Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Je, Harry Kane kujiunga na Arsenal?

Muda wa kusoma: Dakika 2

Mshambulizi wa Uingereza Harry Kane, 31, amekataa kuzungumza kuhusu ripoti kwamba anaweza kuhamia Arsenal mwaka ujao, kwa sababu ya kipengele cha kutolewa katika kandarasi yake ya Bayern Munich. (Mirror)

Chelsea wanatayarisha dau la euro 50m (£41.6m) kumnunua mshambuliaji wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo, 25. (Fichajes - Spanish)

Liverpool wanadaiwa kumfuatilia kwa karibu beki wa Feyenoord na Slovakia David Hancko, 27, kama mchezaji wanayemlenga msimu huu. (Caughtoffside)

Kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 27, ameambiwa Barcelona haitamzuia kuhamia Liverpool msimu ujao. (El Nacional - Spanish)

Mshambuliaji wa Uhispania Ansu Fati, 22, hafikirii ofa kutoka kwa vilabu vya Uturuki na badala yake anaangazia kikamilifu Barcelona. (Fabrizio Romano)

Real Madrid wanataka kuwasajili mabeki wawili wa kati msimu ujao, huku beki wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 23, akiwa miongoni mwa majina kwenye orodha ya klabu hiyo ya Uhispania. (Relevo - in Spanish)

Chelsea ni moja ya klabu tano zinazowania kumsajili kipa wa Liverpool na Jamhuri ya Ireland, 26, Caoimhin Kelleher msimu ujao. (TBR Football)

Arsenal, Manchester United na Liverpool zinaonyesha nia ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Eintracht Frankfurt na Uswidi Hugo Larsson, 20. (Caughtoffside)

Chelsea wanaamini wanaweza kufanya dili kwa ajili ya mlinzi wa Sporting Ousmane Diomande msimu wa joto - chini ya kipengele cha ukubwa wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 21. (TeamTalk),

Imetafsiriwa na Seif Abdalla