Je, Hawa ndiye mwanamke wa kwanza kutokea ulimwenguni kama Biblia inavyosema lakini Je sayansi ya inasema nini?

DNA

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa mujibu wa Biblia, Hawa au Eva alikuwa mwanamke wa kwanza katika historia ambapo kuwa pamoja kwake na Adamu, walitokeza wanadamu wote. Sayansi, kwa upande wake, imechukua jina hilohilo kuelezea kwa angalau miongo minne jambo linalotokea katika chembe za urithi ambazo tunabeba ndani ya seli zetu zote. Kinyume na simulizi ya Kibiblia, hata hivyo, Hawa ama Eva wa "kisayansi" (au Hawa wa mitochondrial, kuwa sahihi zaidi) ndiye bibi au unaweza sema babu kwa maana ya Ancestor wa hivi karibuni zaidi wa wanadamu wote; Hebu tukumbuke neno "karibuni zaidi", kwani ni muhimu kuelewa maana yake hasa. Kutokana na kile kinachojulikana hadi sasa, mwanamke huyu angeishi miaka 150,000 au 200,000 iliyopita katika eneo tunalolijua leo kama Zimbabwe na Botswana, kusini mwa Afrika. Inafaa kusema kwamba hakuwa mwanamke wa kwanza katika historia,na hata hakua pekee katika enzi yake. Lakini, kwa sababu ya mambo kadhaa, kipande kidogo cha vinasaba ama DNA yake huonekana katika kila kizazi cha wanadamu baada ya hapo, kulingana na utafiti uliochapishwa hadi sasa. Ili kuelewa simulizi hii, ni muhimu kuchukua hatua nyuma na kujifunza maelezo ya muundo wa kipekee sana katika mwili wetu: Mitochondria

DNA

Chanzo cha picha, Getty Images

Seli zetu zote zina muundo unaoitwa mitochondria.

"Mitochondria ni chombo kinachozalisha nishati," anafupisha mwanabiolojia Gabriela Cybis, profesa katika Idara ya Takwimu ya Chuo Kikuu Shirikishi cha Rio Grande do Sul (UFRGS).

Kwa maneno mengine, muundo huu una jukumu la kubadilisha sukari katika chakula kuwa molekuli za ATP, aina ya nishati ambayo mwili wetu hutumia kufanya kazi.

Na jenereta hizi ndogo zina sifa ama tabia ya kipekee: hubeba DNA zake zenyewe.

Genome, inayojumuisha jeni 20,000 tofauti na ina jukumu la kuamua sehemu kubwa ya sifa zetu na mwelekeo wa ugonjwa, imehifadhiwa kwenye kiini cha seli.

Mitochondria, ambayo iko ndani ya seli lakini nje ya kiini, ina jeni 37 zake zenyewe. Wanasayansi wanazijua kama DNA ya mitochondrial (au mtDNA).

Hapa ndipo simulizi inakuwa ya udadisi zaidi. Tunarithi mtDNA kutoka kwa mama zetu pekee.

Wakati wa uzazi, wakati yai na manii hukutana, mitochondria ya gamete ya kiume hupotea katika mchakato wa kuunganishwa kati ya seli mbili.

Hivyo basi ni kwamba kiinitete daima huundwa tu na mitochondria ya asili ya uzazi.

Kwa hivyo habari hii inaturuhusu kubaini uwepo wa ukoo usiokatizwa unaoundwa na wanawake pekee kwa vizazi kadhaa na maelfu ya miaka, uliounganishwa kwa usahihi na mtDNA.

Baada ya yote, kila binti ana mama.Lakini sio mama wote wana binti: ikiwa mwanamke ana watot tu (au hazai watoto), DNA yake ya mitochondrial haitaendelezwa kwa wajukuu wa baadaye.

"Kwa hivyo, katika suala la maumbile, inawezekana kufuatilia nani ni mama wa mama, wa mama, wa mama ... Na kadhalika," anasema Cybis.

Mti uliojaa matawi

Maendeleo katika ujuzi wa jenetiki na teknolojia ya kupanga na kuchakata jeni yameruhusu wanasayansi kutengeneza upya asili ya mtDNA. Mwanabiolojia Bibiana Fam, kutoka Maabara ya Tiba ya Genomic ya Hospitali ya de Clínicas de Porto Alegre, anaeleza kwamba kazi za kwanza kuhusu babu zetu wa hivi majuzi zaidi zilichapishwa katika miaka ya 1980. Kulingana na yeye, ripoti za kwanza zinazotumia neno "Hawa au Eve wa mitochondrial" zilionekana: neno hilo bado linatumika leo, licha ya kwenda tofauti na dhana ya kibiblia.

DNA

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ingawa kuna mahali wanakubaliana kati ya wataalam juu ya dhana ya Eva au Hawa wa mitochondrial; wakati ambao angeishi bado ni mada ya mjadala : makadirio ya kuaminika zaidi bado yanaonyesha tofauti ya zaidi ya miaka elfu 50. Matumizi yenyewe ya jina "Eva" katika muktadha huu, kwa namna fulani, ni ukosoaji mwingine uliofanywa na watafiti wengine. Kulingana na wao, inaleta mgongano kati ya dhana za kisayansi na simulizi za kibiblia, ambayo huleta mkanganyiko linapokuja suala la kuwasilisha jambo hilo kwa hadhira pana. Mada hii imekuzwa tangu kazi za kwanza katika eneo hili zilichapishwa mwishoni mwa miaka ya 1980: nakala katika jarida maalum la Sayansi inaangazia "msululu wa utata" kuhusu tafiti katika jambo hili. Mtaalamu wa vinasaba Tábita Hünemeier, kutoka Idara ya Jenetiki na Baiolojia ya Mageuzi ya Taasisi ya Sayansi ya Biolojia ya Chuo Kikuu cha São Paulo (USP), anasema kwamba matumizi ya jina la kwanza katika muktadha huu ilikuwa kama aina ya "leseni ya ushairi" . “Lakini wazo hilo linategemea kabisa uthibitisho wa kisayansi na halihusiani na Biblia,” asema. Wanasayansi wamejifunza kukadiria inachukua muda gani kwa mabadiliko ya jeni kuonekana kwenye vizazi. "Hii ilituruhusu kuelewa vizuri zaidi ni muda gani ilichukua kwa mabadiliko yaliyoonekana katika DNA ya mitochondrial kutokea," asema Fam. Kutokana na hili, iliwezekana kuhesabu kwamba Eve angeishi kusini mwa Afrika kati ya miaka 150,000 na 200,000 iliyopita. Kuanzia wakati huo, mtDNA ya vizazi vilivyofuata ilibadilika polepole. Pamoja na hayo, matokeo (kisayansi) yaliibuka.

Migogoro na mikanganyiko

Hebu tuwe wazi: Eva hakuwa mwanamke wa kwanza katika historia. Kulikuwa na vizazi vingine kadhaa kabla yake, kama vile mama yake, nyanya na babu, na kupitia mamilioni na mamilioni ya miaka ya mageuzi, mababu wa spishi zingine ambazo Homo sapiens iliibuka. Na, kama ilivyoelezwa hapo juu, Eva hakuwa pekee wa wakati wake, pia. Uwezekano mkubwa zaidi, kulikuwa na wanawake wengine wanaoishi katika sehemu moja. Hii ilitokea kwa sababu, katika vizazi fulani, wanawake walio na mtDNA tofauti hawakuzaa watoto, au walikuwa na watoto wa kiume tu, ambao uliingilia "muendelezo" uliofuata wa nyenzo zao za urithi.