'Sikujua kwamba maambukizi katika kifua changu ilikuwa saratani ya damu'

Sophie Wheldon, 24, kutoka West Midlands nchini Uingereza, alisema alipuuza ugonjwa wake wa kifua uliokuwa ukimsumbua, maumivu ya kichwa na shingo vilivyokuwa vikimpa msongo wa mawazo alipokuwa akisoma.

Lakini baada ya kuonana na daktari wake na kisha kwenda hospitalini, aligunduliwa kuwa ana ugonjwa wa damu mwaka 2018.

Kwa mujibu wa taasisi ya Lukemia UK inasema chini ya 1% ya watu wanaweza kutambua dalili za Saratani ya damu (Leukemia), wakati watu 28 hugunduliwa kila siku nchini humo.

Takriban watu laki tano waligunduliwa kuwa na saratani ya damu kote ulimwenguni mnamo 2020, kwa mujibu wa Mfuko wa Kimataifa wa Utafiti wa Saratani.

Dalili nne kati ya zilizoripotiwa sana ni pamoja na

  • Uchovu
  • Michubuko
  • Kutokwa na damu isiyo ya kawaida
  • Maambukizo ya mara kwa mara

Leukemia UK imeungana na shirika la kutoa misaada la Leukemia Care kuwataka watu kufahamu dalili zinazowezekana, wakisema kutambua mapema kunaweza kuokoa maisha.

Wheldon alikuwa akisomea biolojia mwaka 2018 alipokuwa akiumwa na daktari wake akamshauri aende hospitali kwa uchunguzi, akimuonya kuwa maumivu ya shingo yake yanaweza kuwa homa ya uti wa mgongo.

Alisema aliishia kuonana na kidtengo cha dharura A&E hadi kuhamishwa mara moja kwenye wodi "kuu" na vipimo vya damu kila saa, CT scan ya mwili mzima na "ninachojua sasa ni ilikuwa uchunguzi wa uboho".

Baada ya uchunguzi wa biopsy, dalili zake ziliendelea na alirudi kuonana na daktari kwa ushauri ambapo alijigundua kuwa "aliwekwa kwenye kundi la wagonjwa mahututi" hadi pale alipoambiwa kuwa anaweza kustahili aina fulani ya matibabu - tiba ya CAR-T.

Mchakato huo unahusisha kuchukua sehemu ya mfumo wa kinga ya mtu na seli nyeupe za damu na kuzitengeneza ili kutambua na kulenga seli za saratani, Bi Wheldon alisema.

Wheldon alisema alikuwa mtu wa kwanza katika eneo lake kupata matibabu hayo, ambayo ilikuwa siku moja baada ya siku yake ya kuzaliwa kutimiza miaka 21Juni 2019.

"Wakati [seli] ziliporudi, kulikuwa na mfuko huu mdogo - huo ndio ungeokoa maisha yangu," alisema. "Kuwekwa kwa sekunde 20 - unaweza ukapata wazimu sana kufikiria kwamba inawezekana."

Baada ya kuchunguzwa damu yake mara kwa mara, alisema aliambiwa mnamo Julai 2019 "imeondolewa kabisa", ambayo alisema ilikuwa "siku bora zaidi kuwahi kutokea".

Mfumo wake wa kinga umeathiriwa na matibabu, lakini alisema "anashukuru kuwa hapa" na akawataka watu kufahamu ishara za dalili.

"Dalili za saratani ya damu zinaweza kuwa zisizoeleweka na kupuuzwa kwa urahisi, lakini daima amini hisia zako," aliongeza.