Wazee wenye uraibu wa mitandao ya kijamii: 'Tulimzimia intaneti mama yangu'

Muda wa kusoma: Dakika 7

Katika makazi ya familia ya Ester katika kitongoji cha São Paulo, Wi-Fi imezimwa. Mlezi mwenye umri wa miaka 38 na ndugu zake pia wamejiepusha na matumizi ya simu za mkononi kila wanapokuwa pamoja.

Uamuzi wa ghafla wa familia hiyo kuacha kutumia simu wakati huo ni jaribio la kumrejesha mtu mmoja wa familia hiyo"katika maisha halisi": Mama wa Ester mwenye umri wa miaka 74.

"Amekuwa akijitenga sana: anaingia na simu yake ya mkononi hadi bafuni, analala nayo chini ya mto wake, hachangamani na watu na wala haturuhusu kuikaribia simu yake.Amekuwa kama mtoto," anaelezea Ester, ambaye alipendelea kutotaja jina la mama yake na la familia ili kukwepa aibu.

Unaweza pia kusoma

Watoto wake walifikia hatua ya kuondoa SIM kadi kwenye simu ya mama yao ili kumzuia kupata mtandao kwa lengo la kumkwamisha kuingia kwenye Facebook na TikTok.

"Tulizima Wi-Fi na tukaondoa kadi ya simu kwenye simu yake kwa sababu hakukuwa na suluhisho lingine," Ester anaelezea.

Kisa cha familia ya São Paulo kinaonyesha jambo ambalo limejitokeza katika utafiti wa hivi karibuni juu ya matatizo yanayosababishwa na uraibu wa simu za mkononi: "nomophobia."

Sio ugonjwa wala kuchanganyikiwa, lakini viashiria kadhaa vinavyohusishwa na matumizi hatarishi ya vifaa vya umeme.

Katika baadhi ya matukio,kama hofu ya kukaa bila kutumia simu ya mkononi inaweza kumfanya mtu awe na hali ya wasiwasi kuweza kutokwa jasho nyingi au mapigo ya moyo kwenda kasi.

Matumizi makubwa ya simu yanahusishwa na kuzorota kwa afya ya akili, na dalili za kupata mfadhaiko, huzuni na wasiwasi, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanywa na mtaalamu Renata Maria Santos kama sehemu ya udaktari wake katika Kitivo cha Tiba cha Chuo Kikuu Minas Gerais (UFMG).

Kilichomshangaza zaidi mtafiti, ambaye huwafuata wagonjwa katika Hospitali ya UFMG das Clínicas huko Belo Horizonte, alibaini athari zaidi kwa wazee.

"Tulidhani kwamba wazee wangechukia teknolojia, huenda kwa sababu ya ugumu wa kuitumia au kwa sababu ya kutoweza kufahamu kirahisi,hali ambayo ingekuwa kikwazo kuzoea vizuri vifaa hivi," anasema Santos, ambaye alichambua na kuchapisha karatasi 142 za utafiti unaohusisha watu milioni 2 duniani kote.

"Lakini tulichogundua ni kwamba watu wameshikamana sana na kifaa hiki,kiasi kwamba wanakuwa na wasiwasi kuhusu kujitenga[nomophobia]."

Kwa maneno mengine, ugumu wa wazee wengi kukumbuka nenosiri, kupakua programu au kujua jinsi ya kufikia tovuti sio kikwazo tena

Wataalamu ambao BBC News Brasil ilizungumza nao wanasisitiza kwamba simu za mkononi zinaweza kuwa kifaa muhimu katika kuboresha maisha ya wazee (kwa kuwasiliana na familia, kwa mfano).

Lakini kuna mambo fulani ambayo huwafanya wazee kuwa hatarini zaidi kwa kusababisha uwezekano wa kuwa tegemezi:

  • Kujitenga na upweke;
  • Kujihisi "kutengwa" na ulimwengu wa sasa
  • Viwango vya juu vya changamoto za kihisia na mihemko kama vile sonona.

Hali hizi, Pamoja na kupungua kwa uwezo wa kutambua utamaduni wa kidijitali, zinaweza pia kuwafanya watu wazee kuwa na uwezekano mkubwa wa kuathirika au kuwa waraibu wa michezo, anaeleza mwanasaikolojia Cecília Galetti, ambaye ni mtaalamu wa gerontology, sayansi inayochunguza hali ya kuzeeka.

"Ni kama mchezo wa mpira wa theluji. Mzee aliyetengwa nyumbani na mwenye sonona ana hatari zaidi kukumbwa na tabia za uraibu," anaeleza Galetti, ambaye anashirikiana na wataalamu katika chuo kikuu cha USP (São Paulo).

Zaidi ya hayo, "mojawapo ya vigezo vya kiuchunguzi ili kutambua uraibu wa mchezo wa kamari, kwa mfano, ni ikiwa mtu huyo anacheza kamari ili kuepuka hali ya sonona."

"Nilikuwa mraibu"

"Simu yangu Ilikuwa kama sehemu ya maisha yangu na ilinibidi kuwa karibu nayo kila wakati. Vinginevyo, nilihisi kama nilikuwa nikipungukiwa kitu."

Simulizi ya Maria Aparecida Silva, mstaafu mwenye umri wa miaka 70 kutoka São Paulo, ilianza wakati alipogundua kuwa alikuwa mraibu, mnamo 2021.

Brazil ilikuwa bado katika mtego wa janga la Covid-19, na simu yake ikawa kifaa pekee kilichomuunganisha na ulimwengu.

Aparecida, ambaye anaishi peke yake, anakumbuka kwamba "alianza kuingia na simu yake ya mkononi kitandani na hakuweza kulala," na kwamba "aliacha kufanya kazi za nyumbani ili kuendelea kutumia."

Alitumia muda wake mwingi kwenye Facebook, programu ambayo "inavutia umakini wetu vizuri," alisema.

Kwa kweli, mitandao ya kijamii ni mahiri katika kutumia akili zetu." Tuna neva zinazoitikia hisia za raha—kufanya ngono, dawa za kulevya, kamari—na hujirudia tena na tena.

Mitandao ya kijamii, haswa, huwa na kitu kipya cha kutoa: picha, video, ujumbe. Ndiyo sababu huwa na uwezo wa kusababisha uraibu.

Kwa upande wa wazee, mtafiti Renata Maria Santos anaelezea kuwa maendeleo haya ya ulimwengu wa digitali yamesababisha hali inayoitwa hebephrenia, mkanganyiko wa kiakili ambao kwa kundi hilo husababisha "tabia kama za vijana wanaopevuka."

"Nimeona ongezeko la uhitaji wa uthibitishaji wa rika, msukumo wa kufanya manunuzi mtandaoni usio wa lazima, na utafutaji wa masuala yahusuyo urembo," Santos anasema.

Unaweza pia kusoma

"Kinadharia, hizi ni tabia ambazo wangekuwa tayari wamezipoteza katika umri wao, lakini zimerudi kutokana na mitandao. Wazee kwa hiyo wako katika hali sawa na ile ya vijana. Wanataka kujisikia wanahusiana na ulimwengu."

Wanasaikolojia BBC News Brasil walizungumza wakiangazia baadhi ya dalili ambazo wanafamilia wanaweza kuona wanapotumia simu zao;

  • Kutengwa na jamii, hata mbele ya watu;
  • kutokuwa na uwezo wa kufanya shughuli za kila siku na za nyumbani.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa saikolojia Anna Lucia Spear King muasisi wa Delete Institute inayohamasisha matumizi bora ya teknolojia,nomophobia hutokea.

Kwa kawaida hutokea ili "kuashiria hali ya wasiwasi, huzuni au hofu.

"Unapotambua tatizo, unapaswa kutibu ugonjwa uliosababisha uraibu kimsingi," anasema Spear King, ambaye anatafiti uraibu wa kidijitali na ni profesa katika Taasisi ya Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Rio de Janeiro (UFRJ).

Zaidi ya hayo, wataalam wanashauri familia zisalie karibu na watu wazima waliozeeka na kuwatia moyo washiriki katika shughuli za nje ya nyumbani.

Maria Aparecida Silva, aliyestaafu, anasema aliweza kujisikia "huru" baada ya kuachana na simu yake alipoanza kufanya mafunzo ya karate katika vituo vya wazee, kama vile Chama cha Brazil cha Msaada (Abrati), ambacho hutoa masomo huko São Paulo.

"Niliacha kutembea na vitu hivyo kila wakati," Aparecida alisema.

"Leo sihitaji, naacha kwenye chumba kingine na nikiwa nimeizima.

"Nikimnyang'anya simu yangu, anakuwa mkali"

Uhusiano kwa baadhi ya wazee wenye simu za mkononi pia una kipengele kingine: changamoto ya akili, ambayo huathiri karibu 8.5% ya wakazi wa Brazil wenye umri wa miaka 60 na zaidi.

Katika nyumba ya muuguzi Wany Passos huko Petrolina (PE), familia inawafuata madaktari ili kujaribu kuelewa tabia ya mama yao mwenye umri wa miaka 79, ambaye haachi simu yake ya mkononi.

"Aligunduliwa na ugonjwa wa Alzheimer's mapema, lakini sidhani ni hivyo tu. Amekuwa mraibu sana," Wany alisema.

Anasema, mama yake alipitia vipindi tofauti baada ya kupata simu ya mkononi yenye uwezo wa kuingia mtandaoni.

Kwanza, alianza kujitenga na wanafamilia ili aweze kutumia simu yake muda wote. Kisha, akaanza kutazama video kwenye programu ya Kwai siku nzima na kuamini kila kitu alichokiona - ambacho kilimuathiri Wany anasema, kuwa na msimamo mkali wa kisiasa.

Hatimaye, alianza kuhoji kila kitu kati ya ukweli na uhalisia, akiunda marafiki wa kiume na kushirikishana maudhui kana kwamba ni simu ya moja kwa moja.

"Nilijaribu kumpokonya simu yangu, ili kukata mtandao, lakini mara moja anakuwa mkali. Wakati mwingine mimi huamka alfajiri na kugundua kwamba amekuwa akitazama video kwenye mtandao wa Kwai usiku kucha," Wany anasema.

Familia ya Ester huko São Paulo ilipitia hali kama hiyo. Wakikabiliwa na uraibu iliokumba binti zao kutokana na matumizi ya simu za rununu, madaktari walibaini changamoto ya kiakili kwa mama yao.#

"Lakini nadhani kupoteza uwezo wa kutambua unaweza kuwa unahusiana na uraibu wa kutumia simu ya mkononi, kwa sababu yeye ni mwerevu, anazungumza kawaida," Ester anaelezea.

"Lakini anachohitaji kufanya ni kuwa na simu mkononi na tangu hapo alibadilika.Mama yake pia alifikiria juu ya wapenzi aliokumbana nao mtandaoni.

"Nilipompa simu, nilidhani ingechukua na kuvuruga akili yake, lakini kinyume chake kilifanyika. Muda mwingi alikuwa anatumia tu simu yake ya mkononi," anaelezea mlezi huyu kutoka São Paulo.

Mtafiti Renata Maria Santos anaamini kwamba mchanganyiko wa matatizo yanayotokana na simu za mkononi huleta hatari, ingawa hajapata tafiti zinazoafiki hili moja kwa moja.

Santos anaelezea kuwa moja ya dalili za kwanza za magonjwa haya ni hasira na kufuatilia Zaidi masuala ya ngono au ujinsia.

"wakiwa na simu ya mkononi, wanaweza kuacha uchokozi wao."

Anasema pia kwamba utafiti unaonyesha kwamba wakati simu ya mkononi iko umbali wa mita moja, mtu ana uwezo wa hadi 10% ya utambuzi ikilinganishwa na akiwa mbali na simu.

Ni kana kwamba akili inafanya kazi kidogo, kwani kila kitu unachohitaji kinaweza kufikiwa.

Katika wazee ambao wanapoteza uwezo wao wa utambuzi, umakini na kumbukumbu simu ya rununu inaweza kuwa chanzo cha tatizo, anaelezea mtafiti.

Wazee walio na dalili za changamoto ya akili pia ndio walio hatarini zaidi, kwa sababu hawaelewi kila kitu kinachotokea kwenye mitandao ya kijamii, anaonya mwanasaikolojia Cecilia Galetti.

Anaongeza kwamba wengi wa wagonjwa hawa wana kabiliwa na"ugumu zaidi kudhibiti mihemko."

Ndiyo sababu mwanasaikolojia anapendekeza kwanza kuwaelewesha wazee kuhusu masuala ya mtandao, kwa mfano kwa kuwafundisha jinsi ya kutumia smartphone.

Inaweza kuonekana tofauti, lakini hivi ndivyo watumiaji hawa wanavyoweza kutumia zana hizi "kwa njia salama na ya kimaadili," anahitimisha mwanasaikolojia.

Unaweza pia kusoma

Imetafsiriwa na Martha Saranga