Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Man United yaongeza kasi ya kumsajili mshambuliaji wa Mali El Bilal Traore
Man United imeongeza kasi ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Mali El Bilal Toure, 23, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Stuttgart kutoka Atalanta. (TeamTalks),
Tottenham Hotspur wanaonekana kuwa mbele ya Wolves katika mbio za kuwania saini ya beki wa Lens na Austria Kevin Danso, 26. (Talksport), wa nje.
Spurs pia wameonyesha nia ya kumnunua mlinzi wa Chelsea Mfaransa Axel Disasi 26, iwapo uhamisho wa mlinzi wa Uingereza Fikayo Tomori, 27, kutoka AC Milan utashindwa. (Telegraph), nje
Uhamisho wa Bayern Munich kwa mshambuliaji wa Chelsea Mfaransa Christopher Nkunku, 27, hautafanyika katika dirisha hili la usajili lakini unaweza kufufuliwa msimu wa joto. (Christian Falk),
Southampton wana nia ya kutaka kumsajili beki wa Ivory Coast Loubadhe Abakar Sylla, 22, kwa mkopo kutoka Strasbourg. (Fabrizio Romano)
Crystal Palace wamewasiliana na Chelsea kuhusu kumsajili beki wa Uingereza Ben Chilwell, 28, kwa mkopo. (Athletic - subscsription Required)
Pendekezo la beki wa Manchester United Mholanzi Tyrell Malacia kuhamishwa kwa mkopo kwenda Benfica limeporomoka lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 bado anaweza kuondoka Old Trafford katika dirisha la usajili. (Fabrizio Romano)
Burnley wanakaribia kumsajili winga Mwingereza Marcus Edwards mwenye umri wa miaka 26 kutoka Sporting. (Sportsport)
Beki wa Newcastle Muingereza Lloyd Kelly, 26, anakaribia kuhamia Juventus inayoshiriki Serie A. (Chronicles)
AC Milan wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Feyenoord na Mexico Santiago Gimenez, 23. (Goal)
West Ham wametoa ofa yenye thamani ya hadi £30m kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 18 Eli Junior Kroupi, ambaye kwa sasa yuko na Lorient. (Football Insider)
Middlesbrough wako kwenye mazungumzo ya kumsajili winga wa Aston Villa Muingereza Samuel Iling-Junior, 21, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Bologna. (Mail)
Napoli wanatazamia kukamilisha uhamisho wa mkopo kwa winga wa Ufaransa Allan Saint-Maximin, 27, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Fenerbahce kutoka Al-Ahli ya Saudia. (Calciomercato)
Marseille wanataka kumnunua kwa mkopo beki wa Chelsea Muargentina Aaron Anselmino, 19. (Footmercato - In French).
Imetafsiriwa na kuchapishwa na Seif Abdalla