Fahamu shamba linalobadilisha nzi kuwa chakula cha wanyama wa nyumbani - pengine hata kwa binadamu

Wadudu

Chanzo cha picha, Tommy Trenchard

Kuna mahitaji yaliyoongezeka ya wadudu kama chanzo cha protini katika chakula cha wanyama wa nyumbani.

Mpiga picha Tommy Trenchard alitembelea shamba la nzi huko Cape Town, Afrika Kusini, ambako anatarajia kufaidika.

Shamba hilo lilianzishwa mnamo mwaka 2018 kwenye eneo la viwandani pembezoni mwa jiji.

Kila mwezi linazalisha zaidi ya tani 10 za malisho yenye ubora wa protini, nyingi zikiwa zimekusudiwa kusafirishwa nje ya nchi.

Wadudu

Chanzo cha picha, Tommy Trenchard

"Una upungufu wa chakula, na watu ambao wanakufa njaa, na wakati huo huo, una shida ya taka. Kwa hivyo nilianza kuangalia ni jinsi gani tunaweza kupata suluhu," alisema mwanzilishi wa kampuni Dean Smorenberg, akitafakari kile kilichomchochea kuingia kwenye ukulima huu.

Yeye ni mshauri wa zamani ambaye alianza kilimo cha nzi katika bafuni yake mnamo mwaka 2016 kabla ya kujitosa kabisa kwenye biashara hiyo na kuanza kuifanya muda wake wote.

Mfano huo wa ufugaji ni wa kuvutia kwa watumiaji wanaofahamu kaboni: mabuu ya nzi hula chakula cha taka - kwa hali hii hutumiwa sana katika nafaka kutoka kwa kiwanda cha karibu - na kuibadilisha kuwa protini inayouzwa na kutoa bidhaa ya mbolea.

Wadudu wakimiminwa kwenye ukanda wa kusafirishia

Chanzo cha picha, Tommy Trenchard

Mchakato huo hutumia maji na kipande kidogo cha ardhi kuliko aina zingine za uzalishaji wa protini na pia kiwango cha kaboni kinachtumika ni cha chini.

Utafiti wa 2020 uliofanywa na watafiti nchini Uingereza na Ujerumani ulibaini kuwa soko la kimataifa la chakula cha wanyama wanaofugwa nyumbani huchangia kiwango kikubwa cha kaboni dioksidi kwenye anga kama ilivyo kwa uzalishaji jumla wa Ufilipino au Msumbiji.

Badala ya kutafuta kukabiliana moja kwa moja na sekta kubwa ya soya au samaki, ambayo kwa sasa ndio inayotoa protini nyingi kwa bei rahisi ulimwenguni, shamba la Maltento linatafuta kutoa bidhaa ambazo zinakuwa mbadala wa chakula cha wanyama wa nyumbani au lishe bora.

Wadudu wanaelezwa kuwa na thamani zaidi ya kuwa tu protini

Chanzo cha picha, Tommy Trenchard

"Wadudu wana thamani zaidi ya kuwa tu protini," anasema Bw. Smorenberg, akionyesha kwamba kile kinachojulikana kama protiniz a kuuwa wadudu katika mabuu ya nzi husaidia kuboresha afya ya utumbo.

"Na hakuna mazao mengine duniani ambayo yanaweza kukupa mavuno 52 kwa mwaka kufuatana."

Shamba la Maltento, ambalo linapanuka kwa kasi, limegawanywa katika sehemu kadhaa kulingana na hatua za mzunguko wa maisha ya wadudu.

wadudu kwenye mtego

Chanzo cha picha, Tommy Trenchard

Mabuu hupitia mchakato na kubadilika kwenye chumba chenye giza katika ghorofa ya chini kabla ya kuhamishiwa hadi ghorofa ya juu eneo lililotengwa la kuzaliana, ambapo nzi wazee chini ya miale ya jua hutaga mayai kwenye mtego wa chuma.

"Kimsingi hiki ni chumba muhimu katika ufugaji huu, ikiwa ungependa," anasema Dominic Malan, ambaye ana jukumu la kuhakikisha ongezeko la idadi ya wateja wanaotarajiwa.

"Joto na unyevu unyevu ni vitu muhimu zaidi kuhakikisha vinastawi."

"Mlango unaofuata, kuna kitalu ambapo mayai huangua na "vichanga kupatikana" ambao husambazwa kwenye vyombo vidogo vya plastiki vilivyojaa malisho. Vinavyoanguliwa, huwekwa ndani ya vyumba vyenye joto linalodhibitiwa na kuanza kukua kwa ajabu mno.

"Tumeweka gramu 0.5 ya hawa wadogo," anasema Bw. Malan. "Na baada ya siku sita wamekua [kwa pamoja] hadi kufikia uzito wa gramu 4."

Wadudu

Chanzo cha picha, Tommy Trenchard

Inzi wanapokua kabisa, makontena hutiwa ndani ya mashine ambayo huwatenganisha na "mavi"- bora kwa mbolea - ambayo itauzwa kama aina ya mbolea ya kikaboni.

Bwana Malan anasema kumekuwa na hamu kubwa inayozidi kuongezeka katika bidhaa hii kutokana na sekta ya dawa zinazotokana na bangi.

Kutoka wakati huu, nzi wanaweza kwenda moja ya njia kadhaa.

Wengi hukaushwa na kusafirishwa nje ya nchi wakiwa wazima kama chakula cha kuku huko Marekani.

Wengine husagwa na kuwa unga unga ambao hutumiwa na kampuni ya Norway kutengeneza chakula cha mbwa.

Wengine bado wanatengezwa kwa mfano wa kukamuliwa kwa ajili ya mafuta au kutiwa maji maji.

Buu

Chanzo cha picha, Tommy Trenchard

Pembe ya chumba hicho kuna safu ya mifuko mikubwa mieupe iliyojaa hadi pomoni yenye mabuu yaliyokaushwa.

Kwa mwanadamu, wadudu huonja mchanga, na ladha fulani hivi chachu inayotokana na nafaka zilizotumiwa ambazo hulishwa.

Kwa paka na mbwa, anasema Bwana Malan, huwezi kuzuia.

Kulingana na RaboResearch, shirika la utafiti wa biashara ya kilimo la Uholanzi, uzalishaji wa protini ya wadudu kwa chakula cha wanyama wa nyumbani kote duniani, inaweza kufikia tani nusu milioni ifikapo mwisho wa miaka kumi, kutoka tani 10,000 hivi leo.

Na ni sekta ambayo inakua kwa haraka sana.

Kwenye maabara katika kitongoji cha Woodstock, jiji jirani, maoni yanaonesha kuwa wanasayansi wa kilimo wanatafuta kila mara kuboresha ladha na faida za kiafya za bidhaa zinazotona na mabuu.

Hii inategemea lishe inayopewa mabuu, hali ambayo huchangia kukua kwao na pia jinsi bidhaa ya mwisho inavyotengenezwa.

Mchanganyiko ukimiminwa

Chanzo cha picha, Tommy Trenchard

"Kwa kweli sana, " anasema Dk. Leah Bessa, mwanasayansi wa chakula na PhD katika kutumia mabuu ya nzi kama mbadala wa ulaji wa binadamu.

"Kuna utendaji mwingi bado haujatumika".

Bidhaa ya hivi karibuni Dkt. Bessa amekuwa akifanya kazi ni kitu kilichoundwa kuongezwa kwa vyakula vya wanyama wa nyumbani ili kuboresha ladha na faida zao za lishe.

Kabla ya kujiunga na kampuni ya Maltento, aligonga vichwa vya habari nchini Afrika Kusini baada ya kuzindua kampuni iliyouza aiskrimu inayotokana na wadudu.

Wadudu karibu na mwanga wa taa

Chanzo cha picha, Tommy Trenchard

Katika ripoti ya mwaka 2013, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa lilisema kula wadudu kunaweza kusaidia kukabiliana na upungufu wa chakula ulimwenguni.

Lakini licha ya wadudu kuwa vitafunio maarufu katika nchi nyingi, mataifa ya Magharibi yameonekana yanapinga wazo hilo.

Kwa sasa, Dkt. Bessa anaamini utumiaji mkubwa wa wadudu kunaweza kusalia zaidi kwa wanyama wa nyumbani.

"Hatujafika kabisa hapo, bado," anasema, akiongeza kuwa bado kichefuchefu ni kikwazo."

"Mbwa ni rahisi sana kuwalisha wadudu kuliko wanadamu wakati huu."

Picha zote ni kwa hisani ya Tommy Trenchard