Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Kiungo wa Liverpool Luis Diaz anataka kujiunga na Barcelona

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Luis Diaz
Muda wa kusoma: Dakika 3

Mshambulizi wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28 kutoka Colombia Luis Diaz anatumai Barcelona itamnunua mwishoni mwa msimu huu. (Mundo Deportivo – In Spanish)

Nottingham Forest itafufua nia yao ya kumnunua Douglas Luiz wa Juventus msimu huu wa joto, baada ya kushindwa katika ombi la Januari la kumnunua kiungo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 26. (Tuttosport – In Itali).

Everton itamfanya beki wa kati wa Genoa, 22, Mbelgiji, Koni de Winter, kuwa shabaha ya juu ikiwa beki wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 22, ataondoka msimu huu wa joto. (TeamTalk}

Bournemouth wanatumai kubadilisha mlinda lango wa Uhispania Kepa Arrizabalaga kwa mkopo kutoka Chelsea kuwa mkataba wa kudumu msimu huu wa joto. (Telegraph – Subscription Required)

Pia unaweza kusoma
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kepa Arrizabalaga

Manchester United inamfuatilia kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Ujerumani Felix Nmecha, 24. (Florian Plettenberg)

Paris St-Germain na Real Madrid wanafuatilia hali ya Ibrahima Konate katika klabu ya Liverpool, huku beki huyo wa Ufaransa, 25, akiwa bado hajakubali kuongezwa kwa kandarasi yake ambayo inaisha mwaka ujao. (Football Insider)

Sevilla wanapanga kumnunua kiungo wa kati wa Aston Villa na Uholanzi Lamare Bogarde mwenye umri wa miaka 21 msimu wa joto. (Estadio Deportivo – In Spanish)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lamare Borgade

Bayer Leverkusen, Parma na Wolfsburg wameungana na Liverpool, Manchester City na Brighton katika mbio za kumnunua kiungo wa kati wa Independiente del Valle mwenye umri wa miaka 15 kutoka Ecuador Johan Martinez. (TeamTalks)

Lyon wako tayari kumuuza Rayan Cherki mwishoni mwa msimu huu, huku Liverpool, Bayern Munich na Borussia Dortmund zikiwa miongoni mwa vilabu vinavyomhitaji winga huyo wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21, 21. (Sun)

Kampuni inayoongozwa na mshambuliaji wa zamani wa Nigeria, Everton, West Bromwich Albion na Sunderland Victor Anichebe inakaribia kuinunua klabu ya Ligi ya Taifa ya Gateshead. (Chronicle)

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla