbalimbali nchini humo, ikiwemo uwanja wa ndege wa Israel.

Shambulio hilo lilirudiwa takriban miezi sita baadaye mnamo Oktoba 1, 2024.

Walinzi wa Mapinduzi ya Iran walirusha idadi kubwa ya makombora kuliko hapo awali na kulenga shabaha zaidi za Israel kuliko hapo awali.

Kulingana na William Alberc, mtafiti katika Taasisi ya Stimson na mkurugenzi wa zamani wa mpango wa udhibiti wa silaha wa NATO, shambulio la hivi karibuni la Iran limebadilisha hali ya Mashariki ya Kati milele.

Kumbuka kwamba shambulio hili liliwezeshwa na mpango wa makombora wa Iran, ambao umekuwa ukiendelea kwa kasi ya kushangaza kwa miongo kadhaa, na serikali ya Irani ina imani sana na mpango huu kwamba neno 'pointi' linatumika kwa makombora haya kwa sababu ya uwezo wake wa kupiga malengo.

Hivyo mpango huu wa makombora unazidi kuwa tatizo kubwa kwa ulimwengu wa Magharibi na Israel pamoja na baadhi ya nchi za Kiarabu katika Mashariki ya Kati.

Mpango huu wa makombora ni nini? Iran ina makombora ya aina gani na yameendelezwa kiasi gani? Je, mpango wa makombora wa Iran umekuwaje wa hali ya juu licha ya vikwazo hivi vyote? Hebu tupate majibu ya maswali haya.

Unaweza pia kusoma:

Safari ya mafanikio ya mpango wa makombora wa Iran licha ya vikwazo

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Khamenei amesema mpango huo wa makombora unaozitia wasiwasi nchi za Magharibi ulitengenezwa wakati wa vikwazo.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa mujibu wa taasisi ya amani ya Marekani, Iran ina silaha kubwa zaidi na tofauti zaidi ya makombora ya balistiki katika Mashariki ya Kati. Kando na hayo, Iraq ndiyo nchi pekee katika eneo hilo ambayo haina silaha za nyuklia, lakini makombora yake ya balistiki yanaweza kushambulia hadi umbali wa kilomita 2,000.

Teknolojia ya makombora ya balistiki ilitengenezwa wakati wa Vita vya pili vya dunia , lakini ni nchi chache sana ulimwenguni ambazo zina uwezo wa kutengeneza makombora ya balistiki kwa kutumia teknolojia hii zenyewe.

Iran imepata teknolojia hii na kutengeneza makombora ya balistiki katika miongo miwili iliyopita licha ya vikwazo vikali vya kimataifa. Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei alisema katika hotuba yake ya hivi karibuni kwamba mipango ya kijeshi na makombora ambayo yalizivuruga nchi za Magharibi yote yalitengenezwa wakati wa vikwazo hivyo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio mwaka 2006. Chini ya azimio hilo, Iran ilipigwa marufuku kuuza silaha za nyuklia au nyenzo zake. Pia ilijumuisha bidhaa ambazo zingeweza kutumika kwa madhumuni mengine yoyote na kwa madhumuni ya kijeshi.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio jingine miezi mitatu baadaye na pia kuweka vikwazo vya mikataba ya kawaida ya silaha na Iran. Pia inajumuisha teknolojia ya kijeshi. Pamoja na mpango wa nyuklia wa Iran, mpango wa makombora ya balistiki pia ulikuja chini ya wigo wa vikwazo vilivyowekwa chini ya pendekezo hilo.

Hivyo haikuwa rahisi kwa Iran kununua silaha kutoka nchi kama vile Urusi na China. Wakati wa vita vya Iraq, Iran ilikuwa ikinunua bidhaa kutoka nchi zote mbili.

Makombora ya balistiki yana uwezo wa kutoa silaha za nyuklia, na kwa mujibu wa nchi za Magharibi, Iran inapopata teknolojia ya makombora ya balistiki, itafanya kila juhudi kupata nishati ya nyuklia na kurutubisha uranium inayohitajika kutengeneza silaha za nyuklia.

h

Chanzo cha picha, TASNIM

Maelezo ya picha, Kombora la balistiki la 'Scud B' lenye uwezo wa kushambulia umbali wa kilomita 300

Kufuatia kukamilika kwa makubaliano ya mpango kamili wa utekelezaji kati ya Iran na madola sita makubwa duniani mwezi Julai 2015 na kuidhinishwa kwa 'Pendekezo 2231', vikwazo vyote vya Baraza la usalama la umoja wa mataifa dhidi ya Iran viliondolewa.

Hata hivyo, vikwazo vya silaha viliendelezwa na kifungu kinachojulikana kama "njia ya kufyatua risasi". Chini ya mpango huo, mpango wa makombora wa Iran ulipaswa kufuatiliwa kwa karibu kwa miaka mitano. Ilikuwa ni njia ya kuweka shinikizo kwa Iran na kuzuia mpango wake wa makombora.

Kwa hakika Iran imeendeleza mpango wake wa makombora kiasi kwamba mwezi Machi 2016, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zilimwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa barua ya pamoja ikiishutumu Iran kwa majaribio ya makombora na kusema kuwa Iran imekiuka sheria ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Azimio nambari 2231” baada ya makubaliano ya JCPOA ” limekiukwa.

Hatimaye, mwaka 2020, rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliamua kujiondoa kwenye makubaliano hayo. Moja ya sababu zilizoifanya Marekani kujiondoa katika makubaliano hayo ni kwa sababu ya tishio la mpango wa makombora wa Iran na kukosekana kwa utaratibu unaofaa wa kufanya majaribio ya mpango huo.

Ijapokuwa Iran imejaribu kuonyesha kuwa ni sehemu ya mpango wa utekelezaji wa Umoja wa Mataifa, serikali ya Iran imetangaza kuwa itanunua silaha kutoka Urusi na China mnamo Oktoba 2021, huku muda wa mwisho wa azimio nambari 2231 ukikamilika. Kwa vile vikwazo bado vipo, matakwa ya Iran hayakuweza kutimizwa.

Tangu wakati huo Iran imetengeneza zaidi ya aina 50 za roketi, makombora ya balistiki na cruise, pamoja na ndege zisizo na rubani za kijeshi, ambazo baadhi yake zimetumika katika mizozo ya kimataifa kama vile vita kati ya Urusi na Ukraine.

g

Chanzo cha picha, TASNIM

Maelezo ya picha, Hassan Tehrani Muqaddam na Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Khamenei

Wakati wa Vita vya Iraq na Iran, silaha za kivita za Iran zilikuwa na umbali wa kilomita 35, wakati jeshi la Iraq lilikuwa na makombora ya balistiki ya Scud B yenye umbali wa kilomita 300, yakilenga miji kadhaa ndani ya Iran.

Huku jeshi la Iraq likipata nguvu katika mashambulizi ya makombora, Iran nayo ilifikiria kutumia makombora, na kiongozi mkuu wa Iran wakati huo, Ruhullah Khomeini, aliiruhusu Iran kukabiliana na mashambulizi hayo ya makombora.

Shambulio la kwanza la kombora dhidi ya Irani na Iraq lilikuwa mnamo Machi 21, 1985. Ililenga mji wa Kirkuk. Siku mbili baadaye shambulio lingine la Iran lilifanyika kwenye Klabu ya Maafisa wa Jeshi la Iraq huko Baghdad, na kuua makamanda 200 wa Iraqi.

Nchi za Kiarabu na Libya ziliandamana baada ya shambulio hili la kombora la Iran. Washauri wa Libya kisha waliondoka Iran na kuzima mfumo wa makombora na kurusha kabla ya kuondoka.

Katika hali hiyo, kundi la wanachama wa Jeshi la Anga la Iran lilianza jaribio la kombora lenyewe. Kikundi kidogo cha RIGC kilianza uhandisi wake wa nyuma kwa kufungua vipuri vidogo vya roketi na vifyatuzi

v

Chanzo cha picha, TASNIM

Maelezo ya picha, Awamu ya pili na mbaya zaidi ya mpango wa makombora wa Iran ilianza kwa utengenezaji wa kombora la Fatah 110.

Hassan Tehrani Muqaddam anaitwa baba wa mpango wa makombora wa Iran. Katika makala iitwayo 'Programu ya Kombora Zero kwa Mia Moja', Hassan Tehrani anasema kwamba wanachama 13 wa Walinzi wa Mapinduzi walipelekwa Syria kwa mafunzo ya makombora ya balestiki ya Scud baada ya washauri wa Libya kuondoka Iran. Alielewa kazi ya kombora la Scud ndani ya muda mdogo.

Muqadam aliteuliwa kuwa Kamanda wa Makombora wa Jeshi la anga la Iran mnamo 1986. Kisha mnamo 1988, Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Irani kilianza juhudi kubwa za kuunda makombora.

Katika miaka ya 1990, Korea Kaskazini na kisha China pia walijitokeza kusaidia Iraq na mpango wake wa makombora. Kwa sababu hiyo, majaribio ya baadhi ya mataifa makubwa duniani kutaka China kuwa sehemu ya 'utawala wa kudhibiti teknolojia ya makombora' hayajafanikiwa.

Udhibiti wa Teknolojia ya Makombora ni makubaliano ya kisiasa yasiyo rasmi kati ya nchi 35 wanachama ili kupunguza uzalishaji, ukuzaji na teknolojia ya makombora. China haikukubali kuwa mshiriki wake, lakini ilihitaji kujitolea kufuata masharti ya makubaliano hayo.

Roketi za 'Naejat' na 'Mujtama' zilikuwa roketi za kizazi cha kwanza kutengenezwa nchini Iran. Mara tu baada ya hapo, kombora la 'Thunder 69' lilitengenezwa. Kwa kweli ni kombora la masafa mafupi la Uchina B610, iliyoundwa upya kwa vikosi vya jeshi la Irani.

Awamu ya pili na mbaya zaidi ya mpango wa makombora wa Iran ilianza kwa utengenezaji wa kombora la Fatah 110.

Kwa mujibu wa Iran, Hassan Muqaddam alikuwa akijiandaa kwa jaribio jipya la kombora wakati milipuko miwili ilipotokea na kuuawa katika mlipuko wa pili. Sababu halisi ya mlipuko huo haikujulikana kamwe, lakini jiwe la kaburi la Hassan Muqadam lilisemekana kumzika mtu ambaye alitaka kuiangamiza Israel.

Hivi sasa, Kikosi cha wanaanga cha walinzi wa mapinduzi, kinachoongozwa na Amir Ali Hajazada, ndicho chombo kikubwa zaidi cha kutengeneza makombora na ndege zisizo na rubani kwa vikosi vya jeshi la Iran. Kwa kweli, kwa miaka kadhaa iliyopita, shirika hili limefanya kazi kwa Irani nje ya nchi badala ya jeshi la Irani.

Mji wa makombora ulio chini ya ardhi

g

Chanzo cha picha, IMA

Vyombo vya habari vya Iran na walinzi wa mapinduzi wametoa picha kadhaa za maghala ya makombora ya chinichini kufikia sasa.

Iran inaendelea kuonyesha kombora na silaha zake za kijeshi kama mafanikio makubwa, lakini mpango wake wa makombora na maendeleo ya maghala ya makombora ni siri.

Kamanda wa jeshi la anga la IRGC Amir Ali Hajizada alizungumza kwa mara ya kwanza mwaka 2014 kuhusu vituo hivyo vya kuhifadhia makombora vilivyojengwa mita 500 chini ya ardhi katika mikoa mbalimbali ya Iran.

Hakuna habari ya kuaminika inayopatikana kuhusu wakati maghala haya ya chini ya ardhi yalijengwa. Katika mahojiano na gazeti la Al Jazeera, Mehdi Bakhtiari, mwandishi wa idara ya kijeshi ya shirika la habari la Iran amesema kuwa, ghala la kwanza la kuhifadhia makombora ya chini ya ardhi magharibi mwa Iran lilijengwa mwaka 1984, na hapo ndipo mpango wa makombora wa Iran ulipoanza.

Picha ya moja ya ghala hizo za siri za chini ya ardhi inaaminika kuwa ghala la pili kwa ukubwa. Inahifadhi silaha muhimu zaidi za kombora na droni za Walinzi wa mapinduzi.

Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi kilitangaza mnamo Machi 2019 'mji wa kombora la bahari' kwenye mwambao wa Ghuba ya Uajemi. Mahali halisi ya kituo hicho hakikufichuliwa kama hapo awali, lakini vyombo vya habari vya ndani katika mkoa wa Harmuzkan viliripoti kuhusu msingi huo.

Kamanda Mkuu wa Walinzi wa mapinduzi wa Iran, Hossein Salami, alipokuwa akizungumzia 'Mji wa Kombora wa Marion' katika mwambao wa Ghuba ya Uajemi, alisema kuwa kiwanja hiki ni moja ya vituo vya jeshi la majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, ambapo makombora ya kistratejia yanahifadhiwa.

Hakuna anayejua idadi kamili ya maghala kama hayo ya chini ya ardhi ya makombora ambayo Iran inayo, lakini kamanda wa jeshi la Iran Ahmad Raza Pordistan alitangaza Januari 2014 kwamba mji wa chini ya ardhi wa makombora haukuwa wa Walinzi wa Mapinduzi pekee.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi