Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Safari ya kisiasa ya Raila Odinga
Mgombeaji wa urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga amepoteza kiti cha urais kwa mara ya tano hapo jana baada ya mpinzani wake,William Ruto kutangazwa mshindi baada ya kupata kura 7,176,141 au (50.49%) na kumshinda Raila Odinga wa Azimio, aliyepata kura 6,942,930 au (48.85%).
Safari ya Odinga katika siasa imekuwa vipi? Huu hapa msururu wa matukio ya safari ya Odinga katika siasa za Kenya
Azaliwa mwaka wa 1945
1970: Raila Odinga arejea Kenya baada ya kusoma nje ya nchi
1971: Alianzisha Standard Processing Equipment Construction and Erection Limited (baadaye ilipewa jina la East African Spectre)
1982: Alishtakiwa kwa uhaini na kuzuiliwa kwa miaka 6
1988: Alikamatwa kwa kujihusisha na kampeni za vyama vingi
1990: Alikamatwa tena baada ya kuachiliwa kwake tarehe 12 Juni 1989
1991: Alipoachiliwa, alikimbilia Norway kwa hofu ya kuuawa
1992: Alirudi kutoka uhamishoni, na kujiunga na chama cha (FORD)
-Aligombea kwa mara ya kwanza kama mbunge na kushinda kiti cha ubunge cha Langata
-Kujiondoa FORD-K na kuanzisha National Democratic Party (NDP)
1997: Aligombea urais na kushindwa
-Aliongoza muungano kati ya NDP na KANU
2001-2002: Aliwahi kuwa Waziri wa Nishati
2002: Aliunda LDP, wanaungana na National Alliance Party of Kenya (NAK) kuunda NARC iliyomshinda Uhuru Kenyatta katika kura ya 2002.
2005: Raila aliongoza kambi ya ‘Orange’ kupinga katiba iliyopendekezwa
2007: Aliwania urais kwa mara ya pili chini ya ODM na akawa wa pili
2008: Alikuwa Waziri Mkuu wa pili wa Kenya
2013: Aligombea urais kwa mara ya tatu kwa tiketi ya CORD, alishindwa na Uhuru Kenyatta.
2017: Aliwania urais kwa mara ya nne kwa tiketi ya NASA na kushindwa na Uhuru Kenyatta
-Odinga alifanikiwa kupinga ushindi wa Uhuru mahakamani, ushindi ukatangazwa kuwa batili na hivyo kulazimisha marudio ya uchaguzi, Odinga alijiondoa kwenye marudio ya uchaguzi.
-Raila alijiapisha kama "rais wa watu"
2018: Raila-Uhuru aliamua kufanya maridhiano na Kenyatta mbele ya mamilioni ya Wakenya kupitia ‘Handshake’
2022: Aliwania urais kwa mara ya tano kwenye muungano wa Azimio la Umoja - na kumaliza wa pili nyuma ya William Ruto wa chama cha UDA