Fahamu hatari ya kuiandaa kijeshi jamii ya Waisrael?

v

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Jeshi la Israel lilichukua msimamo mkubwa katika jamii, uliotikiswa baada ya shambulio la Oktoba 7.
Muda wa kusoma: Dakika 6

Tunaanza uchambuzi wa magazeti na gazeti la Times la Israel, ambao lilichapisha makala ya Shira Tamer ambayo alizungumzia juu ya "mapambano ya kijeshi " ya jamii nchini Israeli na udhibiti wa jeshi wa maisha nchini na kuonekana kwake wazi, kuanzia usajili wa kijeshi na hadi kuenea kwa alama za kijeshi kila mahali na katika shughuli zote za maisha ya kila siku, kupitia siasa, elimu, burudani, na vyombo vya habari.

"Watu katika jamii hii wanaweza wasione uwepo wa jeshi wazi," Shira alisema, "lakini kwa mtu kama mimi ambaye niliondoka nchini Marekani nikiwa na umri mdogo nimehisi kama mtu wa nje tangu nirejee katika nchi yngu ya kuzaliwa ni vigumu kupuuza hili. Namaanisha, katika nchi gani nyingine ya kidemokrasia unaweza kupata kwamba wananchi wangependelea kusikiliza kituo cha redio kinachoendeshwa na jeshi kusikiliza muziki na habari kinazotoa?.

Mwaka 2024, takwimu zilionyesha kuwa idadi ya wasikilizaji wa Redio Galgalat, inayoendeshwa na jeshi la Israeli, ilifikia milioni 1.3, kulingana na Wikipedia. Inatangaza taarifa za kila baada ya saa ili uweze kuendelea na vita na siasa kuwafanya wasikilizaji wasisahau kuhusu vita."

Alisema kuwa alama za kijeshi pia zimeenea katika ulimwengu wa siasa, na jamii husherehekea mafanikio ya kijeshi zaidi kuliko mafanikio mengine, na kanuni zilizowekwa na maisha ya kijeshi zimekuja ndizo zinazoamua kinachopaswa kuadhimishwa, nini kinapaswa kusahaulika, nini na nani anapaswa kuheshimiwa, na nani anapaswa kuombolezwa na jamii. Kila kitu katika Israeli kimekuwa ni cha kijeshi, kama askari ni sherehe na kuchukuliwa kama mashujaa, kuwa Muisraeli ina maana ya kuwa askari au angalau kutoa msaada endelevu, wa bila masharti kwa jeshi.

Lakini Shira Tamer anasema katika makala yake kwamba uvamizi wa Hamas wa Israel wa mnamo Oktoba 7, 2023, umeharibu sana picha ambayo imechorwa kwa miongo kadhaa ya jeshi la Israel kwa jamii. Raia wamekosa imani, tangu siku hiyo, wakati Waisraeli wapatao elfu moja walipouawa na raia 250 wa Israel na wa kigeni kushikiliwa mateka na Hamas - kwamba jeshi halikuwepo kuwasaidia wakati lilipohitajika.

"Kwangu, janga la Oktoba 7 sio tu hadithi ya kushindwa kwa serikali ya kijeshi," mwandishi alisema. "Ninaona kama ni kushindwa kwa jamii. Kushindwa kufikiria kwamba Israeli inaweza kuwepo nje ya mipaka ya kijeshi na vita. Hadi pale kushindwa huku kutakaposhughulikiwa, hali itabaki kama ilivyo—taifa lililoshindwa na ukweli wake wa nje, utambulisho wake, na chaguo lake."

Unaweza pia kusoma:

Kuchekelewa kwa ishara ya utoaji chanjo Gaza

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Israel na Hamas zamekubaliana kusitisha mapigano kwa ajili ya kuwachanja watoto wa Gaza dhidi ya polio

Israel na Hamas zamekubaliana kusitisha mapigano kwa ajili ya kuwachanja watoto wa Gaza dhidi ya polio

Chini ya kichwa hiki cha habari, gazeti la Saudi Arabia la Asharq Al-Awsat lilichapisha makala ya Amal Moussa, ambapo aligusia kwamba watoto na wanawake huko Gaza wamebeba na wanaendelea kubeba mzigo wa uharibifu uliosababishwa na idadi ya watu wa ukanda huo na vita.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mwandishi anakadiria kuwa theluthi moja ya waathiriwa wa vita hivyo ni watoto, akikosoa vikali kile ambacho Shirika la Afya Duniani lilitangaza siku mbili zilizopita, kwamba Israel na Hamas zilikubaliana "kusitisha mapigano kwa muda katika maeneo maalumu ya Gaza, ili kuruhusu watoto 640,000 kupewa chanjo dhidi ya polio."

Mwandishi aliuliza: "Je, mtu ambaye anaua maelfu ya watoto wasio na hatia anaweza kuelewa ratiba ya chanjo kwa watoto? Halafu inamaanisha nini kuruhusu watoto wapewe chanjo dhidi ya polio wakati wanaishi katika hali ambayo wanatishiwa kifo na kuwa yatima? Je, ombi kama hilo kutoka kwa mtekelezaji ni sahihi?" Alipendekeza kuwa utaratibu huo utakuwa sawa na kuwachanja watoto dhidi ya magonjwa ili wauawe wakati wakiwa na kinga ya polio.

Hatuamini kwamba haki ya afya kwa watoto katika Gaza ni kipaumbele au maslahi ya Israeli. Haki ya kuishi inakiukwa" alisema. Alisisitiza kuwa neno "mkataba" halifai kabisa kwa watoto, akidokeza kuwa ni muhimu kuwapa mazingira salama na kuwaepusha kuwa waathirika wa vita vinavyoendelea katika ukanda huo.

Pia amedokeza kuwa Israel "inalenga" mustakabali wa Palestina kwa kuwaua watoto, akielezea kile ambacho Israel ilikuwa ikifanya katika kuwaua kama "shambulizi dhidi ya idadi ya watu". Alilaani nia ya Israel kushirikiana na Hamas kuwachanja watoto dhidi ya polio, wakati "iliwashambulia watoto 13,000 wa Kipalestina chini ya mwaka mmoja."

Amal Musa aliendelea kusema kuwa "kulenga" watoto na kina mama kwa mashambulizi huko Gaza ni "kitendo cha utaratibu na kilichopangwa ili kuondoa moja ya nguvu za Palestina, ambayo ni kiwango cha uzazi.

Anasema kuwa srael inalenga kupunguza idadi ya watu kwa kuwalenga wanawake na watoto ili kupunguza idadi ya watu wa jamii, kwa kupunguza idadi ya watoto, na kisha vijana baada ya muda na hatimaye idadiya watu kwa ujumla.

Hatari ya mamlaka ya rais wa Marekani

f

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kamala Harris ameonyesha mafanikio makubwa tangu alipoteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Democratic kuwania urais wa Marekani.

Tukiendelea na gazeti la Uingereza la The Guardian, ambalo lilichapisha makala kuhusu uchaguzi wa rais wa Marekani wa 2024 na mwandishi Timothy Garton Ash, ambapo alijadili umuhimu wa uchaguzi huu wa Marekani mwaka huu.

Mwandishi anaamini kuwa uchaguzi wa rais wa Marekani una maslahi makubwa zaidi duniani, ambapo karibu nusu ya idadi ya watu walipiga kura mwaka huu katika uchaguzi wa kidemokrasia katika nchi nyingi. Garton Ash alifupisha umuhimu wa uchaguzi wa urais wa Marekani kwa kuwa utaamua mtu ambaye anashikilia madaraka mengi ya kiutendaji mikononi mwake kwa njia ya kipekee nchini Marekani, na hivyo kufurahia kiasi kikubwa cha nguvu milele, kwani Marekani ni nchi yenye nguvu zaidi ulimwenguni.

Mwandishi alilinganisha uchaguzi wa rais wa Marekani na chaguzi nyingine za Marekani, kama vile uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi na Seneti, na kulinganisha na uchaguzi wa bunge ambao hatimaye hupelekea uteuzi wa waziri mkuu ndani ya serikali ya muungano katika baadhi ya nchi kama Uingereza. Alilinganisha nafasi ya rais wa Marekani na wakuu wengine wa nchi, kulingana na kile kilichoelezwa katika katiba ya Marekani na katiba za nchi nyingine.

"Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatenda kama rais wa Marekani kwa sababu ana haki kamili ya kuunda serikali, lakini hiyo sio kulingana na katiba ya nchi yake," alisema Timothy Garton Ash.

Katika kitabu chake, 'Rais na Watu,' mwanasayansi wa kisiasa Cory Brettschneider anatukumbusha hatari kubwa ya mkusanyiko wa madaraka mikononi mwa rais, ambayo Patrick Henry, mmoja wa mashujaa wa Vita vya Mapinduzi ya Marekani, hapo awali alisisitiza wakati wa majadiliano ya Katiba ya Marekani katika mkutano wa Virginia mnamo 1788. Henry aliuliza, 'Ni nini kingetokea ikiwa rais wa Marekani angekuwa mhalifu na kutumia mamlaka yake kamili ya kiutendaji kama mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu wa majeshi kuendeleza matarajio yake ya uhalifu?''

Mwandishi aliongeza kuwa kile Henry alionya katika maswali yake kilitimia miaka 236 baadaye, kama mhalifu aliyehukumiwa alisimama bega kwa bega na mgombea mpya wa Chama cha Democrat, Kamala Harris.

Lakini haiishii hapo. Chama cha Republican na mgombea wake, ambaye mwandishi anamwelezea kama "mfungwa aliyehukumiwa" na "hatari kwa Marekani na ulimwengu," anakishinda chama cha Democratic katika njia yake ya kushughulikia masuala matatu muhimu yanayoendesha uchaguzi wa rais wa mwaka huu: uchumi, uhalifu, na uhamiaji. Hii inaashiria kuwa mamlaka haya yote ya kiutendaji yanaweza kutawaliwa na mtu ambaye, kwa mujibu wa mwandishi, ni hatari kwa nchi.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi