Nchi tano, milo mitano - jinsi ya kukabiliana na gharama za chakula

Ben Gray

Chanzo cha picha, Ben Gray

Maelezo ya picha, Moja ya milo katika shule ya Donna Martin – ukiwa na maharage badala ya njugu

Chakula kinaendelea kuwa cha gharama ya juu, na wakati mwingine huwa haba kabisa. Kila mahali watu wanalazimika kuzoea hali mpya, na hii wakati mwingine ina maanisha kuwa wabadili kile wanachokila.

Duka la jumla la usiku la Walmart nchini Marekani

Ni alfajiri saa kumi asubuhi na tayari hali ya hewa ni ya joto kali katika msimu wa majira ya joto huko Georgia wakati Donna Martin anawasili kazini.

Siku nyingine inapoingia inamaanisha anaanza mapambano ya kuhakikisha watoto wanakula katika shule yake ya wilaya.

Bi Martin ni Mkurugenzi wa huduma ya chakula mwenye jukumu la kuwalisha wanafunzi, ambao wote wako chini ya mipango ya chakula cha bure shuleni. "Tuna maduka madogo mawili tu katika eneo yetu lenye watu 22,000," anasema. "kusema kweli ni jangwa la chakula ."

Lakini katika mwaka uliopita amekuwa akihangaika kupata kile anachokihitaji.

Donna anaendesha mradi wa chakula wa majira ya baridi kwa ajili ya watoto, 3,000

Chanzo cha picha, Ben Gray

Maelezo ya picha, Donna anaendesha mradi wa chakula wa majira ya baridi kwa ajili ya watoto, 3,000

Mfumuko wa bei za chakula kwa mwaka ulifika hadi 10.9% katika mwezi wa Julai, kikiwa ni kiwango cha juu zaidi cha mfumuko wa bei tangu mwaka 1979. Huku bei zikipanda baadhi ya wasamabazaji wa chakula kama vile wasambazaji wa Bi Martin hawana haja tena ya kulisha shule.

Mpango wa lishe kwa shule za shirikisho nchini Marekani unadhibitiwa vikali. Hiyo ina maanisha kuwa bidhaa kama vile chenga za mikate zinazopakwa kwenye kuku wa kukaangwa lazima zisiwe za ngano ya kukobolewa, lazima ziwe na kiwango cha chini cha sukari na chumvi. Kwahiyo Bi Martin analazimika kutafuta aina zote, kuanzia nafaka hadi chenga aina mbali mbali au yogati.

Anatambua kuwa wanaomuuzia bidhaa hizi pia wanahangaika. Ukosefu wa wafanyakazi wa muda mrefu inamaanisha kwamba hawawezi kuwapata madereva na gharama za mafuta zimeongezeka kwa 60% kwa mwaka.

  • Garama ya chakula kwa mwaka nchini Marekani iliongezeka nchini kwa 10.9% mwezi Julai
  • Wamarekani hutumia 7.1% ya pato lai kwa chakula(USDA 2021)

Tunda la fenesi limekua mwokozi nchini Sri Lanka

Chamil Rupasinghe

Chanzo cha picha, Chamil Rupasinghe

Kuna uhaba wa kila kitu – madawa, mafuta na chakula. Hata watu wenye kazi nzuri wanahangaika kununua bidhaa za msingi.

"Sasa watu wana wasi wasi kuhusu hali yao ya baadaye," Bi Paranathala anasema "Twanahofia hakutakuwa na chakula cha kula."

Katika Jordan, serikali ilipendekeza viwango vya bei ya kuku na bidhaa nyingine.

Wafugaji wa kuku walikubaliana na bei zilizowekwa hadi kufikia mwishoni mwa Ramadan. Lakini mwanzoni mwa mwezi Mei, walilazimika kupandisha bei, na kusababisha mfumuko wa juu.

  • Mfumuko wa bei ya chakula nchini Sri Lanka kwa mwaka ulifikia 75.8% mwezi Juni
  • Wasri Lanka hutumia 29.6% ya pato lao kwa chakula
Chamil Rupasinghe

Chanzo cha picha, Chamil Rupasinghe

Alianza kutengeneza supu ya binzari na nazi pamoja na matunda, badala ya mboga ambazo zingekuwa sasa ghali kununua, au nyama. Fenesi pia sasa inaonekana katika kottu – chakula maarufu cha kukaangwa kinachouzwa kama chakula cha mtaani. Na baadhi ya watu wanasaga mbegu kutengeneza mkate wa unga na keki.

Migahawa nchini inaelekea 'kutoweka'

Tom Saater

Chanzo cha picha, Tom Saater

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa kawaida Emmanuel Onuorah hapendi siasa, ni muokaji, na anataka tu kuuza mikate.

Lakini hivi karibuni nchini Nigeria, kazi yake imekuwa ngumu.

"Katika mwaka uliopita, unga wa ngano umepanda kwa zaidi ya 200%, sukari imepanda kwa karibu 150%, mayai ambayo tunatumia yamepanda kwa takriban 120%," anasema.

"Tunaendesha biashara kwa hasara," anasema. Amelazimika kuwafuta kazi wafanyakazi wake 305 kati ya 350. "Watalisha vipi familia zao?"

Kama rais wa chama cha waokaji wa mikate nchini Nigeria -Breadmakers Association of Nigeria, anaongoza vuguvugu. Mwezi Julai, aliwakusanya waokaji karibu nusu milioni kufunga milango yao kwa siku nne katika mgomo wa "kusitisha utengenezaji "wa mikate.

  • Mfumuko wa bei ya chakula kwa mwaka nchini Nigeria ulifikia 22% mwezi Julai
  • Wanigeria kutumia 59.1% ya pato lao kwa chakula

Nchi pia ina uhaba wa umeme, kwahiyo biashara nyingi hutumia jenereta zinazotumia mafuta. Lakini ya gharama ya dizeli imepanda kwa 30%.

Licha ya kupanda kwa gharama Bw Onuorah anasema anaweza tu kupandisha bei yake kwa 10-12%. Wateja wake hawawezi kulipa zaidi ya pesa gharama hiyo.

tambi

"Wanigeria wanakuwa masikini, biashara zimefungwa na mishahara imebaki pale pale huwezi kuwaongezea bei zaidi," anasema.

Kwa wastani, Wanigeria hutumia takriban 60% ya pato lao kwa chakula. Kinyume chake nchini Marekani kiwango hicho ni karibu na 7%.

Chungu cha jamii huwalisha watu 75 nchini Peru

Guadalupe Pardo

Chanzo cha picha, Guadalupe Pardo

Kutoka Lima, Justina Flores anajaribu kufikiria ni nini atakachopika leo

Ni tatizo linaloendelea kuwa gumu zaidi kila siku.

Wakati wa janga na covid aliungana na majirani zake 60 kukusanya chakula chochote walichonacho kwa ajili ya kupika. Wengi wa wakazi wa San Juan de Miraflores na wapishi wa nyumbanii, wafanyakazi wa nyumbani, walezi wa watoto na watunza bustani – Lakini sawa na Bi Flores, wengi walipoteza kazi wakati wa la covid.Famialia zilikuwa na njaa.

Miaka miwili baadaye wanawalisha watu 75, mara tatu kwa wiki

  • Mfumuko wa bei ya chakula kwa mwaka nchini Peru ulifikia 11.59% katika mwezi Julai
  • Waperu hutumia 26.6% ya pato kwa chakula

Mgomo wa kuku katika Jordan

Ahmad Jaber

Chanzo cha picha, Ahmad Jaber

Maelezo ya picha,

Tarehe 22 Mei ujumbe wa kiarabu uliotumwa kwenye Twitter na mtu asiyejulikana ya kiarabu iliwataka watu watume picha za bidhaa za kuku na alama ya leri -hashtag #Boycott_Greedy_Chicken_Companies.

Siku chache baadaye katika Jordan, Salam Nasralla alikuwa akirudi nyumbani kutoka kwenye duka wakati alipoona kampeni hiyo imeenea.

"Tuliisikia kila mahali, marafiki zetu wengi na familia walikuwa wanaizungumzia. Ilikuwa kote kwenye mitandao ya kijamii na TV," anasema Bi Nasralla.

 Aligundua tu kwamba gharama ilipanda kutokana na bidhaa alizonunua

  • Mfumuko wa bei ya chakula katika Jordan kwa mwaka ilifikia 4.1% katika mwezi Juni
  • Wajordan hutumia 26.9% ya pato lao kwa chakula

 Sababu mbali mbali duniani zilisababisha kupanda juu kwa bei ya mafuta na nafaka – inajijenga baada ya homa ya mafua, ukame Amerika Kusini, na vita katika Ukraine

Familia yaNasralla iliepuka kuku kwa siku 10

Chanzo cha picha, Ahmad Jaber

Maelezo ya picha, Familia ya Nasralla iliepuka kuku kwa siku 10

Nchini Jordan serikali ilipendekeza viwango vya bei ya kuku lakini pia bei za vidhaa nyingine.

Wakulima walikubali bei hadi mwisho wa mwezi wa ramadhan. Lakini mapema mwezi Mei, walilazimika kupandisha bei. Halafu ghadhabu ikaibuka kwenye mitandao ya kijamii huku watu wakipinga bei.

"Kuku iliwakilisha kutoridhika kwa mfumuko wa juu wa bei za vitu vyote ," anasema

Bi Nasralla alishukuru kuona maandamano yalikuwa na athari lakini anahofia kuwa hayakutatua kikamilifu tatizo.

"Bahati mbaya ni wakulima wadogo na wauzaji wa kuku ambao wanaumia zaidi na sio wafanya biashara wakubwa ambao wanapandisha bei za kila kitu anachohitaji mkulima."